Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar: Tulikamata wavuta bangi sio wanaokula mchana

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,335
5,558
WhatsApp Image 2024-04-02 at 16.48.41_515669f8.jpg

WhatsApp Image 2024-04-02 at 16.48.38_f4d7c865.jpg

Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad
Kamishna Mkuu wa Jeshi la polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad amesema hakuna sheria inayowaruhusu Polisi Zanzibar kuwakamata Watu wanaokula hadharani mchana wa Ramadhani na kusema chanzo cha msako uliofanyika ni baada ya video iliowaonesha Watu wakivuta bangi mchana maeneo ya Maisara Zanzibar.

CP Hamad ametoa ufafanuzi huo kufuatia operesheni iliofanyika Mkoa wa Mjini na kuwakamata Watu waliodaiwa kula mchana wa Ramadhan “Hakuna sheri inayokataza Watu wasile mchana wa Ramadhani, nilitoa maelekezo baada ya video ya wanaovuta bangi kwamba ifanyike oparesheni wale wavuta bangi kwasababu bangi ni kosa la jinai hakuna sheria inayoruhusu Watu kuvuta bangi ila hatukuwakamata wala mchana”

“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mampaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili ili zifanyike kwa salama na amani.”

Pia soma:
Marufuku nyingine Zanzibar soma:

Zanzibar yapiga marufuku mambo yafuatayo katika kipindi cha mwezi wa ramadhan
 
TOKA MAKTABA :

Kamanda Ataja majina na kabila za waliokamatwa wakila hadharani

View: https://m.youtube.com/watch?v=l4mmqjdRX3o
Maafisa wa polisi visiwani Zanzibar wametangaza kuwakamata watu 12 kwa tuhuma za kukiuka utaratibu wa dini ya Kiislamu kwa kula mchana hadharani kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonyesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar kula hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na wawili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.

Waliokamatwa ni pamoja na Issa Hamad Juma (40) wa Kikwajuni, Hamad Indole (25) wa Mtwara, , Hashimu Bakari Nassoro (35) wa Kwarara, Selemani Ismail Nalinga (34) wa Magogoni na wengine 8 wote wametupwa mahabusu kituo cha Polisi Madema huku uchunguzi ukiendelea kwa ajili mashitaka waweze kuwafikishwa mahakamani...
 
“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mampaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili ili zifanyike kwa salama na amani.”
Hata haeleweki anataka kusemaje! Kwahio Ile video kuwa wamekamata wanaokula mchana sio sauti zao? Na picha zao?
 
Kamishna Mkuu wa Jeshi la polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad amesema hakuna sheria inayowaruhusu Polisi Zanzibar kuwakamata Watu wanaokula hadharani mchana wa Ramadhani na kusema chanzo cha msako uliofanyika ni baada ya video iliowaonesha Watu wakivuta bangi mchana maeneo ya Maisara Zanzibar.

CP Hamad ametoa ufafanuzi huo kufuatia operesheni iliofanyika Mkoa wa Mjini na kuwakamata Watu waliodaiwa kula mchana wa Ramadhan “Hakuna sheri inayokataza Watu wasile mchana wa Ramadhani, nilitoa maelekezo baada ya video ya wanaovuta bangi kwamba ifanyike oparesheni wale wavuta bangi kwasababu bangi ni kosa la jinai hakuna sheria inayoruhusu Watu kuvuta bangi ila hatukuwakamata wala mchana”

“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mampaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili ili zifanyike kwa salama na amani”
 
Back
Top Bottom