KWELI Zaidi ya watu milioni 91 wanaishi na Ugonjwa wa Homa ya Ini barani Afrika

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa homa ya ini vimeripotiwa Kuongezeka kwa kasi barani Afrika.

Pia, baadhi ya nyaraka zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha kuwa idadi ya visa vya ugonjwa huu vimefikia zaidi ya milioni 90.

shutterstock_1667884225-scaled.jpg

Ukweli wa taarifa hizi upoje?
 
Tunachokijua
Zaidi ya watu milioni 91 wanaishi na aina B au C ya ugonjwa wa homa ya ini barani Afrika. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya July 27, 2022 iliyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Utafiti huu uliofanyika kuanzia mwaka 2021 ulilenga kuchunguza ukubwa wa janga hili kwa kufuatilia aina hizo mbili ambazo huharibu afya ya ini kwa kusababisha makovu na saratani.

Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 8 ya watu wote kwenye nchi 19 barani Afrika wameathirika na aina B ya ugonjwa wa homa ya ini huku nchi zingine 18 zikiwa na asilimia 1 ya watu wake wakiishi na aina C ya ugonjwa wa homa ya ini. Aidha, mwaka 2020 bara hili lilitoa asilimia 26 ya visa vyote duniani, huku vifo 125,000 vikiripotiwa kutokea.

Virusi vinavyo sababisha ugonjwa wa homa ya ini hupatikana kwenye aina kuu 5 tofauti ambazo ni A, B, C, D na E. Pombe, vimelea vingine vya magonjwa, madawa, pamoja na aina mbalimbali za sumu ni visababishi vingine vya tatizo hili.

Aidha, vifo vitokanavyo na Ugonjwa huu vitaongezeka sana ifikapo mwaka 2030 ikiwa jitihada sahihi za Kinga, Utambuzi na Matibabu hazitachukuliwa hadi kufikia Milioni 16 kwa mwaka.

Pamoja na uwepo wa aina tano tofauti za ugonjwa huu, aina mbili za B na C ndiyo hatari zaidi kwa kushambulia na kuua.

Kwa mujibu wa WHO, virusi vya homa ya ini aina B huwa na uwezo mkubwa sana wa kushambulia na kuambukiza mara 50-100 zaidi kuliko VVU.
Miongoni mwa magonjwa yatakayo kuja kuwa ni hatari hapo mbeleni ni hii homa ya ini (hepatitis) pamoja na magonjwa ya saratani,kisukari,figo,Moyo na Matatizo ya afya ya akili

Kibaya zaidi ktk ugonjwa wa ini, watu huutambua ukiwa umeshaleta athari kubwa ktk mwili. Ugonjwa huu ni hatari kuliko hata HIV, ni heri upate HIV sio homa ya ini, Ingawa hakuna ugonjwa ambao ni mzuri ktk mwili wa mwanadamu

Serikali yetu ipunguze gharama za vipimo, pia Iandae mpango wa kampeni ya upimaji afya ktk maeneo mbalimbali hapa nchini na kutoa chanjo ya ugonjwa huu bure au kwa gharama nafuu, na watu wapewe elimu juu ya ugonjwa huu,njia za kuepukana nao ili kuokoa kizazi chetu

Huu ugonjwa ni Silent killer Unakuuwa kimya kimya ⚠️
 
Kwa kizazi hiki kilichokengeuka na kuanza kampeni ya kukataa kila chanjo sijui itakuaje .Ngoja tuone maana huo ugonjwa hauna tiba zaidi ya chanjo. Na hiyo hepatitis B ndio balaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom