NADHARIA Kapteni Edward John Smith alisema 'Hata Mungu asingeweza kuzamisha hii Meli' (Titanic)

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Nadhani wengi tumetizama movie ya Titanic, ikielezea penzi la vijana wawili na pia kuzama kwa meli hiyo. Inasemekana ina uhalisia kiasi fulani na tukio la kweli la kuzama kwa meli hiyo mwaka 1912.

Jambo la kutafakarisha, imekuwa ikidaiwa kuwa aliyekuwa kapteni mkuu wa Meli hiyo Edward John Smith kabla ya kung'oa nanga alisikika akisema kuwa ''Hata Mungu Mwenyewe asingeweza kuzamisha hii meli'' - ( "Even God himself couldn't sink this ship")

Kauli hiyo inayodaiwa kutamkwa na Kapteni wa TITANIC, imetafsiriwa na wengi kama chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu hivyo kupelekea kuwaadhibu maelfu ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo.

Titanic.jpg

Edward John Smith

Titanic meli.png

Meli ya Titanic​
 
Tunachokijua
Titanic ilikuwa meli kutoka Uingereza iliyojengwa kati ya 1909 na 1912 huko Belfast. Wakati ule ilikuwa meli kubwa duniani. Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki kati ya Uingereza na Marekani.

Kwenye safari yake ya kwanza ilipata ajali ya kugongana na mwamba wa barafu tar. 14 Aprili 1912 saa 5:40 na kuanza kuzama saa mbili na dakika 40 baadaye katika usiku wa tar. 15. Aprili 1912.

Kuzama huko kulisababisha mauaji ya watu wapatao 1,500 kati ya abiria 2,224 waliokuwemo kwenye meli na kufanya kuwa ajali mbaya zaidi ya meli kuliko zote. Watu 700 waliookolewa na meli zilizokimbia kuokoa watu.

a%20titanic%20legacy--85598026_v2.jpg

Kapteni Edward John Smith ni nai?

Edward John Smith RD RNR ( 27 Januari 1850 – 15 Aprili 1912 ) alikuwa nahodha wa bahari ya Uingereza na afisa wa Jeshi la Wanamaji.

Mnamo 1880, alijiunga na White Star Line kama afisa, akianza kazi ndefu katika Jeshi la Wanamaji la Wafanyabiashara wa Uingereza.

Smith aliendelea kutumika kama mkuu wa meli nyingi za White Star Line. Wakati wa Vita vya Pili vya Boer, alihudumu katika Hifadhi ya Majini ya Kifalme, akisafirisha askari wa Imperial wa Uingereza hadi Koloni ya Cape.

Smith aliwahi kuwa nahodha wa meli ya Titanic, na alishuka na meli hiyo ilipozama katika safari yake ya kwanza.
330px-Edward_J._Smith.jpg
Je, Kapteni Edward John Smith alisema 'Hata Mungu asingeweza kuzamisha hii Meli' (Titanic)?

Kapteni Edward John Smith, nahodha wa meli ya Titanic anadaiwa kusema, Hata Mungu mwenyewe asingeweza kuzamisha meli hii. Meli nzuri sana, ambayo wakati huo ilikuwa meli kubwa zaidi na mojawapo ya meli za baharini zenye kasi zaidi.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kauli hiyo kuwa ni kweli alisema ivyo, na inaweza kuwa ilibuniwa kutokana na dhana ya kujiamini kupita kiasi kwa nahodha wa meli ya Titanic kwani hata alipopewa maonyo 6 juu ya tahadhari ya uwepo wa barafu alipuuzia na aliendelea kuwa na mwendo mkali sababu ambayo inaweza kuwa imechangia ajali kwa jinsi Titanic ilivyosimamiwa katika safari yake ya kwanza.

Inasemekana kuwa nahodha Edward Smith alikuwa na imani kubwa na meli ya Titanic kutokana na teknolojia mpya na kujengwa kwa viwango vya juu vya usalama. Hii inaweza kuwa sababu ya kwanini maneno kama hayo yanahusishwa naye.

a%20titanic%20legacy--85598026_v2.jpg
Mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonesha kuwa Kapteni Edward John Smith alisema Hata Mungu asingeweza kuizamisha meli ya Titanic, zaidi ya maneno ya kufikirika tu, hivyo madai hayo yanakuwa ni nadharia tu.
Kauli ya Kepteni Edward John Smith ni kauli ya kumkufuru Mungu
Mungu ni pendo, apenda watu... Kwaajili ya upendo wa Mungu kwa watu asingeweza kuizamisha meli ili watu wafe kwa mateso. Umejaribu kuitazama kauli yake kwa mtazamo chanya?

Kauli yake hata kama ilikuwa ya majivuno(ukaichukulia mtazamo hasi) vipi kuhusu hao wasiokuwa na hatia(abiria) nao Mungu alichukulia kama 'samaki akioza mmoja, wameoza wote?'...
 
Well said...

Listening to James Cameron akiongea kuhusu ajali ya Titan sub Vs Titan the ship....was all caused by bad seaman ship....warnings were ignored na finally disaster zikatokea!

Tuache kutetea uzembe huku tukimsingizia Mungu.
 
Nadhani wengi tumetizama movie ya Titanic, ikielezea penzi la vijana wawili na pia kuzama kwa meli hiyo. Inasemekana ina uhalisia kiasi fulani na tukio la kweli la kuzama kwa meli hiyo mwaka 1912.

Jambo la kutafakarisha, imekuwa ikidaiwa kuwa aliyekuwa kapteni mkuu wa Meli hiyo Edward John Smith kabla ya kung'oa nanga alisikika akisema kuwa ''Hata Mungu Mwenyewe asingeweza kuzamisha hii meli'' - ( "Even God himself couldn't sink this ship")

Kauli hiyo inayodaiwa kutamkwa na Kapteni wa TITANIC, imetafsiriwa na wengi kama chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu hivyo kupelekea kuwaadhibu maelfu ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo.

View attachment 2731258
Edward John Smith

View attachment 2731326
Meli ya Titanic​
Nimeona picha ya marehemu Kinyondo kwenye bandiko lako. Umefanya vyema kumkumbuka mtu aliyekuibua na ukafika ulipofika!!
 
Inawezekana alisema Cpt. Smith ila bado hiyo haikuwa sababu, huo ulikuwa mpango mkubwa sana ulioandaliwa kuwalenga watu kadhaa ili kuwapoteza ambao kwa namna fulani walikuwa na influence kubwa katika world economy.

Cpt. Smith ni moja ya familia ya Jesuits alikuwa hapo kutimiza agizo kuu.....

Kumbuka

Thesis × Antithesis= Synthesis
 
Mungu ni pendo, apenda watu... Kwaajili ya upendo wa Mungu kwa watu asingeweza kuizamisha meli ili watu wafe kwa mateso. Umejaribu kuitazama kauli yake kwa mtazamo chanya?

Kauli yake hata kama ilikuwa ya majivuno(ukaichukulia mtazamo hasi) vipi kuhusu hao wasiokuwa na hatia(abiria) nao Mungu alichukulia kama 'samaki akioza mmoja, wameoza wote?'...
Kauli aliyoitoa Kepteni Edward John Smith ni Kauli ya Kumkufuru Mungu.Hata kama mimi Mungu angenipa uwezo na kuniambia nihukumu Kepteni Edward John Smith basi ninge izamisha Meli kwa sababu ya kufuru zake hizo alizo zitoa Kepteni Edward John Smith . Unakumbuka Farao alivyo mkufuru Mungu? Na je Mungu alimuacha hai duniani? Mungu alimzamisha Farao na majeshi yake katika Mto Nile. Unakumbuka Nabii Luti wafuasi wake walivyofanya machafu duniani? Je Mungu Aliwaacha eti kwa sababu kuna wengine hawahusiki na hayo makosa? Unakumbuka Nuhu na safina yake watu wa Nuhu waliomkufuru Mungu Je Mungu aliwaacha hai? Ukikufuru Mungu hapa hapa Duniani atakuadhibu.
 
Inawezekana alisema Cpt. Smith ila bado hiyo haikuwa sababu, huo ulikuwa mpango mkubwa sana ulioandaliwa kuwalenga watu kadhaa ili kuwapoteza ambao kwa namna fulani walikuwa na influence kubwa katika world economy.

Cpt. Smith ni moja ya familia ya Jesuits alikuwa hapo kutimiza agizo kuu.....

Kumbuka

Thesis × Antithesis= Synthesis

Sinema la kutisha...

1695421987448.png
 
Inawezekana alisema Cpt. Smith ila bado hiyo haikuwa sababu, huo ulikuwa mpango mkubwa sana ulioandaliwa kuwalenga watu kadhaa ili kuwapoteza ambao kwa namna fulani walikuwa na influence kubwa katika world economy.

Cpt. Smith ni moja ya familia ya Jesuits alikuwa hapo kutimiza agizo kuu.....

Kumbuka

Thesis × Antithesis= Synthesis
Only few can understand you. There is an evil spiritual world operating 24/7 with a highly organized chain of commands. Most of the disasters happening today have a root of this spiritual world. ONLY GOD CAN PROTECT & SAVE US!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom