Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni:
1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa).
2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende.
3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake.
4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.
1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa).
2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende.
3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake.
4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.
- Tunachokijua
- Kubemenda ni nadharia inayohusishwa na udumavu wa mtoto. Ni kitendo kinacho maanisha kushindwa kukua vizuri kwa mtoto kuendana na umri wake.
Udumavu huu huhusisha maeneno muhimu ya ukuaji wa ubongo, kimo, ongezeko la uzito wa mwili na uwezo wa mwili katika kupambana na magonjwa.
Watoto wenye udumavu wa aina hii hupitia changamoto nyingi za kiafya katika makuzi yao na madhara ya changamoto hii huendelea pindi wawapo shuleni na nyakati zingine za maisha yao ya kila siku.
Ukweli upoje?
JamiiCheck imepitia baadhi ya vyanzo mtandaoni ambavyo vinaeleza hoja hiyo ni imani tu za kijamii ambazo hazina ushahidi wa kisayansi.
Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa Kitaalamu Baba na Mama wanaruhusiwa kujamiiana (kufanya mapenzi) mara tu baada ya SIKU 42 kupita tangu kujifungua.
Hii ni baada ya kukoma kwa majimaji na uchafu wa uzazi unaoitwa lochia.
Aidha, wataalamu hawa wanaeleza kuwa sababu ya mtoto kudhoofu na kutokua zinaweza kuchangiwa na mambo yafuatayo;
- Mtoto kutokupata maziwa ya kutosha (mama hanyonyeshi, au hana maziwa ya kutosha au mtoto hanyonyi)
- Uwepo wa maambukizi ya Magonjwa kama UKIMWI, magonjwa ya kuzaliwa nayo, pneumonia.
- Mtoto kukosa lishe inayofaa, yaani utapiamlo pia huwa unadhoofisha mtoto na kuleta shida kwenye Ukuaji.
Chanzo cha Nadharia hii
JamiiCheck imezungumza na baadhi ya wazee kujua sababu ya kuweka katazo la kufanya mapenzi kwa Mama anayenyonyesha.
Wanaeleza kuwa sababu zilizopelekea kusisitizwa kwa jambo hili ilikuwa ni kuepusha ujauzito wa mapema kabla mtoto hajakua vizuri na kuwafanya wanawake/ wasichana wawe waaminifu katika ndoa zao.
Zaidi ya hayo, JamiiCheck imezengumza na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dkt. Godfrey Chale anayepatikana Jijini Dar es Salaam anafafanua:
Mama anayenyonyesha anaweza kuendelea kushiriki tendo na mwenza wake kama kawaida kwa muda wote wa ujauzito kadiri atakavyojisikia na kuona inafaa kwake.
Dhana ya kuwa anaweza kumbemenda mtoto akishiriki kujamiiana sio kweli, kisayansi na kitaalam hakuna ukweli juu ya suala hilo.
Aidha, Dkt. Chale anaeleza kuwa Mama anayenyonyesha akipata ujauzito anatakiwa kuendelea kunyonyesha kama kawaida.
Anatakiwa kufanya hivyo hadi miezi mitatu ya mwisho kabla ya kujifungua, ili maziwa yakate kisha yaanze kujitengeneza mengine kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa.
Ikitokea mjamzito ameendelea kunyonyesha hadi anapojifungua, anaweza maziwa yatakosa ubora kiasi, hivyo mtoto atakayezaliwa atakosa maziwa mazuri na hivyo anaweza kukosa afya njema.
HITIMISHO
Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo na ufafanuzi Wataalamu wa Afya hoja inayodai Mama anayenyonyesha akifanya mapenzi anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto, haina ukweli.