PesaX / CashX (Singularity) wanatumia taarifa binafsi za watu na wanakiuka mamia ya sheria Tanzania

May 6, 2024
8
5
Ndugu zangu wa Tanzania,

Kuna kampuni inayotoa huduma za kukopesha pesa mtandaoni ambayo inajulikana kwa majina kadhaa katika aplikesheni zake, ambayo kwa ujumla hutumia jina la "Singularity". Sijawahi kukutana na kampuni inayoendeshwa hovyo kama hii! Nimekuwa nikikopa pesa mara kwa mara kutoka kwao na kurudisha bila kuchelewa wala kuchenga. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kwamba, unapokopa pesa, unakuwa na makubaliano ya kuchagua muda wa kurejesha pesa. Kwa mfano, ukichagua siku 7, huduma ya wateja yao huanza kukusumbua siku ya 6 ili urudishe pesa kabla ya "due date" kufika. Wanatuma meseji za hovyo bila mpangilio, na kupiga simu mara kwa mara, hata kufikia kiwango cha kero. Meseji zao za vitisho na kauli zao za kukera na dharau huathiri sana.

Haya yote yanakiuka sheria, miongozo, kanuni, na sera zilizowekwa na TCRA: Kuna muda maalumu wa kufanya mawasiliano na mteja, na si nje ya muda huo. Kuna lugha maalumu na namna ya kumfikia mteja, sio kiholela na kutumia namba mpya kila siku na huduma ya wateja au watoa huduma za kukusanya madeni kutuma meseji kwa namna wasiyojali.

Kampuni hizi zinakiuka haki ya raia kwa kuchukua taarifa binafsi na kuzitumia kwa njia isiyofaa. PDPC (Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi) inapaswa kuchukua hatua. Aidha, kampuni hizi zinaenda kinyume na miongozo ya BOT. Mtu akichukua mkopo, hatakiwi kusumbuliwa kulipa kabla ya tarehe ya mwisho ya urejeshaji wa mkopo tena kwa vitisho.

kwa uchache hayo ni baadhi tu ya mambo yanayofanywa na kampuni hii.
images.png

Je ni yapi mengine umekutana nayo ama kuskia kuhusu kampuni hii?
 
Ila wee jamaa unachekesha kweli,yaani unasema unakopa mara kwa mara alafu unasema kampuni ya hovyoo..kwani wanakulazimisha uendelee kukopa au mwenyewe unapenda kukopa ukitegemea huruma ya watu
 
Back
Top Bottom