Maadhimisho ya Miaka 10 ya ACT Wazalendo, waelezea kupigania Maslahi ya wote na Zanzibar yenye Mamlaka kamili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,842
12,045
WhatsApp Image 2024-04-15 at 16.57.40_711928da.jpg
Miaka 10 ya kupigania Maslahi ya wote na Zanzibar yenye Mamlaka kamili.

Ndugu waandishi wa habari, ACT Wazalendo inatimiza 10 tokea kuanzishwa kwake. Kilele cha Miaka 10 ya ACT Wazalendo itakuwa tarehe 5/5/2024, katika Viwanja vya Mwami Ruyagwa, Kata ya Gungu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Ndugu waandishi wa habari, Maadhimisho ya Miaka 10 ya ACT Wazalendo yatakuwa na Kauli mbiu isememayo MIAKA 10 YA KUPIGANIA MASLAHI YA WOTE NA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI ambayo inaakisi ahadi yetu kwa Watanzania ya TAIFA LA WOTE, MASLAHI YA WOTE na Ahadi yetu kwa Wazanzibari ya ZANZIBAR MPYA, ZANZIBAR MOJA, MAMLAKA KAMILI.

Maadhimisho ya Miaka 10 ya ACT Wazalendo yatafanyika katika Mwezi huu mzima wa Aprili mpaka tarehe 5 Mei 2024. Maadhimisho yatapambwa na shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Baadhi ya shughuli hizo ni kama ifuatavyo;

1. Kongamano la Vijana Zanzibar tarehe 21/04/2024 ambalo litajadili dhima na Wajibu wa Vijana Katika Kuipigania Zanzibar Mpya, Zanzibar Moja na Zanzibar Yenye Mamlaka Kamili. Kongamano hili litafanyika Unguja na kuhudhuriwa na mamia ya Vijana wa Zanzibar Pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa Chama na Wadau mbalimbali wa mageuzi nchini.
WhatsApp Image 2024-04-15 at 16.57.41_7255b279.jpg

Shangwe Ayo
2. Kutoa kwa Jamii (Corporate Social Responsibility) ambapo Pamoja na mambo mengine ya kijamii nchi nzima, Wanachama wa ACT Wazalendo Pamoja na Viongozi wa Kitaifa wataweka kambi Wilayani Rufiji kufanya huduma za kijamii kwa waathirika wa Mafuriko. Vile vile Vijana na Wanawake wa ACT Wazalendo watakusanya na kutoa Misaada kwa Wananchi wa Rufiji.

3. Mkutano wa Kidemokrasia Moshi, Kilimanjaro tarehe 27/4/2024 ambapo Wanachama wa ACT Wazalendo Nchi nzima watakutana na Kiongozi wa Chama na kujadiliana naye masuala ya Chama chao. Katika Mkutano huo wa Kidemokrasia Nembo mpya ya Chama na Bendera mpya ya Chama vitazinduliwa Rasmi na Kiongozi wa Chama Ndugu. Doroth Manka Jonas Semu.

Mkutano wa Kidemokrasia ni Kikao cha kikatiba na ni wa wazi kwa Wanachama wote watakaokuwa na uwezo wa kufika Moshi. Chama kitaweka utaratibu mzuri kufanikisha wanachama wanaotaka kuhudhuria Mkutano wa Kidemokrasia wa Mwaka huu. #TwenzetuMoshi.

4. Pamoja na ushiriki huu wa mikutano na makongamano wanachama wa ACT Wazalendo watashiriki shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kuchangia damu katika Benki ya Damu ya Taifa, Kufanya usafi kwenye masoko, Kufanya usafi kwenye hospitali na kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo. Shughuli hizi za kijamii zitafanyika kote Tanzania Bara na Zanzibar.

5. Mkesha wa ACT Wazalendo utakuwa Tarehe 04/05/2024 Makao Makuu ya Chama Jengo la Maalim Seif, Magomeni Dar es Salaam na Ofisi Kuu ya Chama Vuga Zanzibar. Mkesha huu utashuhudia kupandishwa kwa Bendera mpya za Chama.

6. Tarehe 5/5/2024 itakuwa ni kilele cha kuadhimisha miaka 10 ya ACT Wazalendo Mkoani Kigoma. Mwenyekiti wa Taifa wa Chama atapandisha rasmi bendera mpya ya Chama katika mkutano mkubwa wa hadhara. Mkutano huu utafanyika katika Kata ya Gungu na utatanguliwa na maandamano kutoka pande mbalimbali za Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya Kigoma kuelekea Viwanja vya Mwami Ruyagwa, Gungu.

Maandamano yatapokelewa na Mwenyekiti wa Chama Ndugu Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye atahutubia Taifa kutokea Kigoma na kufunga Rasmi maadhimisho ya Miaka 10 ya Chama chetu.

Chama kinatoa rai kwa wanachama wake wote na viongozi nchi nzima, Mikoa yote Tanzania kushiriki maadhimisho haya ya miaka 10 ya Kuzaliwa kwa Chama chetu kwa kufanya shughuli za kijamii na Kupandisha bendera kwenye ofisi zetu zote.

Tunatoa shime kwa Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Chama kushiriki nasi kusherehekea Miaka 10 ya mafanikio makubwa katika Ujenzi wa Demokrasia ya vyama vingi hapa Tanzania.

Imetolewa na

Shangwe Ayo
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma,
ACT Wazalendo.
15 Aprili, 2024
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom