UZUSHI Kim Jong Un awashauri Waafrika waanze kutafuta Dini zao ili waendelee

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu,

Nimekutana na taarifa imepostiwa na Times FM ikiwa na maneno yanayodaiwa kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim kuwa anashangaa jinsi wazungu walivyofaulu kuwaaminisha Waafrika kwamba mitala ni dhambi lakini LGBTQ+ ni haki ya binadamu. Waafrika wanapaswa kujifunza jinsi ya kufuata dini zao. Hadi siku Waafrika wakifuata utamaduni wao wenyewe, dini za kigeni wakizikumbatia hawataweza kamwe kujiendeleza.

Naomba kufahamu ukweli wa taarifa hii, maana nimependa sana haya maneno nataka niitumie sehemu.

UZUSHI TMFM.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na taarifa inayosambaa mtandaoni ikimnukuu Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuwa anashangaa jinsi wazungu walivyofaulu kuwaaminisha Waafrika kwamba mitala ni dhambi lakini LGBTQ+ ni haki ya binadamu.

Aidha, taarifa hiyo inafafanua zaidi kuwa Waafrika wanapaswa kujifunza jinsi ya kufuata dini zao. Hadi siku Waafrika wakifuata utamaduni wao wenyewe, dini za kigeni wakizikumbatia hawataweza kamwe kujiendeleza.

Kwa mujibu wa mdau wetu Heparin aliyenzisha mada hii, taarifa hii ameiona kwenye kukurasa kwa Mtandao wa Kijamii wa Times FM, redio iliyo na Makao yake makuu Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Hadi JamiiCheck inaanza kushughulikia mada hii, watu 3763 walikuwa wameipenda (Likes) huku maoni 581 yakitolewa kwenye mjadala ulioihusisha.

Ukweli wake upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini taarifa hii si ya kweli kwani haijachapishwa na chombo chochote kikubwa cha kuaminika pia chanzo cha taarifa husika hakijawekwa wazi.

Pia, utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo ya Google Image Search, ueonesha kuwa taarifa hii imekuwepo mtandaoni kwa muda mrefu. Mathalani, iliwahi kupostiwa hapa mwaka 2020.

Aidha, taasisi zingine za uhakiki wa taarifa ziliwahi kuikanusha taarifa hii. Rejea taarifa ya Code for Africa ya Septemba 5, 2022 pamoja na taarifa ya The Star ya May 6, 2022 zote kwa pamoja zikikanusha madai haya.

Kwa ukubwa wa taarifa hii ulivyo, JamiiCheck inaamini ingevuma na ingepatikana kirahisi kwenye vyombo vya habari vikubwa.
Sawa. Lakini hata kama hakusema hivyo, ni kweli kabisa kwamba waafrika dini ni za kuletewa. Hatuna dini zetu zinazoambatana na tamaduni zetu. Tumechukua au tuseme tumelazimishwa dini na tamaduni za watu wengine!

Tunaenda kuhiji Yerusalem na Maka! Wahindi wana dini (Hinduism, Sickism) na utamaduni wao. Wachina, wajapani wana dini (budhism) na utamaduni wao n.k. waafrika tunasikiliza na kufuata kutoka nje! Maendeleo yatakuwa magumu sana mpaka hapo tutakapotambua kutokuwa wafuataji!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom