NADHARIA Nadharia mbalimbali kuhusu Maambukizi na Matibabu ya VVU na UKIMWI

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
VVU/UKIMWI vinasalia kuwa janga kuu la afya ya Umma duniani, janga lililogunduliwa zaidi ya miaka 40 iliyopita likiwa limechukua uhai wa watu zaidi ya milioni 40.4 huku maambukizi yakiendelea katika nchi zote duniani.

Hadi kufukia mwishoni mwa mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa watu milioni 39.0 wanaoishi na VVU, theluthi mbili kati yao (milioni 25.6) wakipatikana barani Afrika.

Pia, mwaka 2022 pekee, watu 630 000 walipoteza maisha kutokana na sababu zinazohusiana na VVU na watu milioni 1.3 walipata VVU.

National-HIV-Testing-Week-Poster-e1665398900695.png
 
Tunachokijua
JamiiForums inakuwekea pamoja mkusanyiko wa nadharia mbalimbali zinazohusiana na maambukizi ya ugonjwa huu ili kuweka rejeo muhimu kwa sasa na baadae.

***
1. Mbu wanaweza kusambaza VVU
Miaka ya mwanzoni ya kuibuka kwa ugonjwa huu kulikuwepo na mawazo yanayodai kuwa mbu anaweza kuwa chanzo cha maambukizi. Baadhi ya jamii hadi sasa bado zinaamini madai.

Ukweli ni upi?
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha madai haya.

JamiiForums imezungumza pia na wataalam wa afya pamoja na kupitia tafiti mbalimbali za afya na kubaini kuwa Mbu hawezi kusambaza VVU.

Pamoja na ukweli kuwa wanaweza kusambaza baadhi ya magonjwa mfano Malaria, homa ya manjano na dengue, wanasayansi wamethibitisha kuwa mbu anakosa sifa muhimu za kusambaza ugonjwa huu.

Mbu hawana seli maalumu (T cells) ambazo huhitajika na virusi ili viweze kuishi na kuzaliana, hii inamaanisha kuwa hata mbu wenyewe hawawezi kuathirika na VVU/UKIMWI.

Wanapomng'ata binadamu huingiza mate yao na sio damu. Aidha, ili mbu awe na uwezo wa kupitisha VVU mwilini mwa binadamu, anapaswa kubeba kiasi cha kutosha cha virusi. Kiuhalisia, mbu hana uwezo wa kubeba kiasi kingi cha virusi kutosha kusababisha maambukizi.

***
2. UKIMWI sio ugonjwa wa zinaa
Madai ya kuwa UKIMWI sio ugonjwa wa zinaa (Ugonjwa unaosambazwa kwa njia ya ngono) yanaendelea kukubalika kwenye baadhi ya jamii duniani. Baadhi ya jamii na makundi ya watu hayaamini kuwa mojawapo ya sababu za kusambaa kwa VVU/UKIMWI ni kupitia ushiriki wa tendo la ndoa, na kwamba ugonjwa huu sio wa zinaa.

Ukweli ni upi?
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), VVU ambavyo husababisha UKIMWI vinaweza kusambazwa kupitia majimaji ya mwili kama vile damu, shahawa, maziwa na majimaji ya uke kutoka kwa mwathirika kwenda kwa mtu asiye na ugonjwa.

Kwa kuwa majimaji ya sehemu za siri kama yale ya uke na shahawa yanahusishwa na maambukizi, inaamaanisha kuwa tendo la ndoa linaweza pia kuhusika.

Taasisi ya Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC) nayo inathibitisha uambukizwaji wa VVU kwa njia ya ngono.

Taasisi za UNAIDS, NIH, NHS pamoja na tafiti nyingi za afya zote zinathibitisha kuwa UKIMWI ni ugonjwa wa zinaa, hivyo unaweza kuambukizwa kwa kushiriki tendo la ndoa kwa njia yoyote na muathirika wa ugonjwa huu.

Ni muhimu kuwa makini kuchukua tahadhari na kutokupuuza ukweli huu.

***
3. VVU (HIV) havisababishi UKIMWI
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki aliwahi kuwaandikia viongozi wa nchi zingine duniani juu ya kutokuwa na imani juu ya dhana iliyopo ya VVU kusababisha UKIMWI, na kwamba ugonjwa huo husababishwa na mambo mengine.

Mwaka 2000 alianzisha kamati maalumu ya kumshauri ambayo pamoja na mambo mengine ilikubaliana naye kuwa VVU havisababishi UKIMWI, hali iliyopelekea juhudi za watu kutumia dawa za kufubaza virusi zirudi nyuma kwa kasi kubwa pamoja na kuongezeka kwa vifo vya waathirika wa UKIMWI.

Madai haya yameendelea kusambaa hadi sasa, na watu wengi huamini kuwa ni kweli.

Ukweli ni upi?
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), VVU hushambulia seli nyeupe za damu za mwili na kudhoofisha mfumo wa kinga. Hii hurahisisha kuugua magonjwa nyemelezi kama vile kifua kikuu na baadhi ya saratani.

VVU vinaweza kutibiwa na kuzuiwa kwa tiba ya vidonge vya kufubaza virusi na kurefusha maisha (ART). VVU ambayo haijatibiwa inaweza kuendelea hadi UKIMWI, mara nyingi baada ya miaka mingi. Hivyo, UKIMWI ni hatua ya mwisho, kubwa na ya juu zaidi ya maambukizi ya VVU.

Kwa mujibu wa CDC, VVU visipotibiwa vinaweza kusababisha UKIMWI na kwamba ugonjwa huo kwa sasa hauna tiba.

Uthibitisho mwingine wa VVU kusababisha UKIMWI ni andiko lenye kichwa cha habari "The Discovery of HIV as the Cause of AIDS" la Robert C. Gallo, M.D. na Luc Montagnier, M.D. lililochapishwa kwenye jarida la Kitabibu la The New England Journal of Medicine

JamiiForums inashauri wagonjwa kutumia dawa za kufubaza virusi vizuri ili kupunguza maambukizi pamoja na kuishi maisha marefu yasiyo na changamoto nyingi za kiafya.

***
4. Kila mwenye VVU huwa na UKIMWI
Watu huamini kuwa kila mwenye virusi vya UKIMWI (VVU) huugua UKIMWI.

Ukweli upoje?
Sio kila mtu aliye na VVU huugua UKIMWI.

Kisayansi, kila mwenye UKIMWI huwa na VVU lakini sio kila mwenye VVU huwa na UKIMWI kwa kuwa UKIMWI ni hatua ya mwisho na kubwa zaidi ya maambukizi ya VVU ambayo hutokea baada ya kushambuliwa na virusi hawa pasipo kupata tiba.

Hivyo, mtu mwenye VVU akijigundua mapema na kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi huku akifuata mtindo borsa wa maisha usiofanya kuongezeka kwa maambukizi huishi umri mrefu na anaweza asipate kabisa UKIMWI maisha yake yote.

UKIMWI ni neno jumuishi linalosimama badala ya "Upungufu wa Kinga Mwilini", hali inayotokea kwa watu walioishi na VVU kwa muda mrefu bila kupata matibabu, wakati ambao mfumo wa kinga mwili huwa umedhoofika kiasi cha kushindwa kupambana na magonjwa nyemelezi.

Mtu mwenye VVU pamoja na mambo mengine huthibitika kuwa na UKIMWI baada ya seli za CD4 kushuka chini ya 200 kwa kila mililita ya damu (200 cells/mm3).

***
5. Unaweza kuambukizwa VVU kwa kutangamana na watu walioathirika
Baadhi ya Nadharia zinazotajwa kuchangia maambukizi ya VVU ni kukaa pamoja na watu wenye VVU pamoja na kushirikiana nao kwenye mambo mbalimbali ya kijamii kama vile kuvuta hewa pamoja, Kukumbatiana, kubusiana, au kusalimiana, Kutumia pamoja vyombo vya kula chakula pamoja na Kugusa kiti cha msalani, komeo la mlango na kadhalika.

Nadharia hizi zinaamikina miongoni mwa jamii nyingi, Tanzania ikiwemo.

Ukweli wake upoje?
Nadharia hizi hazina ukweli kisayansi.

VVU haviwezi kuambukiza kwa kugusana, au kushirikiana na wa watu walioathirika

Njia za uambukizwaji wa VVU zipo bayana. Kwa mujibu wa CDC, watu wengi huambukizwa VVU kwa kushiriki ngono kwa njia ya kawaida (uke) au njia ya haja kubwa, kushirikiana vitu vyenye ncha kali, kupokea damu ya mwathirika, mama kwa mtoto wakati wa kunyonyesha au kujifungua.

Jamii inaaswa kuachana na dhana hizi potofu zinazochangia uwepo wa unyanyapaa kwa watu wenye VVU.

6. Mitishamba (dawa za kienyeji) zinaweza kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI
Baadhi ya tamaduni huamini kuwa zipo dawa za kienyeji ambazo mtu akioga baada ya kufanya tendo la ndoa au kufanya ngono.

Ukweli ni upi?
Utamaduni wa utakaso ambao ulipata umaarufu katika mataifa ya jangwa la sahara na maeneo ya India na Thailand, umetajwa kuwa hatari sana.

Umesababisha wasichana kubakwa na watoto wadogo kunajisiwa hali ambayo inawaeka katika hatari ya kuambukizwa VVU.

Chimbuko la utamaduni huo linaaminiwa kuwa barani Ulaya katika karne ya 16 ambapo watu walianza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende.

Utamaduni wa matumizi ya mizizi (mitishamba) haujawahi kuthibitishwa kisayansi kutibu au hata kuzuia maambukizi ya VVU.

***
7. Baadhi ya Makundi ya damu hayawezi kuambukizwa VVU
Kumekuwa na uvumi kuwa baadhi ya makundi ya damu hayawezi kuambukizwa VVU.

Mathalani, watu husema kuwa wale wenye kundi la damu O+ hawawezi kupata maambukizi ya VVU/ UKIMWI.

Ukweli wake upoje?
JamiiForums imebaini kuwa kila kundi la damu lina hatari sawa kupata maambukizi ya VVU endapo utajiingiza kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kupata VVU, kuwa na aina yoyote ya kundi la damu siyo kigezo cha mtu kutoambukizwa virusi vya UKIMWI endapo usipozingatia tahadhari mfano; kufanya mapenzi bila kinga, kuchangia au kupokea damu isiyopimwa na wataalamu wa afya, na kuchangia vitu venye ncha kali na mtu mwenye maambukizi.

VVU haijali kundi lako la damu, wala virusi vingine. kundi la damu halitoi kinga dhidi ya magonjwa, VVU huambukiza aina zote za damu ikiwa ni pamoja na kundi la damu O.

Aina za makundi ya damu huamuliwa na antijeni kwenye uso wa seli nyekundu za damu, na seli nyekundu hazina jukumu lolote katika kuwezesha maambukizi ya VVU kwa njia yoyote. Kwasababu virusi vya UKIMWI (VVU) huambukiza seli nyeupe za damu, ambazo hazina jukumu lolote katika kuamua aina za damu.
VVU/UKIMWI vinasalia kuwa janga kuu la afya ya Umma duniani, janga lililogunduliwa zaidi ya miaka 40 iliyopita likiwa limechukua uhai wa watu zaidi ya milioni 40.4 huku maambukizi yakiendelea katika nchi zote duniani.

Hadi kufukia mwishoni mwa mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa watu milioni 39.0 wanaoishi na VVU, theluthi mbili kati yao (milioni 25.6) wakipatikana barani Afrika.

Pia, mwaka 2022 pekee, watu 630 000 walipoteza maisha kutokana na sababu zinazohusiana na VVU na watu milioni 1.3 walipata VVU.

Ahsante kwa Somo.
 
Somo limeeleweka na ndio uhalisia.
UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) kwa njia moja nyingine umekuwepo hata kabla ya janga la vvu.
Visababishi vingine ambavyo hupelekea kuwepo kwa upungufu wa kinga mwilini ni pamoja na
1. Utapia mlo mkali (severe malnutrition) kutokana na mwili kukosa lishe bora kinga za mwili hushindwa kufanya kazi na hivyo kupelekea wagonjwa wenye utapia mlo kupata magonjwa nyemelezi ambayo ni kuhara, homa ya mapafu (pneumonia) fungus za njia ya mfumo wa chakula nk
2. Saratani ni ugonjwa mwingine unao sababisha mwili kupungua kinga zake hasa hasa saratani ya damu ambapo mfumo wa kuzalisha damu kwenye uboho hushindwa kufanya kazi hivyo kupelekea mwili kukosa kinga

Kwa maana hiyo siyo VVU pekee inayoweza kufanya mwili uwe na upungufu wa kinga. Ieleweke kwamba hata akina mama wanapopata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mifumo ya mwili hupelekea kushuka kidogo kwa kinga zao na miongoni mwa ugonjwa nyemelezi kwa wajawazito ni fangas za ukeni ( vulvo vaginal candidiasis) wakishajifungua hii kadhia ya fungus huisha.
 
Kujifariji ni tiba sana
 
Upo sawa kabisa mkuu
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom