Tunaweza kuwa na Muungano wa Serikali mbili na nusu pia, sio lazima kufikiria ni moja, mbili au tatu tu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,247
47,443
Kila mara kunapozuka mjadala kuhusu muungano wetu mara zote watu hubishania kati ya serikali mbili au tatu, kuna kundi dogo pia ambalo huwazia na kuibua hoja za serikali moja kabisa. Je tunaweza kujiongeza kufikiria nje ya mawazo haya? Mfano uwepo wa serikali mbili na nusu.

Katika mfumo huu tunakuwa na serikali ya muungano wa Tanzania inayoundwa na viongozi wale wale wa Serikali za Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika inakuwa na serikali kamili kama ilivyo Zanzibar sasa halafu kunakuwepo na baraza la muungano la nchi mbili ambalo Rais wa baraza hilo anakuwa Rais wa Tanganyika na makamu wake anakuwa rais wa Zanzibar, kunakuwa na katibu wa baraza ambaye anapatikana kwa kupokezana kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar pamoja na wajumbe kutoka pande zote mbili kadri nchi hizi mbili kila moja itakavyojiwekea utaratibu wake wa ndani wa kuwachagua hao wajumbe wa baraza.

Zile hoja zote zinazoitwa za muungano kwa sasa ndio zinakuwa hoja ambazo zitashughuikwa na hilo baraza la muungano. Pia ili kuongeza au kupunguza jambo fulani kama hoja ya muungano mabunge ya nchi zote mbili lazima yapitishe au yaondoe jambo hilo kwa theluthi mbili ya kura.

Hapa tutakuwa tumepunguza gharama za kundesha muungano na pia ile hofu ya Rais wa muungano kuzidiwa nguvu na rais wa Tanganyika haitakuwepo. Mfano mzuri wa muundo huu ni kama Rais wa Zanzibar alivyo mwenyekiti wa baraza la mapinduzi pia.
 
Back
Top Bottom