UZUSHI Pafyumu inaweza kutibu jeraha la kujikata

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Kumekuwa na dhana ya kwamba ukijikata na jeraha kuanza kutoka damu basi ukipulizia Pafyumu damu inakataa na kidonda kukauka.

Je, kuna uhalisia wowote? Na kwa upande mwengine kuna madhara yeyote kwenye hili?

1712672797283.png
 
Tunachokijua
Pafyumu au uturi ni kimiminika kilicho andaliwa maalumu na kuwekea harufu nzuri. Pafyumu hutumiwa na watu kukabiliana na harufu mbaya au kuondoa harufu mbaya.

Kumekuwa na tabia ya watu kupulizia Pafyumu (Uturi) kwenye kidonda au wanapopata jeraha kwa lengo la kukausha damu na kutibu jeraha.

Upi ukweli kuhusu suala hili?
JamiiCheck imewasiliana na Mtaalamu wa Afya Dkt. Norman Jonas, Daktari na Mkufunzi wa Afya ambaye amekanusha suala la pafyumu (Uturi) kuweza kutibu jeraha. Akiifafanulia Jamiicheck suala hili Dkt. Norman Jonas anasema:

Hakuna uhalisia wowote wa kuwa pafyume inatibu jeraha la kujikata, kufanya hivyo kunaweza kusababisha jeraha lingine.
Dhana hii imetokana na baadhi ya Watu kujua kuwa kuna viambatanishi vingine kwenye pafyumu ikiwemo Alcohol ambayo ni ‘disinfectant’ ambapo inaua bakteria lakini Alcohol iliyopo katika pafyumu sio disinfectant. Disinfectant kitaalam ni kama ilivyo Spirit.
Kuliko kuanza kutumia Pafyumu ambayo ina mambo mengi pamoja na Alcohol ndani yake, tumia maji kuosha kidonda hicho, au usitumie spirit ambayo ni maalum kwa vidonda wewe utumie Pafyumu!
Hivyo, kutokana na ufafanuzi wa Mtaalamu huyu wa Afya hoja inayodai kutumia uturi kunaweza kutibu jeraha haina ukweli.
Kumekuwa na dhana ya kwamba ukijikata na jeraha kuanza kutoka damu basi ukipulizia Pafyumu damu inakataa na kidonda kukauka...je kuna uhalisia wowote..? Na kwa upande mwengine kuna madhara yeyote kwenye hili?

Mkuu perfume zote component kuu ni ethanol (alcohol).

2. Kumbuka "spirit" hutumika hospitalini kuulia bacteria ambao wao kwenye vidonda ndio lango Bora zaidi la kuingilia mwilini.

3. Bila kusafisha haraka Kwa ethanol kwenye kidonda tegemea infection ya bacteria. Kuepuka hilo safisha kidonda kwa ethanol mara tu unapoumia.

4. Kama spirit huna tumia hata perfume au pombe badala yake.

5. Hapo #4, itakusaidia mno kuliko kuacha.
 
Hahahahah mimi huwa nikipata muwasho najitwanga perfume muwasho unakata

1. Uko sahihi wala usiache. Perfume ni mbadala Bora tu kama huna spirit kuzuia infection ya bacteria.

2. Perfume kama ilivyo pombe Ina component ya alcohol ndani kama ilivyo Kwa spirit.

3. Uko vizuri, perfume kama spirit huna ni heri kuliko bila bila.
 
Inaweza kufaa kwa mtoto mdogo wa miaka 6 mwenye muwasho wa mara kwa mara kumpulizia..?
 
Kumekuwa na dhana ya kwamba ukijikata na jeraha kuanza kutoka damu basi ukipulizia Pafyumu damu inakataa na kidonda kukauka...je kuna uhalisia wowote..? Na kwa upande mwengine kuna madhara yeyote kwenye hili?

Ni uwepo wa -OH group kwenye perfume ndio husaidia kufanya disinfection ya kidonda lakini si vyema kuitumia mara kwa mara...
 
Ingia town Tafuta perfume yenye ingredients za ajabu, Iliyo-expire muda wake kisha weka kwenye kidonda kibichi uje utupatie mrejesho.
kwahiyo kiongoz hyo athari yake ni kwa pafyum uliyopitiliza muda wake pekee?
 
Ukiwa na fangas kwenye vidole vya miguu dawa rahisi Ni kupuliza pafyum ukienda kulala, ukiamka asbh haku fangas Wala muwasho.
Kuna wakati ngozi ya pumb* imawasha hasa Kama Jana au juzi ulitembea na Malaya. Ukihisi huo muwasho pulizia kalale bila boxer.
 
Inaweza kufaa kwa mtoto mdogo wa miaka 6 mwenye muwasho wa mara kwa mara kumpulizia..?

Mkuu elewa nilichoandika. Miwasho si kidonda. Ipo hadi miwasho ya minyoo, hiyo nenda hospitali. Kumbuka hata hapa hii ni first aid si dawa:

1. Ethanol hutumika kuulia bacteria (antiseptic), ndiyo maana hospitalini spirit hutumika kusafishia vidonda, kusafisha mwili kabla ya opretion na pia kusafisha mwili kabla ya sindano.

2. Infection ya bacteria mwilini hupitia kwenye jeraha, vidonda yaani kwenye ngozi iliyojeruhika.

3. Hapo kwenye #1 na #2 hiyo siyo miwasho bali uwazi kwenye ngozi.

4. Zingatia kutumia spirit, ila kama huna unahitaji ethanol kusafisha kidonda kuzuia infection ya bacteria hapo (antiseptic); ni afadhali kutumia japo perfume au hata pombe kuliko kukomaa bila bila.

5. Hapo #4 ni kwa sababu ya component ya ethanol iliyoko humo ambayo ndiyo antiseptic yenyewe.

Acheni kukaza ubongo wandugu. Hili ni jambo la kitaaluma Siyo siasa.
 
Ukiwa na fangas kwenye vidole vya miguu dawa rahisi Ni kupuliza pafyum ukienda kulala, ukiamka asbh haku fangas Wala muwasho.
Kuna wakati ngozi ya pumb* imawasha hasa Kama Jana au juzi ulitembea na Malaya. Ukihisi huo muwasho pulizia kalale bila boxer.
Kwenye ngozi ya pumb* umetisha kiongozi.
 
Ingia town Tafuta perfume yenye ingredients za ajabu, Iliyo-expire muda wake kisha weka kwenye kidonda kibichi uje utupatie mrejesho.

1. Kwa nini nitafute iliyo expire ndugu?

2. Zingatia perfume inaweza tumika kama first aid mara tu baada ya kuumia kuzuia bacteria walioko around pale kupenya mwilini kama spirit Hamna.

3. Ninakazia: Ni heri kutumia perfume mara Moja unapoumia kama spirit huna kuliko kuacha.

4 Angalizo: Haya ni mambo kitalaamu, acheni kukaza ubongo kwenye msiyoyajua.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom