JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kumekuwepo na madai yanayosambaa mtandaoni kuwa makasha ya dawa za meno huwa na rangi (code) za aina mbalimbali zinazofafanua aina ya kemikali zilizotumika kutengenezea dawa hiyo. Aidha, madai hayo yanafafanua zaidi kuwa kemikali husika ni hatari kwa afya na husababisha saratani, na kwamba makampuni yanayozalisha dawa hizi hayawezi kukupa siri hii. Ukweli wake upoje?
Habari, Ninanukuu kutoka kwenye meseji iiyotummwa kwenye kundi moja la Telegram ambalo mimi pia nimo. Huku mitaani kuna taarifa kuwa kuwa uvunaji wa damu unaifanyika maeneo mbalimbali nchi huwa siku hizi hawatupi damu yoyote hata kama wataikuta ina ugonjwa wowote kwa kuwa damu hiyo wata muongezea mtu mwenye ugonjwa ulipo kwenye damu, mfano wakakuta damu waliyovuna ina virusi vya ukimwi hawaitupi akija mgonjwa mwenye ukimwi basi wata muongezea damu hiyo je hii ni kweli? Inasadikika hili limechangiwa na ugumu wa kupata damu lakini pia hakuna shida yoyote mfano mtu ana virusi vya UKIMWI akiongezewa damu ya virusi vya UKIMWI kwa kuwa tatizo lake hapo ni damu si salama au isiyo salama, eti hata kama wangemuongezea damu iliyo salama bado...
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa. Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo. Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.
Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo. Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika. Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya...
Habari Jamiichek Kwa muda sasa katika Jamii yetu ya Kiswahili kumekuwa na hii nadharia kwamba mwanaume akitumia pombe Kali Aina ya konyagi au k vant halafu akaenda kufanya mapenzi, hutumia muda mrefu Sana kufika mshindo kitu ambacho inasemekana kinaridhisha wanawake kiurahisi. Huku mitaani, nimeshuhudia vijana wengi wakiingia katika mkumbo huu wa matumizi ya pombe Kali kwa lengo wakashiriki mapenzi na wanawake zao na kuthibitisha uanaume wao, tena kulingana na wimbi kubwa la tatzo la upungufu wa nguvu za kiume imefanya pombe hizi kupendwa na vijana wengi zaidi Sasa ni vema Jamiichek na madaktari wa mambo ya uzazi hasa kwa wanaume mjitokeze mtoe ufafanuzi zaidi. --- Chanzo cha picha: Getty Images
Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri Mambo ya Ndani mwaka 1977 na Nafasi yake kuchukuliwa na Mzee Natepe. Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka Waziri Mzee Mwinyi kutoka katika nyumba ya Waziri arudi kwao Zanzibar ili yeye aweze kuishi hapo kama Waziri. Ilikuwa shida kidogo maana Mzee Mwinyi bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka. Nasikia Mzee Mwinyi ilibidi atoke hivyo hivyo bila kujiandaa lakini siku anatoka pale nyumbani alizuiwa na Mzee Natepe kuchukua mabati na mifuko ya simenti aliyokuwa amenunua kwa pesa zake mwenyewe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi. Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya Serikali. Kweli Mzee Mwinyi akaviacha akaondoka. Baada ya miaka kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa...
Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni: 1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa). 2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende. 3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake. 4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.
Wakuu, Nimekutana na taarifa imepostiwa na Times FM ikiwa na maneno yanayodaiwa kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim kuwa anashangaa jinsi wazungu walivyofaulu kuwaaminisha Waafrika kwamba mitala ni dhambi lakini LGBTQ+ ni haki ya binadamu. Waafrika wanapaswa kujifunza jinsi ya kufuata dini zao. Hadi siku Waafrika wakifuata utamaduni wao wenyewe, dini za kigeni wakizikumbatia hawataweza kamwe kujiendeleza. Naomba kufahamu ukweli wa taarifa hii, maana nimependa sana haya maneno nataka niitumie sehemu.
Back
Top Bottom