JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame. Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri. Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.
Salaam Wakuu, Nimekutana na stori mtaani zinadai kwamba mnamo mwaka 1990 Bondia Maarufu Muhamedi Ali alienda nchini Iraq kuzungumza na rais wa nchi hiyo wakati huo Sadam Hussein kuwaachia mateka wa Marekani na kufanikiwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu sakata hili? Tunaombeni ufafanuzi ====== Muhammad Ali alizaliwa mnamo 17 Januari 1942 na alifariki 3 Juni 2016. Muhammad Ali alikuwa mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani. Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964. Baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975 Ndipo alipobadili jina na kuanza kufahamika kama Muhammad Ali. Alipata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara...
Matumizi ya tumbaku ni moja ya maafa ya afya ya umma yanayojulikana sana. Licha ya ripoti nyingi kuhusu afya ya umma, matumizi ya tumbaku yanazidi kuongezeka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takriban watu Bilioni 1.3 duniani wanavuta sigara ambapo 80% kati yake wanatoka kwenye nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati. Aidha, takriban watu Milioni 7 hupoteza maisha kutokana na athari za moshi wa sigara unaotokana na kuvuta sigara moja kwa moja au pia kuvuta moshi uliotolewa na mvutaji wa Sigara. Tumbaku huathiri karibu kila kiungo na mfumo katika mwili, ikisababisha matatizo mbalimbali kama vile saratani, Magonjwa ya mfumo wa upumuaji, Ugonjwa wa Mishipa ya Moyo, Kiharusi...
Kuna picha nimeona Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama akizindua uidhinishaji wake wa mwisho wa mgombea urais 2022 nchini Kenya ambapo alionesha wazi kumuunga mkono Naibu Rais Ndugu William Ruto. Barack Obama ana vinasaba vya Ujaluo, sijui ilikuwa vipi akashindwa kumuunga mkono Mjaluo mwenzio Mwamba Raila Amolo Odinga. Chanzo: BBC === Video halisi iliyotumika kutengeneza picha hiyo
Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza kuchubua utumbo. Sasa hii ya kuambukiza kwangu imekuwa mpya sana, tena mwandishi alifafanua zaidi kuwa eti iwapo mwenza wako ana ulcers basi uwezekano wa wewe kuupata ni mkubwa maana anaweza kukuambukiza.
Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha 1. Tembelea Google Image Search Fungua kivinjari chako na nenda kwenye ukurasa wa Google. Bonyeza kwenye sehemu ya 'Images' au 'Picha' kwenye ukurasa wa kwanza wa Google, au ingiza 'Google Image Search' moja kwa moja kwenye sanduku la utafutaji wa Kifaa chako 2. Ingiza Picha Kuna njia kadhaa za kuingiza picha kwenye Google Image Search: Bonyeza kitufe cha kamera kilichopo kwenye sanduku la utafutaji ili kuwezesha utafutaji wa picha kwa kutumia kamera. Kama picha unayo kwenye kifaa chako, unaweza kuiweka moja...
Mara nyingi nikiwa na stress na kupelekea kukosa usingizi, huwa navuta sigara ili kupunguza stress hizo. Hata iwe usiku wa manane nitajitahidi niende kwenye Club zinazokesha nikafuate sigara. Suala la kuwa inanisaidia au lah, sidhani lakini pale napokuwa navuta huwa nakuwa katika hisia nyingine kabisa. Chanzo cha kutumia sigara kama relief ya stress, ni baada ya kuona kwenye muvi mara kwa mara, na ushauri kutoka kwa marafiki. Nachotaka kujua kitaalam ni kama kweli sigara inasaidia kupambana na msongo wa mawazo tunaokumbana nao mara kwa mara.
Baada ya Afrika, bara la Amerika Kusini ndilo lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takriban milioni 120. Nchi ya Argentina inatajwa kuwa mpaka sasa watu weusi ni chini ya laki mbili wakiwa takriban asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800. Inadaiwa watu weusi baada ya kuisaidia Argentina kupigana vita na maadui zake, watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague” ambapo serikali iliwanyimwa huduma muhimu hivyo upelekea vifo vyao. Zitto kupitia ukurasa wake wa Twiiter aliwahi kumhoji jamaa kuhusu kuishabikia Argentina, nanukuu 'Una support argentina ambayo...
Kumekuwepo na barua inayiosambaa Mtandaoni ikionesha kuandikwa na Mfalme Mswati III ametoa tangazo linalodai kuwa kutokana na uhaba wa Wanaume kwenye nchi yake, amewaomba wananchi wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara kuomba uraia kwenye nchi yake, na kila mwanaume atayeoa walau wanakwake 5 atamlipia gharama za harusi zao pamoja na kuwanunulia nyumba. Ukweli wa taarifa hii upoje?
Katika pitapita mitandaoni nimekutana na huyu chawa wa Mtoto wa Rais Museveni, Kainerugaba Muhoozi akimtuhumu Kakwenza Rukira kuingia makubaliano ya siri na umoja wa Ulaya nchini Uganda katika kuhamasisha ushoga nchini humo. Nakumbuka Uganda imezuia mahusiano ya jinsia moja na Rais Museveni amebana kweli kweli wazungu hawana pa kupumulia, naona wameamua kupitia njia za panya kuleta ushenzi wao.
Back
Top Bottom