- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Ninaomba kufanyiwa uhakiki wa taarifa kuwa 'Watu wanaochelewa kulala wapo hatarini kupoteza maisha mapema'
- Tunachokijua
- Kulala ni kitendo cha kupumzika na kupoteza fahamu ambayo hutokea mara kwa mara kwa wanadamu na wanyama wengine, ambayo ni muhimu kwa afya na ustawi. Ni wakati ambapo mwili na akili zinapumzika na kujitengeneza upya.
Tafiti zinaeleza kuwa Viumbe wengi ikiwamo binadamu wanatumia sehemu kubwa Maisha yao kulala (soma hapa). Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa kulala ni lazima na muhimu kwa kiumbe yoyote (soma). Binadamu anapaswa kulala mtu mzima anapaswa kulala kuanzia saa 7 au zaidi kwa siku (soma hapa) ikitokea analala chini ya hapo si salama kwa Afya yake.
Je, kuchelewa kulala kunaweza kuchangia mtu kuwahi kufa?
Katika kuoata uhakika wa hoja hii JamiiCheck imepitia vyanzo mbalimbali vya Afya pamoja na kuzungumza na Wataalamu wa Afya.
Vyanzo vyote vinakubaliana kuwa kuchelewa kulala au kupata saa chache za kulala usiku ni hatari kwa Afya kwa sababu huweza kuchochea kuibuka kwa changamoto mbalimbali za kiafya pamoja na kudhoofisha Kinga ya mwili.
Mathalani, ukurasa wa Healthline unaozungumzika masuala mbalimbali ya Afya unabainisha kwa undani namna kutolala vizuri kunavyoweza kuchochea changamoto nyingi za kiafya.
Wakifafanua hoja hii Healthlie wanasema:
Kutopata usingizi wa kutosha kunachosha uwezo wako wa kiakili na kuweka afya yako ya kimwili hatarini. Tafiti za kisayansi zimebaini kuwa kutolala vyema kunachochea usingizi matatizo mengi ya kiafya, ikiwamo kuongezeka uzito kusiko kawaida, kuathiriwa mfumo wa kumeng'enya chakula, kuathiriwa mfumo wa upumuaji pamoja na kudhoofisha mfumo wa Kingamwili.
Zaidi ya hayo JamiiCheck imezungumza na Isaac Maro, Daktari na Mtafiti wa Masuala ya Afya aliyefafanua kuwa
Kulala kwa muda mfupi kunaweza kusababisha changamoto za Kiafya kama mwili kutorekebisha hitilafu mbalimbali.Pia inaweza kusababisha changamoto za Akili mfano kudumaza uwezo wa kufikiria, inaweza ikachelewesha tishu za kuponesha vidonda. Inaweza kusababisha Sonona na wasiwasi, mwili kuchoka. Inashauriwa kulala angalau kwa saa nane.Mawazo ya Wataalamu hao yanakubaliana kuwa mtu anayechelewa kulala anaweza kupata changamoto mbalimbali za kiafya tofauti na mtu anayewahi kulala.
Hivyo, kutona na hoja hizo kutoka kwa Wataalamu wa Afya JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa watu wanaochelewa kulala wapo hatarini kufa mapema, Ina ukweli