UZUSHI Picha ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, Wafula Chebukati akiwa kitandani anaumwa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimeona picha inasambaa mtandaoni ikimuonesha mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka ya kenya, Wafula Chebukati akiwa anaumwa, na maelezo mengine yanadai amesafirishwa kwenda Ujerumani kutibiwa.

JamiiCheck nisaidieni kuhakiki hii.
CHEBUKATI UZUSHI.jpg
 
Tunachokijua
Mei 2, 2024, Ukurasa wa Mtandao wa X wenye Jina la Jesus ulichapisha picha inayomuonesha Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati wakiwa akiwa amelala kitandani huku pembeni yake akiwepo mhudumu wa Afya.

Picha hii iliambatana na ujumbe unaobainisha kuwa Chebukati alikuwa amesafirishwa kwenda Ujerumani, na kwamba lilikuwa ni suala la muda tu kwani kitu chochote kibaya kinaweza kumtokea.

Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hii si halisi bali imehaririwa.

Hili linaweza kuthibitishwa kwa kutumia utafutaji wa Kimtandao wa Google Image Search unaoonesha asili halisi ya Picha hii.

Kwa kutumia njia hii, picha tajwa inaonekana kuwahi kutumika miaka ya nyuma ikizungumzia taarifa za kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli. Wakati huo, kichwa cha Hayati Magufuli kilipachikwa ili kuonesha ujumbe wake huku nyuma akiwemo Mke wake, mama Janeth Magufuli. Kumbukumbu zake zimehifadhiwa hapa na hapa.

Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa picha halisi hutumiwa na hospitali kadhaa kuandaa machapisho mtandaoni yenye lengo la kubainisha huduma zao. Pia, waadishi wa makala za Mtandaoni huitumia, tazama hapa na hapa.

Adm.jpg

Picha halisi: Chanzo, Mtandao
Picha ya kughushi imewekewa Kichwa cha Chebukati pamoja na mabox yenye dawa za Virusi maarufu kama TRUVADA ambacho hakipo kwenye picha halisi.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom