KWELI Nungunungu harushi miiba kujilinda dhidi ya adui yake

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari wakuu,

Kumekuwa na mawazo tofauti juu ya hatari ya mnyama Nungunungu. Kuna baadhi wanaamini kuwa Nungunungu hurusha miiba kujilinda na adui yake wakati wengine wanadai mnyama huyu harushi miiba bali huitegesha na adui hujichomesha mwenyewe.

Screenshot_20240403-013346_1.jpg


Je upi ni ukweli hapa?
---
animals_hero_porcupine.jpg

Picha: Nungunungu akiwa amesimamisha miiba yake (Credit: AnimalSandiegoZoo)
 
Tunachokijua
Nungnungu au nungu ni ni mnyama mdogo wa porini anayetambulika kwa kuwa na ngozi yenye miiba iliyochongoka anayoitumia kujilinda dhidi ya maadui. Ana manyoya magumu ya kahawia na meupe kichwani na shingoni, lakini miiba yake yenye ncha za rangi ya manjano ndiyo humtambulisha zaidi. Nungnungu hupendelea kushi milimani, mashambani, na porini.

Kumekuwapo na hoja za pande mbili zinazodai kuwa Nungunungu ni mnyama ambaye hurusha miiba yake pindi anapombana au kujilinda dhidi ya adui yake. Baddhi ya wadai wanadai mnyama huyo hurusha miiba kushambulia maadui zake huku wengine wanadai harushi miiba bali huichomoza tu na maadui hujichoma wenyewe.

Je Upi ni uhalisia wa hoja hizi?
JamiiCheck imefatilia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa kundi lenye hoja ya kuwa nungunungu harushi miba bali maadui (wanyama wanaomuwinda) hujichoa wenyewe wanapomshambulia wapo sahihi. Mathalani taasisi ya WonderOpolis, tovuti ya Mass Audubon wametoa makala maalumu kuelimisha namna ambavyo Nungunungu hana uwezo wa kurusha miiba yake kama wengi wanavyoamini. Katika kuelezea jambo hili WonderOpolis na Mass Audubon wanasema:

Nungunungu amekuwa anatumika kama muhusika kwenye filamu nyingi za katuni za watoto na amekuwa akioneshwa kama mnyama mwenye uwezo wa kurusha miiba yake kwa maadui lakini jambo hili ni kinyume kabisa na uhalisia wa mnyama huyo katika maisha ya kawaida. Japo kuwa mnyama huyo ana miiba lakini hairushi miiba hiyo kwa maadui na wanyama wanaomvamia. Pamoja na kwamba Mnyama huyo harushi miiba yake lakini haiondoi ukweli uwa ni miongoni mwa wanyama hatari.
Mass Audubon wanaeleza kuwa Wanyama hawa ni wataratibu, hupenda kuishi wakiwa wenyewe. Huwa na miiba ambayo mara nyingi huwa imelala kwenye ngozi yao na huisimamisha pindi wanapohisi hatari kwa lengo la kujilinda. Wanyama hawa hawarushi miiba yao na ikitokea umekutana naye unashauriwa kumuacha tu naye hatokudhuru.

Zaidi ya hayo JamiiCheck iliwasiliana na Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Beatus Maganja ili kupata ufafanuzi wa jambo hili ambaye aliitufafanulia kuwa:

Nungungungu hana kawaida ya Kurusha miba, ingekuwa anarusha miba maana yake sasa ingefikia sehemu ingekuwa inaisha katika ule mwili wake.
Miba kwa Nungunungu ni Mechanism ambayo Mungu amempa ya kujilinda dhidi ya maadui zake. Anachofanya Nungunungu huwa anajitanua kuichomoza ile miba yake anakuwa anajizungusha mbele ya adui yake kama chui au mnyama mwingine ili akimsogelea ajichome.
Watu wanaofikiri miba hiyo inarushwa inatokana na mnyama anapomvamia nungungungu kwa nguvu inamuingia na anapotoka anatoka nayo. Wanyama wengi wanavamia nungunungu huchukua muda mrefu kutafuta eneo laini ili kumdhibiti na ndiyo sababu hukumbana na miba kutoka kwa mnyama huyo. Wanyama wengi hukata tamaa na kumuacha Nungunungu kuondoka zake.
Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo JamiiCheck inaona hoja inayobainisha kuwa mnyama Nungunungu harushi miiba yake wakati anapovamiwa na adui au kuhisi hatari ni ya kweli
Habari wakuu,

Kumekuwa na mawazo tofauti juu ya hatari ya mnyama Nungunungu. Kuna baadhi wanaamini kuwa Nungunungu hurusha miiba kujilinda na adui yake wakati wengine wanadai mnyama huyu harushi miiba bali huitegesha na adui hujichomesha mwenyewe.

View attachment 2952319

Je upi ni ukweli hapa?
Yeaah, yuko sahihi, nungunungu hana uwezo wa kurusha miba, anajitegesha tu. Hana mechanism ya ku push hiyo miiba ana kifanya ni kugeuza mwili wake ili ukutane na miiba.

Zingine zilizobaki ni Story tu.
 
Habari wakuu,

Kumekuwa na mawazo tofauti juu ya hatari ya mnyama Nungunungu. Kuna baadhi wanaamini kuwa Nungunungu hurusha miiba kujilinda na adui yake wakati wengine wanadai mnyama huyu harushi miiba bali huitegesha na adui hujichomesha mwenyewe.

View attachment 2952319

Je upi ni ukweli hapa?
Uko sahihi kabisa kwa 100%, atakayebisha atakuwa mvivu wa kujisomea kwa kiwango cha SGR.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom