sgr

The SGR-A1 is a type of sentry gun that was jointly developed by Samsung Techwin (now Hanwha Aerospace) and Korea University to assist South Korean troops in the Korean Demilitarized Zone. It is widely considered as the first unit of its kind to have an integrated system that includes surveillance, tracking, firing, and voice recognition. While units of the SGR-A1 have been reportedly deployed, their number is unknown due to the project being "highly classified".

View More On Wikipedia.org
  1. Abraham Lincolnn

    Video: Treni ya SGR yadaiwa kusimama baada ya kupata hitilafu eneo la Gongo la Mboto

    ====== UPDATES ======= Habari zinazosambaa Mtandaoni zikidai Treni ya SGR yadaiwa kusimama baada ya kupata hitilafu si za Kweli kwani Treni ipo kwenye Majaribio.
  2. Stephano Mgendanyi

    Mbunge Santiel Kirumba Ataka Serikali Kutatua Changamoto ya Ajira Kwenye Miradi ya Kimkakati ya SGR Mkoani Shinyanga

    MBUNGE SANTIEL KIRUMBA Ataka Serikali Kutatua Changamoto ya Ajira Kwenye Miradi ya Kimkakati ya SGR Mkoani Shinyanga Swali la Mhe. Santiel Eric Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga aliyetaka kufahamu, Serikali ina mpango gani kutatua changamoto ya ajira kwenye Miradi ya Kimkakati...
  3. G

    SoC04 Tanzania Tutakayo: Bei ya nauli ya SGR izingatie hali halisi ya uchumi wa wananchi

    Rai yangu ni kuona bei ya nauli zinazopangwa na mamlaka husika zinazingatia hali ya maisha ya wananchi ili reli hii iwafae wengi kutokana na usalama wa safari, safari kutumia muda mchache pia kutokana na kutumia nishati mbadala ya umeme badala ya mafuta sababu tumekuwa tukishuhudia kupanda kwa...
  4. G

    SoC04 Tanzania Tuitakayo: SGR kukuza uchumi wa nchi, kupunguza ajali barabarani iwapo bei za nauli zitazingatia vipato vya wananchi

    Naipongeza serikali kwa ujenzi wa reli ya kisasa,pia kwa kuona kuwa hatuwezi kuendesha reli ya kisasa bila kuwa na umeme wa uhakika na wakaona wajenge Bwawa kubwa la maji la Mwl.Nyerere kwa ajili ya kuzalishia umeme sababu umeme tuliokuwa nao usingetosha kwa matumizi na kwa ajili ya kuendeshea...
  5. Keynez

    Reli ya SGR itakidhi mahitaji ya baadaye?

    Nikiangalia ujezi wa reli ya SGR naona una track moja tu inayotoka Dar es Salaam mpaka Dodoma na ujenzi wa kwenda maeneo mengine kama Mwanza na Kigoma ukiendelea. Kuna matarajio makubwa sana kwenye reli katika usafirishaji wa abiria na mizigo. Swali langu la msingi ni hili. Kama track ya reli...
  6. Kijakazi

    SGR yetu waweke Polisi au JKT chooni!

    Huu ni ushauri wangu tu kwa kuanzia kila choo kiwe na askari mlangoni kukagua kila anayetoka chooni kama kachafua au kakiacha choo kisafi kama alivyokikuta. Na atakayechafua aidha asafishe mwenyewe au apigwe faini ndefu. Bila ya hivyo itakuwa SGR ya kichocho na kipindu pindu baada ya safari ya...
  7. TODAYS

    Hii ni Off show au itaendelea kudumu?

    Wale wa kwenye ndege wanabeba mabegi makubwa na hawa wababeba madogo kama haya. Swali hii show itadumu au ni kwa ajili ya kupigia picha.
  8. Leak

    Nimeona picha za wahudumu wa treni ya kisasa ya SGR ambayo inafanyiwa majaribio leo kutoka Dar -Dodoma

    Nimeona picha za wahudumu wa treni ya kisasa ya SGR ambayo inafanyiwa majaribio leo kutoka Dar -Dodoma! Na fikira zikanijia kuwa kuna uwezekano mkubwa wana Jf nao wamenufaika lakini nimefanikiwa kumjua mwana Jf mmoja tuu hapo ! Vijana hizi fursa hamkuziona? Au hamkutangaziwa?
  9. TwinsOrg_88

    DOKEZO SGR LOT 5 Hali ni tete. Wafanyakazi zaidi ya 200 wasimamishwa kazi

    Habari Wana JF, Hali ni Tete sana Mradi wa reli ya SGR LOT 5 kutoka Isaka to Mwanza ambao upo chini ya ujenzi wa Kampuni CCECC. Kwa sasa Mradi umesimama ujenzi sababu hela hakuna ya uendeshaji mradi, wamepunguza wafanyakazi zaidi ya 200 na bado wanaendelea kupunguza. Aliye karibu na Mama...
  10. TwinsOrg_88

    DOKEZO Mradi wa SGR LOT 5 Ujenzi unasuasua sana

    Habari Wakuu! Kampuni ya China inayotengeneza SGR LOT 5 kutoka Isaka to Mwanza CCECC, inakaribia kuacha kuendelea na ujenzi huo wa reli sababu wanadai fedha nyingi serikali wanasema hawajalipwa wanatengeneza kwa fedha zao wenyewe kuanzia vifaa mpaka kulipa mishahara ya wafanyakazi, hivyo...
  11. Lady Whistledown

    Hadi sasa Mradi wa SGR umegharimu Tsh. Trilioni 10.69

    Serikali ya Tanzania hadi sasa imetumia jumla ya Shilingi Trilioni 10.69 kwenye Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kama sehemu ya miradi mikubwa ya nchi. Akitoa ombi kwa Bunge kuunga mkono jumla ya Shilingi Bilioni 532.8 kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2024/25...
  12. Tanzania Railways Corp

    Treni Mchongoko yawasili nchini

    Seti ya kwanza ya EMU Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa ya kuwasili katika Bandari ya Dar es salaam kwa seti ya kwanza ya Treni ya kisasa ya EMU, Vichwa vitano vya umeme na Mabehewa matatu ya Abiria ( iliyowasili ni seti moja ambayo kikawaida hufungwa behewa nane na vichwa viwili...
  13. BARD AI

    Waziri Mkuu: Tsh. Trilioni 10.69 zimetumika kujenga Reli ya SGR Dar mpaka Moro

    Serikali imeendelea kutoa fedha za utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) wa kilomita 1,219, kwa kutoa jumla ya Sh10.69 trilioni na kwa ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro. Hayo yamesemwa leo Jumatano, Aprili 3, 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa...
  14. TODAYS

    SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

    Mkurugenzi mkuu wa TRC ndg Kadogosa alikuwa akiongea na kamati ya bunge walipotembelea mradi huo na kusema "Kuhusu mchakato wa nauli, sisi TRC tumemaliza sehemu yetu ambapo tumewasilisha kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) kila kinachohitajika." Alisema wanaelewa kuwa...
  15. FaizaFoxy

    ATCL, Reli ya Kati, TAZARA na SGR tuwape wanaoweza kuendesha kwa ufanisi mapema kabla ya kuumizwa

    Kuwawachia Watanzania waendeshe nashirika hayo makubwa ni ujinga uliokithiri. Hivi hatuelewi mashirika hayo yaliuliwa na kina nani mpaka kuwa chali? Tumeona mwendokasi imetushinda kuendesha na sio kwa mara ya kwanza. ATC tuliiuwa na sasa ipo njiani kuuliwa tena. Reli ya kati na TAZARA...
  16. Roving Journalist

    TRC: Suala la Nauli za Treni ya SGR tumekabidhi mapendekezo kwa LATRA

    Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefanya ziara ya kukagua Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kujionea majaribio ya treni hiyo ambayo yalianza hivi karibuni. Ziara hiyo imeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vuma Augustine (Mbunge wa Kasuru vijijini), ambapo...
  17. Greatest Of All Time

    Kadogosa: Asilimia 70 ya Ujenzi wa SGR umefanywa na awamu ya 6

    Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli nchini (TRC) amesema asilimia 70 ya ujenzi wa reli ya kisasa umefanywa na awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa mantiki hiyo, awamu ya tano chini ya hayati Magufuli ilihusika na asilimia 30 tu🤣 My take: Legacy inafutwa kwa kishindo, mnyonge...
  18. Roving Journalist

    Mkurugenzi TRC: Tutaruhusu Wawekezaji binafsi kwenye Mradi wa SGR kuingiza Vichwa cya Treni na mabehewa yao

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali itanatarajia kuweka milango wazi kwa wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye mradi wa reli ya kisasa (SGR) kwa kuingiza vichwa vya treini na mabehewa yao. Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini...
  19. S

    Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

    Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma. Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na...
  20. Roving Journalist

    Waziri Mbarawa: Treni yetu ya SGR haiwezi kwenda Spidi 160 kwa Saa, tunaenda kwa Awamu

    Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Makame Mbarawa amesema majaribio treni ya SGR yamekuwa yakizingatia usalama unaofanya treni kutembea kwa mwendokasi wa chini tofauti na itakavyokuwa baada ya safari rasmi kuanza. Mbarawa amesema treni hiyo kwa kawaida itakuwa na mwendo kasi wa Kilometa...
Back
Top Bottom