SI KWELI Video inayomuonesha mwanaume akichapwa Zanzibar ni ya Ramadhani ya mwaka huu 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na video ya kusikitisha ikimuonesha raia anayesemekana kuwa ni raia wa Tanzania Bara akichapwa viboko na Raia wa Zanzibar kwa kosa la kula mchana wa Ramadhani. Je video hiyo ni ya mwaka huu?



1711716685283.png
 
Tunachokijua
Leo tarehe 29/03/2024 kumesambaa video (hii) ikimuonesha raia anayedhaniwa kuwa ni mtu wa Tanzania Bara alionekana anatandikwa bakora na raia wanaodhaniwa kuwa ni Wazanzibar kwa kosa la kula hadharani wakati wa mchana wa mfungo wa Ramadhani Zanzibar.

Video hii imezua taharuki ambayo imekuja siku Moja baada ya kuwapo kutoka taarifa ya Polisi Zanzibar(hii) iliyoeleza kuwakamata raia 12 siku ya 28/03/2024 kwa kosa la kula mchana wa Ramadhani.

1711715762164-png.2948161

Picha: Sehemu ya taarifa ya kukmatwa kwa watu 12
Video hii ililalamikiwa pia na Mwanachama JamiiForums Mawele aliyeleta uzi (huu) akihoji namna Zanzibar wanavyowachukulia watu wa Bara. Katika andiko hilo Mawele anahoji uhalali wa watu wa Zanzibar kuwapiha watu wasiofungwa.

Je, video hiyo ni ya mwaka 2024
Kama Mdau wa alivyoomba kujua tarehe ya video hii, JamiiCheck imefatilia video hii katika vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa video hii iliyombaa leo 29/03/2024 sio ya Mwaka huu. Taarifa yenye video hii (Soma hapa) Iliwahi kuletwa ndani ya Jukwaa la JamiiForums.com Juni 11, 2017 na Mwananchama Waziri Kivuli aliyekuwa akilalamikia kitendo kilichofanywa na wahusika walioonekana ndani ya video hiyo. Waziri Kivuli aliandika:

Huu si uungwana, mambo haya ndio huchochea hasira na visasi! Waliofanya kitendo hicho sidhani kama hata funga yao ina maana zaidi ya kujitesa kushinda njaa bure!

Aidha, JamiiCheck imebaini video hii imewekwa katika mitandao mbalimbali tangu (Juni 11 na 12, 2017). Mathalani, video hii iliwekwa katika mtandano wa YouTube kupitia Channel hii, hii na hii. Tazama kwenye picha hapa chini:
1711715928574-jpeg.2948167

Picha inayoonesha tarehe ya video hii kuwekwa YouTube​


Hivyo, licha kuwa video hii kuonesha tukio lililotokea kweli lakini kutokana na vyanzo hivyo hapo Juu JamiiCheck imejiridhisha kuwa si tukio la mwaka huu na halihusiani na habari (hii) ya 28/03/2024 inayoelezea watu waliokamtwa kwa kula mchana wa Ramadhani Zanzibar.
Mkuu wa wilaya ya Mjini Zanzibar mh Rashid Msaraka amesema clip inayotembea mitandaoni Juu ya Kijana aliyechapwa kwa kulewa mchana Mwezi wa Ramadan ni ya zamani 2017

Source: Kitenge Tv
wanaokula usiku wakati wengine wamelala , wamewakamata watu 12 ambao walilala usiku na kula mchana na kuwapeleka kwa vyombo vya sheria ....nikiriporti kutoka forodhani ni mimi dish namba7
 
Kwahiyo barua ya serikali ya kukana kuwatumia hao wanaochapa viboko wanaokula mchana ni feki?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom