JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Jukwaa la Jamiicheck lipo mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa ili kujua kama ni kweli, uzushi au nadharia. Hukuwezesha raia kufanya uhakiki kwa kuweka maudhui ndani ya jukwaa yanayotakiwa kuhakikiwa na kutoa mchango wa kuhakiki taarifa hizo kwa kile wanachokifahamu. Je, ungependa Jamiicheck ihakiki jambo gani la kijamii ili upate kujua uhalisia wake?
Umewahi kunywa sumu yoyote ile kimakosa kisha baadhi ya watu wakakushauri utumie maziwa fresh kama sehemu ya tiba? Madai ya maziwa fresh kuwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini yamekuwepo wa muda mrefu. Katika kujadili ufanisi wake, mdau mmoja wa JamiiForums amekosoa vikali tiba hii kwa kusema kuwa maziwa hayana uwezo wowote katika kuondoa sumu. Amewashauri watanzania kuacha kufanya mambo kwa mazoea pasipo kuwa na uhakika kwanza wa jambo husika. Taarifa za kitabibu zinasemaje kuhusu nadharia ya uwezo wa maziwa katika kudhibiti/kutibu sumu mwilini? Kwa muda mrefu kumekuwa na imani kwamba pale ambapo mtu amepita kwenye vumbi, au amevuta hewa chafu yenye moshi au vumbi jingi basi atakunywa maziwa kwa imani kwamba anakunguza uwezekano wa...
Haya mambo yasikie tu, watoto wetu siku za shule huwa wanalazimishwa kulala tu punde wamalizapo kula. Hii ni hatari kwa mujibu wa tafiti za afya. Uelewa mdogo na kutojali kwa wazazi kunaweza kupelekea watoto wetu kupata madhara hapo mbeleni. Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii si nzuri kiafya, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wansayansi wa chuo kikuu cha Loannina Medical watu wanaosubiri kulala kwa muda kidogo mara baada ya kula wana nafasi ndogo ya kupata ugonjwa wa mshtuko na hii ndio sababu inashauriwa kukaa masaa mawili mara baada ya kula ndipo kulala.
Kukua kwa utandawazi kumepelekea wimbi la uzwalishwa wa taarifa potofu kuongezeka zaidi licha ya kuwepo tangu awali. Katika kukabiliana na wimbi hili zipo njia mbalimbali ikiwemo kuhakiki chanzo cha taarifa na kuuliza kwenye jukwaa la uhakiki kama hili la JamamiiCheck. Huwa unatumia mbinu gani kutambua uhalali wa taarifa unazokutana nazo mtandaoni kabla ya kuziamini?
Wote mnaweza kufikiria ni namna gani mtu asiye mkazi au mfanyakazi au mwenye appointment kwenye makazi rasmi ya Malkia wa Uingereza angeweza kupenya bila kuonekana, akafanikiwa kuingia ndani ya jumba hilo, akapiga misele kidogo, akaingia ofisi ya Malkia Elizabeth kufyonza mvinyo maalum wa Malkia, na mwisho wa siku akazama ndichi kwenye hiyo room ya Malkia na kumkuta Malkia akiwa katikati ya njozi tamu, akaketi pembeni yake na kumsubiri Malkia aamke ili wayajenge/wapeane maelekezo. Basi kunaye dogo mmoja alileta makwaru na kufankiwa mpaka Malkia mwenye alipomsanukisha. Inadaiwa tukio hilo lilisababisha ulinzi zaidi uimarishwe na baadhi ya walinzi walifukuzwa.
Viongozi wanaweza kupotosha umma kwa njia mbalimbali ili kujiongezea umaarufu na kukubalika kwa wananchi. Mojawapo ya njia wanazoweza kutumia ni kutoa ahadi ambazo hawawezi kutekeleza au kuficha ukweli ili kuepuka lawama. Aidha, wanaweza kutumia propaganda na mawasiliano ya kisiasa yenye kuleta hisia za uaminifu na ufanisi, hata kama si kweli. Wakati timu ya wahakiki wa Maudhui (Fact Checker) wa The Washington Post ilipoanza kwanza kuhesabu madai ya uzushi au yenye kudanganya ya Donald Trump, ilirekodi madai 492 ya kutiliwa shaka katika siku 100 za kwanza za urais wake. Novemba 2 pekee, siku kabla ya kura za 2020, Trump alitoa madai ya uwongo au yenye kudanganya 503 aliposafiri kote nchini katika jitihada za kuomba kura akitaka...
Kukoma hedhi ni wakati ambapo mzunguko wa hedhi wa mwanamke hukata. Ki kawaida hutokea mwanamke anapokaribia umri wa miaka hamsini. Wakati hedhi inapokaribia kukata, wanawake hupitia dalili mbalimbali kama mzunguko wa hedhi usio wa kawaida, matatizo ya kihisia na ya kimwili ambayo hawajawahi kuyapata. Mwanamke akinyanyua vyuma vizito (Chanzo: Adobe Stock) Kuna nadharia kwamba wanawake wanaofanya mazoezi ya kutunisha misuli na kunyanyua vyuma vizito vinaweza kusababisha mwanamke kufika (menopause) mapema kabla ya umri wake. Umri wa mwanamke kufikia kikomo cha hedhi ni umri wa 50.
Nimekuwa nikisikia kuwa wabunge wetu hawalipi kodi kwenye mshahara mnono wanaopata. Kuwa walimu wanalipwa Tsh 400,000 lakini kamshahara hako kanaliwa na PAYE. Wabunge wetu wakiwa kwenye vikao, sitting allowance na Perdiem wanakunja 470,000 kwa siku, Mshahara wa mwisho wa mwezi nao mnono hatari. Je, hakuna sababu ya wabunge kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi? Tena napendekeza hata yale marupurupu wanayopata nayo yakatwe kodi.
Back
Top Bottom