JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Salaaam Wakuu, Nimeona katika sehemu mbalimbali picha zikisambaa zikionesha nembo inayotumika kwenye Podium ya Rais Samia haina bibi na bwana kama ambayo alikuwa anaitumia Rais Magufuli. Hili limekaaje Wakuu tunaomba ufafanuzi. Nembo anayotumia Rais Samia ikiwa haina Bibi na Bwana Nembo aliyokuwa akiitumia Hayati Magufuli ikiwa na Bibi na Bwana
Salaam ndugu zangu, Nimepata taarifa kwamba Shirikisho la soka nchini Zanzibari limeweka ugumu kwa wachezaji wa Tanzania Bara na itawasajili kama Wageni. Taarifa hii imeandikwa: Bodi inayosimamia Ligi kuu ya Zanzibar (PBZ) imepitisha kanuni mpya za Usajili kuwa Klabu yoyote itakayomsaini mchezaji kutoka Tanzania bara ataingizwa kwenye system kama Mchezaji wa kigeni kwa maana lazima akatiwe Kibali cha kuishi Zanzibar ambacho kina gharimu pesa za kitanzania laki 5. Pia kwenye klabu Moja hawatakiwi kuzidi wachezaji 9 Kwa ligi ngazi ya Mkoa Mchezaji kutoka Tanzania bara atakatiwa kibali cha kuishi na kufanya kazi kwa msimu. Mmoja ambacho kita gharimu Pesa za kitanzania Laki 3. Kwa upande wa Tanzania Bara, mchezaji akisajiliwa kutoka...
Wakuu mko vyede? Kuna kipindi fulani hili suala lilizuka sana kuwa wanaoishi na HIV hasa matajiri walikuwa wanaenda South Afrika kubadilisha damu ili kupunguza makali ya ugonjwa huo. Hii ilikuwa kweli? Maana mpaka leo naamini walikuwa wanafanya hivyo, ila swali likaja wanabadilishaje? Wanamtoa damu nusu halafu wanamuongezea nyingine ambayo haina virusi ama? Msaada wenu kung'amua hili wajuvi.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazohusisha taasisi na watu maarufu duniani kuwa na mpango wa kupunguza idadi ya watu duniani. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na Bill Gates kuelezwa kuandika katika mitandao wa kijamii akimshauri kiongozi wa World Economic Forums (WEF), Klaus Schwab juu ya matumizi ya "death panels" kupunguza watu duniani. Lakini pia, video nyingine ambayo imesambaa mtandaoni inamuonesha Mtendaji Mkuu wa Pfizer, Albert Bourla, akidaiwa kusema wanatazamia kufanikisha kupunguza idadi ya watu duniani kwa 50%. Je, taarifa hizi zina ukweli?
Inadaiwa kuwa mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi). Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada. Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya...
Back
Top Bottom