Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,558
113,751
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,

1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.

2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.

Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.

Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar

Mkanganyiko wa Katiba.

Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu muungano na serikali moja.
 
Tatizo hao ndugu zenu wasio na vichogo, watapinga ili waendelee kufaidika na huu muungano wa sasa wa changu changu, chako changu. Hivyo bora ungevunjwa tu ili kila nchi ijitegemee kivyake kwa 100%.
Kwa mujibu wa zile articles of the union, muungano wetu sio mkataba, not a contract, ni makubaliano, an agreement na ulidhamiriwa uwe ni muungano wa milele!, hakuna any provisions za kuuvunja muungano!. Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
P
 
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna
binafsi sina shaka kabisaa,
ndoto ya Baba wa Mwl.J.K.Nyerere yaweza kutimia vizuri sana na kikamilifu, endapo tu viongozi wenye wenye utashi dhabiti wa kisiasa, watathubutu, watatuelekeza, watatusimamia, watatupitisha na kutuongoza kufikia huko kwa maridiano na amani, huku sote tukiwa na ufahamu, uelewa na nia moja dhabiti ya kua nchi moja Tanzania 🐒
 
lets hope for the best
p
 
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya

Paskali
Yes, Serikali moja tu inatakiwa, Zanzibar iwe ni Wilaya tu, yaani iwe Wilaya ya Unguja na Wilaya ya Pemba.
Ikishindikana kuunda Serikali moja, Basi Muungano huu uvunjwe na kila upande ubaki na hamsini zake
 
binafsi sina shaka kabisaa,
ndoto ya Baba wa Mwl.J.K.Nyerere yaweza kutimia vizuri sana na kikamilifu, endapo tu viongozi wenye wenye utashi dhabiti wa kisiasa, watathubutu, watatuelekeza, watatusimamia, watatupitisha na kutuongoza kufikia huko kwa maridiano na amani, huku sote tukiwa na ufahamu, uelewa na nia moja dhabiti ya kua nchi moja Tanzania 🐒
Muungano hauleti ugali mezani, na wananchi hawataki muungano wanataka maendeleo. Lugha za majizi ya ccm. Hivi wananchi wote waliuelewa muungano ndio ukaanza?
 
Naunga mkono hoja. Kwa wakati huu yakitokea kama yale ya 'kuchafuka hali ya hewa Zanzibar', hoja za OIC au kashikashi kama zile za wale G55 na lile azimio la bunge la madai ya serikali tatu sijui nani atasimama kuliokoa taifa.

Ili tuwe salama ni muhimu tuwe na serikali moja tu.
 
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,

1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.

2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.

Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.

Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar

Mkanganyiko wa Katiba.

Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Mkuu huoni kuwa Zanzibar based on existing fact and experience ya Zanzibar kuwepo ndani ya union kwa miaka 60 sasa bila shida yoyote ya kudhofisha muungano huu, the best option ni federation ambapo Tanganyika nayo iijiamulie mambo yake kama ilivyo kwa Zanzibar.

Mkuu unafikiri Zanzibar itakubali kupoteza uhuru wake ambao imeenjoy kwa miaka 60 huku ikiona vividly maumivu ya umauti wa Tanganyika??!

Hakuna mtu anaye penda hali ya umauti Mkuu hata kidogo, kosa lishafanyika kuiacha Zanzibar iwe huru, usirudie kosa hilo la kuiua Tanganyika kwa Zanzibar.

Njia rahisi na isiyokuwa na maumivu na majuto ni kuipa Tanganyika uhuru wa ndani kama Zanzibar huku muungano ukiimarishwa zaidi kwa mambo ya Muungano.

Nchi hizi mbili ziwe ni states ndani ya Muungano/Federation. Viongozi wake waitwe magavana sio Rais na Tanganyika iwe na baraza lake la wawakilishi, wabunge wa muungano wawe ni Maseneta.

Hakuna dhambi kuboresha kuliko kufifisha. Hofu ni ya nini??
 
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,

1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.

2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.

Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.

Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar

Mkanganyiko wa Katiba.

Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Serikali moja ndiyo lengo la uvamizi wa Nyerere kwa Zanzibar , lakini hapo ndiyo Tz itapogeuka Kongo
 
Back
Top Bottom