JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Katika mitandao ya kijamii nimeona video inayohusishwa na Rais Mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, akikemea Ufaransa kuwa ni wakati wa kuondoka bara la Afrika. Video hiyo inamuonesha Rais Faye akiimbia Ufaransa kuwa "Inakuwa wakati wa Ufaransa kuinua magoti yake kutoka shingoni mwetu na kumaliza ukandamizaji huu usio wa haki. Karne nyingi za mateso, biashara ya binadamu, ukoloni, na ukoloni mamboleo vimesababisha mateso yasiyohesabika. Ni wakati wa kumaliza mzunguko huu wa ukandamizaji," Wachangiaji wengi kwenye video hizo zinazozunguka mitandaoni walionesha furaha kwamba Rais Faye ameonesha msimamo imara dhidi ya Ufaransa kulikandamiza bara la Afrika. Video hiyo inanipa mashaka.
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame. Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri. Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.
Kuna picha nimeona Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama akizindua uidhinishaji wake wa mwisho wa mgombea urais 2022 nchini Kenya ambapo alionesha wazi kumuunga mkono Naibu Rais Ndugu William Ruto. Barack Obama ana vinasaba vya Ujaluo, sijui ilikuwa vipi akashindwa kumuunga mkono Mjaluo mwenzio Mwamba Raila Amolo Odinga. Chanzo: BBC === Video halisi iliyotumika kutengeneza picha hiyo
Mara nyingi nikiwa na stress na kupelekea kukosa usingizi, huwa navuta sigara ili kupunguza stress hizo. Hata iwe usiku wa manane nitajitahidi niende kwenye Club zinazokesha nikafuate sigara. Suala la kuwa inanisaidia au lah, sidhani lakini pale napokuwa navuta huwa nakuwa katika hisia nyingine kabisa. Chanzo cha kutumia sigara kama relief ya stress, ni baada ya kuona kwenye muvi mara kwa mara, na ushauri kutoka kwa marafiki. Nachotaka kujua kitaalam ni kama kweli sigara inasaidia kupambana na msongo wa mawazo tunaokumbana nao mara kwa mara.
Kumekuwepo na barua inayiosambaa Mtandaoni ikionesha kuandikwa na Mfalme Mswati III ametoa tangazo linalodai kuwa kutokana na uhaba wa Wanaume kwenye nchi yake, amewaomba wananchi wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara kuomba uraia kwenye nchi yake, na kila mwanaume atayeoa walau wanakwake 5 atamlipia gharama za harusi zao pamoja na kuwanunulia nyumba. Ukweli wa taarifa hii upoje?
Katika pitapita mitandaoni nimekutana na huyu chawa wa Mtoto wa Rais Museveni, Kainerugaba Muhoozi akimtuhumu Kakwenza Rukira kuingia makubaliano ya siri na umoja wa Ulaya nchini Uganda katika kuhamasisha ushoga nchini humo. Nakumbuka Uganda imezuia mahusiano ya jinsia moja na Rais Museveni amebana kweli kweli wazungu hawana pa kupumulia, naona wameamua kupitia njia za panya kuleta ushenzi wao.
Habari Wadau, Nimekutana na tangazo la kazi likionesha kuwa Kampuni ya usafirishaji ya Tilisho inahitaji Wafanyakazi kwa nafasi ya Wakatisha Tiketi na wahudumu wa ndani ya Mabasi. Nimepata mashaka baada ya kuona ukilifuata tangazo hili ndani yake linahitaji usambaze link kwenye magroup ya WhatsApp na Facebook ili kuendelea hatua inayofuata. Je, kuna ukweli juu ya Tangazo hili?
Back
Top Bottom