SI KWELI Matumizi mfululizo ya vidonge vya Kuzuia ujauzito (p2) huondoa kizazi cha Mwanamke

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Screenshot 2023-07-21 093206.png

Ni kweli kuwa matumizi ya mara kwa mara (Mfululizo) ya vidonge aina ya p2 huondoa kizazi cha mwanamke?
 
Tunachokijua
Tembe za uzazi za dharura, wakati mwingine hujulikana kama tembe za uzazi za asubuhi baada ya kushiriki tendo la ndoa, ni dozi ya dawa inayotumia vichocheo kuzuia ujauzito usiotarajiwa.

Zinaweza kuwa na mjumuiko wa vichocheo vya progestin levonorgestrel 1.5 mg, ethinyl estradiol 300 mcg, mifepristone 600 mg au ulipristal 30 mg.

Hata hivyo, progestin levonorgestrel 1.5 mg ndio chaguo la kimataifa linalokubalika zaidi kama tembe yenye ufanisi mkubwa katika kuzuia ujauzito kwa matumizi ya dharula.

Tembe hii inaweza kumezwa mara moja ikiwa na kiwango cha 1.5 mg au mara mbili kwa siku (kwa tofauti ya saa 12) ikiwa itakuwa kwenye ujazo wa 0.75 mg.

Humezwa lini?
Hufaa kumezwa moja kwa moja baada ya kushiriki tendo la ndoa na hufanya kazi ndani ya saa 72.

Hivyo, mtu akimeza ndani ya muda huo huwa na zaidi ya asilimia 95 ya kuzuia ujauzito.

Hata hivyo, tembe za ulipristal zinaweza kutumika hadi saa 120 baada ya kushiriki ngono. Hii ni wastani wa siku 5.

Lakini ni muhimu kufahamu kuwa ufanisi hupungua kadri mtu anavyokawia kumeza. Mtu aliyemeza mapema huwa na asilimia kubwa ya kufanikiwa kuzuia ujauzito kuliko yule aliyemeza kwa kukawia.

Hufanya vipi kazi?
Tembe za uzazi za dharura huwa na njia 2 za kuzuia ujauzito ambazo ni kuzia au kuchelewesha yai kutoka kwenye mfuko wa mayai wa mwanamke au kuzuia pamoja kutengeneza ute mzito unaozuia mbegu za kiume zisikutane na yai.

Mazingira ya matumizi yake
Vimetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya dharura kama vile kubakwa, kupasuka kwa kondomu wakati wa kushiriki tendo la ndoa au kufanya mapenzi kwenye siku zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ujauzito katika mazingira ambayo wahusika walikuwa wamesahau.

Pia, inaweza kutumika kama mwanamke anatumia njia nyingine ya vidonge kisha akawa hajameza vidonge husika kwa siku 3, au kama kaanza dozi hiyo kwa kuchelewa siku 3, kama kachelewa kwa wiki 2 kupata mwendelezo wa sindano ya uzazi wa mpango maarufu kama depo provera au kama kitanzi kimetoka kwenye sehemu yake.

Madai ya p2 kuondoa kizazi
Tembe za uzazi za dharura huwa na athari kadhaa kwa afya.

Athari hizo huwa ni kuchelewa au kuwahi kwa hedhi, kupatwa na hedhi nzito na chafu, kiungulia, maumivu chini ya tumbo, maumivu ya kichwa, kuwasha kwa matiti, kutapika pamoja na kuvurugika kwa vichocheo vya mwili.

Ikiwa zitatumika vibaya, hasa kwa matumizi ya mara kwa mara, tembe hizi zinaweza kusababisha ugumba pamoja na kufanya ujauzito utungwe nje ya mji wa uzazi.

Tafiti za afya na maelezo ya tahadhari yaliyotolewa kwenye nakala za maelezo ya matumizi ya dawa hizo kutoka kwa watengenezaji na mamlaka za udhibiti wa dawa duniani hazioneshi uwepo wa athari ya kuondoa kizazi.

Kizazi (Uterus) hakiwezi kuondolewa kwa kumeza tembe za p2. Kiungo hiki chenye mchango muhimu kwa afya ya uzazi wa mwanamke hasa kwenye kuruhusu hedhi na utunzaji wa ujauzito kinaweza kuondolewa kwa upasuaji maalum unaofahamika kwa jina la kitaalam la hysterectomy.

Baaadhi ya sababu zinazoweza kuchangia kuondolewa kwa kizazi ni uwepo wa saratani, uvimbe au kuvuja kwa damu kusiko na ukomo.

Madai ya tembe za p2 kuondoa kizazi hayana ukweli, ni uzushi usio na uthibitisho wa kisayansi.

Ushauri
Hii ni njia ya dharura, haipaswi kutumika kila siku kwani inaweza kuleta athari kubwa kwa afya.

Ikiwa kujizuia kabisa kushiriki tendo la ndoa hakutawezekana, njia zingine za uzazi wa mpango kama matumizi ya kalenda, kitanzi au kipandikizi zifuatwe ili kuondoa mazoea ya matumizi ya mara kwa mara ya dawa hizi.
Watumiaji waje watupatie evidences za hayo yote.

kifupi ma. jia ya uzazi wa mpango ya kizungu ni matatizo matupu.

labda ndom japo inapunguza utamu …
 
Kitu watu wanatakiwa kujua p2 inafanya kazi kwa ku extend time ya ovulation (yaan kusogeza muda wa yai kutoka kwenye ovaries kwa ajili ya kwenda kurutubishwa na mbegu).... Ila kama yai tayari limesha toka basi p2 haisaidii tena na mkifanya mapenzi na mbegu zikamwagikia ndani hata kama utakunywa hicho kidonge ndani ya saa 5 baada ya tendo mimba itaingia. ..so be careful usije kuwa surprised.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom