KWELI Senzo Mthethwa yupo hai, hakuuawa na Lucky kama wengi walivyodai

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimesikia kuwa msainii wa reggae wa Afrika kusini, Senzo Mthethwa, yupo hai na kwamba hakuuawa na Lucky Dube kama ambavyo nilisikia hapo awali.

Senzo nilikuwa namkubali sana kwa kazi zake kama "Nothing but Prayer", " Irene", "Worshiping Your Love", "Am Sorry".

Je, taarifa za kuwa yu hai ni za kweli? Nitafurahi sana kujua.

1710233103566.jpeg
 
Tunachokijua
Senzo Mthethwa, msanii wa reggae wa injili kutoka Afrika Kusini alikuwa maarufu katika miaka ya 90 na alifanikiwa kuwakamata hadhira mpaka maeneo ya Afrika Mashariki na Kati.

Hakuna aliyefahamu kilichotokea kwake hadi kila mtu alipoamini kwamba amefariki, hata baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kifo chake bila kufanya uchunguzi. Alikuwa maarufu zaidi na kupendwa nje ya Afrika Kusini, na alionekana kupata wafuasi wengi nchini Malawi ambapo hata alikuwa na mipango ya kuanzisha studio ya kurekodi, na mwendeshaji wa matamasha wa Malawi, Tailos Bakili wa Tai-B Promotions.

Studio ilipangwa kufunguliwa mwezi Disemba 1998, huko Blantyre, kwa matumaini ya kuendeleza wasanii wa ndani wa Malawi. Chini ya lebo mpya ambayo ingejulikana kama TAI-B Records, wasanii wangeweza kuendelezwa tanto nchini Malawi na Afrika Kusini.

1710228595581-jpeg.2932496
Baadhi ya watu wanaamini kwamba aliuawa na Lucky Dube kutokana na albamu yake ya Single ambayo ilipata umaarufu mkubwa. Watu walimuhusisha Lucky dube kwa kuhisi alitishwa na umaarufu wa Senzo ambao ungeweza kupunguza umaarufu wa Lucky Dube kwani wote walikuwa wanamuziki wa reggae huko Afrika kusini.

Baada ya kusambaa kwa taarifa za kifo chake kwa muda mrefu Senzo alikuja kujitokeza mwenyewe hadharani kwa kurekodi kipande cha video ambapo alieleza kuwa yeye hakufa, yupo hai ila alipata maradhi yaliyosababisha kushindwa kuendelea kuimba na ndio chanzo cha ukimya wake mpka baadhi ya watu kumzushia kuwa kafariki.

Hata hivyo baada ya hapo aliendelea kuonekana kwenye matamasha mbalimbali akiedeleza kazi zake za sanaa ambapo tarehe Oktoba 30 2022 alikuwa jukwaani akitumbuiza huko Malawi. Pia tarehe Septemba 16, 2023 alikuwepo Malawi jukwaani akitumbuiza.
screenshot-2024-03-12-at-12-37-17-senzo-live-in-malawi-png.2932579

1710236878828-png.2932583
Kutokana na vithibitisho vya yeye mwenyewe kujitokeza kukanusha uvumi wa kifo chake Jamiicheck imejiridhisha kuwa Senzo yupo hai na madai ya Lucky Dube kumuua yalikuwa ni uzushi.

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom