UZUSHI Barua ya Kampuni ya Pepsi kudai Tsh. 30,000 kwa waajiriwa wapya

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Habari wakuu naomba uthibitisho wa hii barua kwa mwenye dondoo za kampuni ya pepsi maana imekaa kaa kitapeli.

1000025403.jpg
 
Tunachokijua
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa barua hii haijatolewa na Kampuni ya Pepsi kama inavyodaiwa:
  1. Tovuti rasmi ya Pepsi inataja Anwani ya Posta ya Shirika hilo kuwa ni 4162 na sio 24568 kama inavyoonekana kwenye barua hii.
  2. Barua pepe rasmi ya Kampuni hii ambayo hutumika kwenye matangazo mengi ya ajira zinazotolewa huwa ni sbc-recruitment@sbc.co.tz na sio gsupervisorpepsitanzania@gmail.com kama ilivyooneshwa kwenye barua
  3. Tovuri rasmi ya Kampuni hii imeweka bayana kuwa huwa haidai wala kuchukua kiasi chochote cha pesa kutoka kwa yeyote kwenye mchakato wa utoaji wa Ajira. Aidha, imewatahadharisha watu kuwa makini na uwepo wa Matangazo gushi ya kazi.
JamiiCheck imebaini pia ulipaji wa Malipo kwa njia ya Simu, kitu kinachoingeza wasiwasi wa ukweli wa barua hii. Makampuni mengi makubwa huwa na mifumo rasmi ya malipo ambayo mara nyingi hufanyika kupitia benki.

Aidha, barua hii ina makosa mengi ya kiuandishi yanayoweza kutumika kama sehemu ya uthibitisho wa kuifanya ionekane sio barua halali. Mathalani, aya ya kwanza pekee imeanza kwa kuandikwa 'Uongozi wa kampuni ya SBC TANZANIA LIMITED inapenda...'.

Kwa kutambua uwepo wa aina hii ya utapeli kupitia matangazo ya kazi, Machi 4, 2024, JamiiCheck ilichapisha mada inayofafanua jinsi ya kutambua matangazo haya na jinsi ya kuepuka kutapeliwa.

Katika nyakati hizi zenye uhaba mkubwa wa ajira ni muhimu kuwa makini ili kujiepusha na matapeli wanaoweza kutumia mwanya huu kujipatia kipato.

Attachments

  • WITO WA KAZI PEPSI.pdf
    82.1 KB · Views: 4
Watu wajifunze kusoma kiundani barua hizi. Kimsingi barua ina makosa mengi sana ya katika spelling na mpangilio wa kimantiki. Mtu yeyote mwenye akili timamu ataliona hili hata katika jina la baruapepe wanayotumia.
 
Mungu atusimamie watanganyika na ww ni msomi.



KAZI ni kipimo Cha utu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom