JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Wakuu, Nimekuja na swali hili baada ya jamaa mmoja kusema jambo hili sio la kweli, lakini mimi pia nimeshawahi sikia hii, bi mkubwa alituhadisia kuna ndugu yao mmoja aling'atwa na mbwa mwishowe alipokaribia kwenda kwenye ulimwengu mwingine alikuwa akibweka kama mbwa. Naamini hata wewe unayesoma hapa umeshawahi kusikia kuhusu hili. Je, suala hili ni kweli au stori tu za mtaani wataalamu wa JamiiCheck?
Magonjwa mbalimbali yametufanya binadamu kubuni tiba aina mbalimbali ambazo zitatusaidia kuondokana na magonjwa hayo. Moja ya tiba iliyobuniwa na binadamu ni pamoja na mkoja wa binadamu kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Tena unaambiwa ukipata mkojo wa asubuhi ndio kiboko ya magonjwa kama anavyosema mdau hapa wa mtandao wa JF kuwa Mkojo wa asubuhi ni dawa murua Shuhuda ni nyingi sana, moja ikiwa ni ya mdau huyu wa JF kutibu maumivu ya meno kwa kunywa mkojo wa asubuhi Miaka ya 2013-2016 nchini Tanzania kulitokea kundi la wanunuaji wa mkojo wa binadamu kwa madai kuwa unaenda kutumika kama dawa. Katika ukuaji wangu, mimi ni mmoja wa walioshawishika kutumia mkojo kwa kunywa au kupaka. Kwa kutokuzingatia suala la afya, nimewahi pia kunywa...
VVU/UKIMWI vinasalia kuwa janga kuu la afya ya Umma duniani, janga lililogunduliwa zaidi ya miaka 40 iliyopita likiwa limechukua uhai wa watu zaidi ya milioni 40.4 huku maambukizi yakiendelea katika nchi zote duniani. Hadi kufukia mwishoni mwa mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa watu milioni 39.0 wanaoishi na VVU, theluthi mbili kati yao (milioni 25.6) wakipatikana barani Afrika. Pia, mwaka 2022 pekee, watu 630 000 walipoteza maisha kutokana na sababu zinazohusiana na VVU na watu milioni 1.3 walipata VVU.
Nadhani wengi tumetizama movie ya Titanic, ikielezea penzi la vijana wawili na pia kuzama kwa meli hiyo. Inasemekana ina uhalisia kiasi fulani na tukio la kweli la kuzama kwa meli hiyo mwaka 1912. Jambo la kutafakarisha, imekuwa ikidaiwa kuwa aliyekuwa kapteni mkuu wa Meli hiyo Edward John Smith kabla ya kung'oa nanga alisikika akisema kuwa ''Hata Mungu Mwenyewe asingeweza kuzamisha hii meli'' - ( "Even God himself couldn't sink this ship") Kauli hiyo inayodaiwa kutamkwa na Kapteni wa TITANIC, imetafsiriwa na wengi kama chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu hivyo kupelekea kuwaadhibu maelfu ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo. Edward John Smith Meli ya Titanic
Kevin Carter alikuwa ni mpiga picha, sasa katika kazi zake alifanikiwa kufika Sudan na alikuta eneo fulani nchini Sudan likikabiliwa na njaa kali sana. Wakati anaendelea kuchukua matukio katika picha, alikutana na mtoto dhoofu mwenye utapiamlo aliyekuwa akikabiliwa na njaa kali pamoja na kiu, cha kusikitisha zaidi nyuma ya mtoto huyo dhoofu kulikuwa na ndege hatari aina ya TAI akimuwinda huyo mtoto ili kujipatia kitoweo. Inadaiwa Kevin Carter alipiga picha na kusepa. Inasemekana huko nyuma mtoto yule kutokana na kuwa dhoofu aliweza kuuawa kirahisi na TAI yule. Inasemekana picha ile ya Kevin Carter ilipata umaarufu sana mpaka kupata tuzo ya Pulitzer iliyoanzishwa na Joseph Pulitzer. Inadaiwa Kevin Carter umaarufu aliopata...
Covid-19 ni janga ambalo lilitikisa ulimwengu kuanzia mwaka 2019. Virusi vya korona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS). Virusi hivyo kwa mara ya kwanza viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Uzi huu utapitia baadhi ya nadharia zilizoibuka wakati huo pamoja na fafanuzi za kitalamu za nadharia hizo.
Kando ya barabara ya Iringa - Mbeya maeneo ya Njia panda ya Mlolo kuna Kaburi la mtu aliyekuwa maarufu katika fani ya Uganga wa jadi mkoani Iringa na alifahamika kama Mzee Martin Kiyeyeu. Inaelezwa mzee huyu alifariki mwaka 1974 na kuzikwa lakini muonekano wa Kaburi hilo ni kama alizikwa hivi karibuni. Inaelezwa baada ya kufariki, Mganga huyo alizikwa kwa kufuata taratibu na mira za Machifu ambapo alizikwa kwa kusindikizwa na mtu aliye hai, aliyejitolea kuzikwa naye akiwa hai ili kumsindikiza, ambapo inadaiwa mtu huyo alikaa na kumpakata Mganga huyo aliyezikwa huku akiwa amekaa. Kaburi la Mganga Martin Kiyeyeu na nyanya za umeme zilizohamishwa upande Inadaiwa kumekuwa na maajabu mengi yanayotokana na Kaburi hili ila moja maarufu ni...
Rais Mstaafu Joseph Kabila inasemekana hakuwa mtoto halisi(Biological Son) wa Rais Mstaafu Joseph Desire Kabila. Inasemekana jina halisi la Joseph Kabila ni Hypolite Kanambe Kazemberembe akiwa na asili ya Kitusi kutoka nchi ya Rwanda. Pamoja na machapisho mengi kumtambua Joseph Kabila kama mtoto halisi (Biological son) wa Hayati Joseph Desire Kabila, baadhi ya machapisho yamehabarisha kuwa baba mzazi wa Joseph Kabila Kabange anajulikana kama Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje. Maswali ambayo wakongo wengi wanajiuliza, ilikuwaje wakatawaliwa na Rais aliyezaliwa Rwanda na mwenye asili ya Kitusi kutoka Rwanda huku Moise Katumbi aliyezaliwa Congo DR na Mama Mkongo na Baba Mgiriki akiwekewa...
Katika pita pita zangu mitandaoni leo nimekutana na "Twit" inayosema kwamba Gavana wa BOT Gilman Rutihinda (1989 - 1993) alifariki kutokana na ajali ya gari mwaka 1993 kama hii tweet inavyojieleza: Hata hivyo kuna article ya Mwaka 2011 hapa katika Forum inayoelezea kifo cha Gavana Rutihinda pamoja na Waziri wa Fedha wa wakati huo Steven Kibona kwamba vilitokana na 'food poisoning' baada ya kurudi kutoka safarini India. - Sababu ya kifo cha Steven Kibona na Gilman Rutihinda Je tunaweza kupata ukweli wa vifo hivi?
Wakati wa ukuaji wangu nilikuwa nasikia matendo mabaya sana kuhusu aliyekuwa Rais wa Uganda, Id Amini Dada, moja ya matendo hayo ni pamoja na ulaji wa nyama za watu hasa waliokuwa wapinzani wake wakubwa. Rejea Idi Amin Dada : The Ugandan Butcher & Murderous Cannibal Uvumi ulienea kwamba aliweka vichwa vya wanadamu kwenye jokofu lake. Na alikiri kula nyama mara kadhaa. Kuna mahali nimeona amenukuliwa mwaka wa 1976 akisema "Nimekula nyama ya binadamu, ina chumvi nyingi, hata zaidi ya chumvi kuliko nyama ya chui." Kuna wanaosema kuwa suala la Idi Amini ni propaganda zilizozushwa na maadui zake, pia kuna waliosema ni kweli alikuwa mtumiaji mzuri wa nyama za binadamu. Aliyekuwa Rais wa Venezuela, Hugo Chavez aliwahi kunukuliwa haya...
Kijana mmoja aliejulikana kwa jina la Israel Daudi, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi 3 na askari Polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuachia ng'ombe kuingia shambani. Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Olaresho, Kata ya Olasiti katika Halmashauri ya Jiji la Arusha. Akizungumzia tukio hilo Diwani wa Kata ya Olasiti, Alex Martin amesema hilo ni tukio la pili kwa askari huyo kufanya mauaji katika Kata hiyo ya Olasiti kwani huko nyuma alishafanya mauaji na Wananchi walitaka kumuua askari huyo lakini diwani aliingilia kati kwa kumuepusha askari huyo kuuliwa na Wananchi. Lakini cha kushangaza askari huyo amerudia tena kufanya mauaji katika kata hiyohiyo. Diwani Alex ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kutotumia nguvu na mabavu kwa...
Ulaji wa viazi vitamu kwa kipindi kirefu unadaiwa kusaidia uzalishwaji wa mayai mengi kwa Mwanamke na hivyo kupelekea kupata watoto mapacha. Jiji la Igbo-Ora lililopo nchini Nigeria ni jiji lenye mapacha wengi na Nigeria imepewa jina la mji mkuu wa Mapacha Duniani kwa kuwa na watoto mapacha wengi zaidi kuliko eneo lolote duniani huku viazi vitamu vikiliwa zaidi nchini humo. Ni kweli kuwa Viazi vitamu huongeza homoni aina ya ‘phytoestrogen’ ambayo huchangia kwenye kupevusha yai zaidi ya moja kwa wakati mmoja hivyo kusababisha kuzaliwa kwa watoto mapacha?
Back
Top Bottom