tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. M

    Bando sasa ziwe bila ukomo wa muda wa matumizi

    Salam kwenu. Kufuatia changamoto ya internet tunayoendelea kuipata niiombe TCRA kuyaagiza makampuni yote yanayotoa huduma za internet. 1. Kufidia wateja wote kwa kurejesha bando zilizolika ama ku expire kipindi hiki cha tufani la internet. 2. Vifurushi vyote vya internet sasa visiwe na ukomo...
  2. BARD AI

    TCRA: Kuna tatizo la Mfumo wa Mawasiliano ya Intaneti kwenye Mkongo wa Baharini

    Kama umekosa huduma ya intaneti kwa saa kadhaa leo, tambua shida sio kifaa unachotumia bali ni tatizo la kiufundi lililotokea kwenye miundombinu ya intaneti iliyopitishwa baharini. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari amelithibitisha hilo alipotafutwa na...
  3. J

    PesaX / CashX (Singularity) wanatumia taarifa binafsi za watu na wanakiuka mamia ya sheria Tanzania

    Ndugu zangu wa Tanzania, Kuna kampuni inayotoa huduma za kukopesha pesa mtandaoni ambayo inajulikana kwa majina kadhaa katika aplikesheni zake, ambayo kwa ujumla hutumia jina la "Singularity". Sijawahi kukutana na kampuni inayoendeshwa hovyo kama hii! Nimekuwa nikikopa pesa mara kwa mara kutoka...
  4. Stroke

    Content ya media nyingi sio kwa ajili ya kuelimisha, uchambuzi wa mpira umetamalaki. Kama jamii tunapaswa kubadilika

    Kama wiki mbili hivi sikuwa online kwenye social media hivyo nilipata wasaa wa kusikiliza redio zetu hapa nchini. Katika wiki zote hizo mbili nilikua natune almost radio zote , ila vipindi vingi vya radio zetu vinafanana na sio elimishi, burudani imechukua sehemu kubwa na hasa uchambuzi wa...
  5. BUSH BIN LADEN

    BASATA Na TCRA waache Double Standards

    Je, sababu zilizotumika kuzifungia nyimbo kama Kibamia na Nyegezi hazipaswi kuwa hizo hizo kukifungia kipindi cha Bao la asubuhi cha Bongo Fm(TBC Fm ya zamani). Naomba tujadili.
  6. MLUGURU

    Makampuni ya Mawasiliano yaboreshe vifurushi viwe rafiki kwa ajili ya viziwi

    TCRA pamoja na haya makampuni ya simu ya Tanzania (Tigo, Vodacom, Halotel, Zantel, Airtel,ttcl), miongoni mwa wateja wenu kuna hawa wenye mahitaji maalumu ambao ni viziwi kiasili. KIZIWI maana yake ni mtu ambae hawezi kuwasiliana kwa namna yoyote ile kwa njia ya sauti zaidi ya video call na sms...
  7. JITU BANDIA

    TCRA mmeshindwa kufuatilia uhuni unaofanywa na Vodacom upande wa M-Pesa?

    Ni wiki ya pili sasa nimekuwa nikifuatilia hiki kitu kwa namba tofauti tofauti. Iko hivi: Sasa hivi ukiweka pesa kwa wakala yeyote yule, iwe unamtumia mtu, ama unaweka kwako hautumiwi sms kuonesha ya kwamba umewekewa kiasi fulani, wala kwa mpokeaji! Wakala anachoweza kukwambia ni kwamba...
  8. P

    Ukiangalia vizuri mpotoshaji mkubwa ni serikali, kwanini inachukuliwa hatua pale tu mwananchi akipotosha?

    Wakuu kwema? Tumeshudia mara kadhaa wananchi wakichukuliwa hatua kwa makosa ya "Kusambaza taarifa za uongo" au kufanya "Upotoshaji", mfano wa juzi juzi hapa ni yule dada aliyeimba mnatuona manyani "Tanzania inaelekea wapi?" baada ya kuona shtaka la kusababisa uchochezi ni weak shataka likageuka...
  9. Roving Journalist

    Waziri Nape Nnauye awateua Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Machi 21, 2024

    UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) Tarehe 21 Machi, 2024 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb) kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003...
  10. Mkoba wa Mama

    TCRA waichunguze kampuni ya simu za mkononi ya Halotel

    Mtandao wa Halotel umekuwa na tabia ya kukata salio la muda wa maongezi mara tu unapoongeza salio. Hii imenitokea zaidi ya mara tatu sasa, na nikipiga simu huduma kwa wateja naambiwa kuna huduma nimejiunga inayokata salio hilo, wakati hakuna huduma yoyote ambayo mimi nimejiunga. Mbaya zaidi...
  11. tpaul

    TCRA na TCU wachukue hatua kali kwa Wasafi TV kutokana na 'kiki' ya mapacha kufanyiana mtihani

    Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna hiki kipande cha video kinachobamba mtandaoni kuhusu mapacha wawili ‘wanaokiri’ hadhrani kufanyiani mtihani ‘chuoni’. Ukisikiliza kwa makini na kwa utulivu wa hali ya juu, utagundua kuwa hawa watu wanaigiza tu. Haiingii akilini watu...
  12. hp4510

    Serikali na TCRA chukueni hatua kampuni ya Flex cash

    Wangudu Leo nikiwa kwenye feri natoka kigamboni kwenda mjini, nilikaa karibu na ndugu mmoja alikuwa busy kuongea na simu Baada ya muda kidogo nikaona anakosa nguvu kama anataka kuzimia, anatokwa na jasho Sana, Ikabidi kwenda kumsaidia na kumuuliza shida ya mkasa uliompata Kumbe bwana ana...
  13. Chizi Maarifa

    Kwa jambo hili niliwaunga Mkono TCRA . Nchi hii wenye akili ni wachache sana

    Hakuna Mtangazaji mwenye akili anaweza ongea jambo kama hili. Tanesco wana matatizo yao na pengine ni ya kisiasa zaidi. Hakuna mtanzania mwenye akili timamu atapendezwa na suala hili la kukatika katika umeme. Lakini ni mtu mpumbavu tu anaweza fanyia mzaha jambo hili zito Kitaifa. Ni wakati sasa...
  14. snipa

    Precision ya "Tuma kwenye namba hii" na Apps za Mikopo.

    Kuna Thread niliwahi zungumzia juu ya Apps hizi scam za Mikopo. Sasa Leo tujaribu kuangalia kwa upande wa matapeli wa tuma kwenye namba hii ambalo ni gang kubwa na wanafunikwa na kivuli Cha wakubwa. Kama nilivyowahi kueleza kuwa Apps za Mikopo kama vile PesaX, Msafi, Twiga Loans n.k hizi apps...
  15. P

    Waziri Nape aruhusu magazeti kuendelea kusomwa kwa mbwembwe. Mpaka matamko yanakinzana huwa hakuna mawasiliano ndani ya wizara?

    Nimeona mjadala wa “Kusoma magazeti”. Nimeelekeza TCRA kuruhusu UBUNIFU kwenye tasnia ya Habari. Staili ya usomaji we magazeti imeongeza MVUTO kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa KUTIWA MOYO badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti. Maelekezo mengine yeyote...
  16. Mjanja M1

    TCRA: Hakuna kanuni inayokataza kusoma Magazeti kwa Mbwembwe

    Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Andrew Kisaka amesema kauli yake imepotoshwa kuhusu wasomaji wa Magazeti kwenye Redio akisema hakumaanisha usomaji wa mbwembwe bali wasomaji kusoma na kuingia ndani. Akizungumza leo asubuhi na Kipindi cha Good Morning cha...
  17. Mjanja M1

    TCRA: Vyombo vya habari vinavyochanganya lugha kuchukuliwa hatua, ‘kuna haja ya kukiita kipindi Goodmorning?’

    Meneja huduma za Utangazaji, TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuwa tabia ya vyombo vya habari kuruhusu watangazaji kuchanganya lugha kwenye vipindi vyao ni kosa kisheria na watachukuliwa hatua. 📹 TheChanzo Written by Mjanja M1 ✍️
  18. JanguKamaJangu

    TCRA yazifungia Laini 21,000 zilizohusika kufanya utapeli

    ZAIDI ya laini 21,788 za mawasiliano ya simu zimefungiwa kupokea na kutoa mawasiliano kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutumika kufanya uhalifu mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita. Kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa sekta ya mawasiliano iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa...
  19. J

    TCRA imesema watumiaji wa internet wapo 35M

    TCRA Wametoa report ya Q2 inaonyesha watumiaji wapo 35M wa internet. Hii ni work force kubwa sana , na ni muda wa serikali kuwaza sasa kutengeneza ajira za mitandaoni nyingi sana. Ukosefu wa ajira za kawaida na ongezeko la watumiaji wa internet inaleta picha ya ama serikali itengeneze ajira...
  20. Mtini

    TCRA imeshindwa kuwadhibiti matapeli wa mitandao? Au wanakula nao?

    Walipoleta utaratibu wa kusajiri kwa alama za vidole walituambia ni kwasababu ya kudhibiti matapeli, ila kadri siku zinavyoendelea ndivyo wanavyoongezeka. Je, mfumo ulikuwa wa upigaji umeshindwa kuwadhibiti? Au TCRA wanashirikiana na hawa wapigaji? Je, kwanini wasiweke utaratibu rahisi kabisa...
Back
Top Bottom