Wakuu,
Kuna video nilikutana nayo huko mtandaoni (nimeangalia sijaiona), huyo dada alikuwa anasimulia jinsi rafiki yake alivyokufa baada ya kung'atwa chura. Chura huyo alikuwa ndani ya kiatu chake, wakati anavaa hakumuona, basi huyo chura akamng'ata kwenye kidole baada ya kushtuka (unajua jinsi wadada tunaogopa wadudu) akamtoa kwenye kiatu na kuvaa na kuendelea na kazi zake.
Baada ya siku mbili yule dada akaumwa, homa kali ikamshika kumpeleka hospitali ndio ikaonekana ni hiyo sumu ya chura, na imeshambaa mwilini kiasi ambacho hakuna msaada tena. Mwisho dada alikuwa anakoroma kama chura (kama vile inavyotokea mtu aking'atwa na mbwa mwenye kichaa) mwishowe akafa.
Sasa wakuu mimi nauliza, hawa chura tunaopishana nao majumbani ndio...