Umewahi kunywa sumu yoyote ile kimakosa kisha baadhi ya watu wakakushauri utumie maziwa fresh kama sehemu ya tiba?
Madai ya maziwa fresh kuwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini yamekuwepo wa muda mrefu. Katika kujadili ufanisi wake, mdau mmoja wa JamiiForums amekosoa vikali tiba hii kwa kusema kuwa maziwa hayana uwezo wowote katika kuondoa sumu.
Amewashauri watanzania kuacha kufanya mambo kwa mazoea pasipo kuwa na uhakika kwanza wa jambo husika.
Taarifa za kitabibu zinasemaje kuhusu nadharia ya uwezo wa maziwa katika kudhibiti/kutibu sumu mwilini?
Kwa muda mrefu kumekuwa na imani kwamba pale ambapo mtu amepita kwenye vumbi, au amevuta hewa chafu yenye moshi au vumbi jingi basi atakunywa maziwa kwa imani kwamba anakunguza uwezekano wa madhara yanayoweza kujitokeza kwa vumbi hilo kuingia kwenye mfumo wa hewa?
Je, kuna uhusiano wowote kati ya kunywa Maziwa na kusafisha mfumo wa hewa dhidi ya madhara yatokanayo na vumbi na moshi?

- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa Idara ya Chakula ya Marekani (USDA), maziwa ni chakula chenye utajiri mkubwa wa virutubisho vinavyohitajika kwa ukuaji bora wa binadamu.
Huwa na madini chuma, protini, nishati, sukari, calcium, magnesium, sodium, zinc, folate, choline pamoja na virutubisho vingine muhimu kwa afya.
Nadharia ya sumu pamoja na tiba zake
Sumu ni kitu chochote kilicho kwenye hali ya kimimika, gesi au yabisi chenye kuleta hatari kwa afya baada ya kupakwa, kumezwa, kuingizwa au kuvutwa mwilini kwa njia ya hewa.
Chakula, madawa pamoja na vinywaji vya kawaida vinavyotumika kila siku vinaweza kugeuka pia kuwa sumu ikiwa vitatumika kwa namna isiyofaa. Hivyo, sumu isiangaliwe kama kemikali mbaya pekee, bali kitu chochote kile chenye uwezo wa kuamsha au kupoozesha mifumo na kinga za mwili hasa kinapotumika vibaya.
Kitaalam, kila aina ya sumu huwa na tiba yake ambayo kwa lugha za kitabibu huitwa Antidotes. Huu ni kama ufunguo kwenye kufuli, ukimaanisha kuwa ni aina moja tu ya funguo ndio inaweza kufungua kufuli husika.
Mfano, sumu ya paracetamol (panadol) hutibiwa kwa N-Acetylcysteine, chuma kwa Deferoxamine, baadhi ya dawa za kulevya kwa Naloxone, Benzodiazepines kwa flumazenil, sumu ya nyoka kwa Anti snake venom, virusi vya mbwa na Anti rabies.
Pia, sumu nyingi za viwandani mathalani Arsenic hutibiwa kwa D-Penicillamine, cyanide kwa Hydroxocobalamine pamoja na copper kwa methylene blue.
Hii inatoa maana kuwa, matibabu ya sumu ni jambo la kuangaliwa kwa tahadhari kubwa kwani siyo kila njia au tiba hufaa kwa aina zote za sumu.
Maziwa katika kutibu sumu
JamiiForums imebaini kuwa Maziwa hayana tofauti na maji katika kutibu sumu. Ni kimiminika kisicho na uwezo wowote katika kuokoa uhai wa mtu aliyekufa kutokana na kumeza aina fulani ya sumu. Pia, hayana uwezo wa kuzuia madhara endelevu ya sumu husika.
Imani ya kunywa maziwa baada ya kumeza dawa kimakosa, kuvuta vumbi au kemikali yoyote kwa lengo la kuepusha madhara haina mantiki kisayansi. Kwa kuwa maziwa huwa na kampaundi fulani hai zenye nguvu kubwa ya kutengeneza muunganiko, unywaji wa maziwa unaweza kusababisha hatari kubwa zaidi ikiwa aina ya sumu husika itakuwa na kampaundi shikizi, zenye uwezo wa kuungana na maziwa.
Kwa maana hiyo, mgonjwa aliyemeza sumu anapaswa kuwahishwa mapema hospitalini ili achunguzwe na kupatiwa msaada wa haraka kuokoa uhai wake.
Huduma ya kwanza kwa mhanga wa sumu
- Usimlazimishe mgonjwa kutapika, unaweza kuziba mfumo wa hewa na kusababisha kifo.
- Kama hapumui, msaada wa usaidizi wa upuaji (CPR) wa haraka unahitajika.
- Kama kameza hiyo sumu, akorogewe na kunyweshwa mkaa uliounguzwa kwenye hewa (Activated charcoal)
- Kama sumu ipo kwenye macho, yasafishe haraka kwa maji tiririka kwa dakika 20.
- Kama sumu ipo kwenye ngozi, mvue nguo alizovaa, kisha msafishe kwa maji safi kwa dakika zisizopungua 15.
- Kama kaivuta kupitia hewa, mhamishie kwenye eneo lililo na hewa safi.