Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imezinduliwa, ianze na wale wanatumia taarifa za watu kwenye Vifungashio

Swala mdogo

New Member
Nov 15, 2023
2
1
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022, ilianza kutumia rasmi Mei 01, 2023 na Tume inayosimamia Ulinzi wa Taaarifa Binafsi japo ilianza kufanya kazi tangu Mei 2023, imezinduliwa jana na Rais wa Samia Suluhu Hassan.

Najua Tume ina kazi nyingi za kufanya hasa kwa wakati huu ambapo ndio kwanza imeanza, ila napendekeza waanze na watu wale wanaotumia taarifa za watu za shule au hospitali zikiwa kwenye makaratasi kama vifungashio. Sheria imeeleza wazi kabisa kuwa Taarifa Binafsi ni pamoja na Jina la mtu lakini vifungashio hivi vingi vina majina na matokeo ya watu ya mitihani au majibu ya hospitali jambo ambalo sio sawa.

Naomba Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ikiwa chini ya Mkurugenzi wake, Ndugu Emmanuel Mkilia ishughulikie suala hili kwa kuanza kushughulika na Wakusanyaji wa Taarifa hizo hadi watengenezaji.

Ina huzunisha sana unanunua Vitumbua kwa Mama Ntilie na kifungashio ni Mtihani wa mtoto wa Kidato au darasa fulani na jina lake likiwa linaonekana. Wengine wanaenda mbali nakutumia hadi kopi za Leaving Certificates za watu na zikiwa na picha kabisa.

Naamini Tume itashungulikia na kukomesha suala hili. Asante

photo_2024-04-04_17-03-30.jpg

photo_2024-04-04_17-03-28.jpg

photo_2024-04-04_17-03-23.jpg
 
Hii ni balaa, unanunua zako maandazi kwa Mama Muuza unakutana na matokeo ya mwanao ya mtihani 😁😁
 
Back
Top Bottom