Heri ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
570
3,792
Wasaalam mpendwa katika JMT 🇹🇿.

Huenda mimi na wewe hatukuwepo wakati Muungano wa 🇹🇿 ulipozaliwa, ila leo tumepata Neema ya kuwepo unapotimiza miaka 60. Tumeingia kwenye historia hii kubwa.

Nami nimefika mapema Sana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujumuika kuadhimisha, kusikiliza na kuelimika zaidi juu ya historia hii ndefu.

Heri ya Miaka 60 ya Muungano wa 🇹🇿🌹

IMG-20240426-WA0000.jpg

Tudumishe Amani na Mshikamano
Tusherekehe kwa kuwaenzi waasisi wetu kwa kukemea vitendo vya rushwa, ufisadi.
Ili wananchi wetu wapate maendeleo.

Kheri ya Muungano Dkt Gwajima...endelea kuchapa kazi
 
Wasaalam mpendwa katika JMT 🇹🇿.

Huenda mimi na wewe hatukuwepo wakati Muungano wa 🇹🇿 ulipozaliwa, ila leo tumepata Neema ya kuwepo unapotimiza miaka 60. Tumeingia kwenye historia hii kubwa.

Nami nimefika mapema Sana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujumuika kuadhimisha, kusikiliza na kuelimika zaidi juu ya historia hii ndefu.

Heri ya Miaka 60 ya Muungano wa 🇹🇿🌹

View attachment 2974160
View attachment 2974161
View attachment 2974162
Waliopaza sauti na kuhanikiza ,Asurubiwe,asurubiwe ni wale waliokuwa wanafaidika na mfumo wa utawala uliokuwepo wakati ule.Wengine ni wale machawa na wasiojitambua.Hizi ni sherehe zenu nyie mnaokula matunda ya mifumo yenu.Sherekeeni.
 
bila shaka unatoka kenya hakuna mtanzania mwenye ujasiri kama huu. Kiongozi kwetu huwa ni kupambwa tu😂😂usituletee matatizo kaa huko huko kwenu
 
Wasaalam mpendwa katika JMT .

Huenda mimi na wewe hatukuwepo wakati Muungano wa ulipozaliwa, ila leo tumepata Neema ya kuwepo unapotimiza miaka 60. Tumeingia kwenye historia hii kubwa.

Nami nimefika mapema Sana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujumuika kuadhimisha, kusikiliza na kuelimika zaidi juu ya historia hii ndefu.

Heri ya Miaka 60 ya Muungano wa

View attachment 2974160
View attachment 2974161
View attachment 2974162
SWALI .Habari waziri wetu....mungu abariki muungano wetu..serikali imefanya hatua kubwa kushughulikia kero za muungano kwa Muda wa miaka 60 sasa...swali ni lini serikali itakuja na wazo la kuunganisha hizi serikali ili iwe serikali moja?, kwasababu nchi ni moja kwann tusiwe na serikali moja? Kwann nchi moja imefuta jina lake, haina serikali, lakini kwa nchi ya upande wa pili mpaka sasa wanadai pasipoti kuingia zanzibar tena bila aibu kwenye muhimili wa bunge Tukufu?@Dkt. Gwajima D
 
Huu Muungano kati ya Nyerere na Abeid.Muungano ambao haukuconsult watu wa nchi zote mbili.Muungano gani Zanzibar kuna Rais wake.Tusiosherekea Muungano tujuane.
 
Huu Muungano kati ya Nyerere na Abeid.Muungano ambao haukuconsult watu wa nchi zote mbili.Muungano gani Zanzibar kuna Rais wake.Tusiosherekea Muungano tujuane.
Karibia watu wote waliopigania uhuru, na wale wamapinduzi hawapo tena.....wengine ni wazee nguvu zilikwisha muda tu.... ni sisi tuliopo sasa kuelewana, kutoka 2 twende 1.....maisha hayaendi kinyume nyume, hatuwezi kurudi nyuma tena....
 
Kwa Nini mtanganyika akienda Zanzibar haruhusiwi kumiliki aridhi tofauti na Huku Tanganyika ambapo wazanzibar wamejimilikisha mahekari na mahekari Hadi watanganyika wamekosa aridhi Yao?
 
Ndugu waziri, Tunaungana sote kwa furaha kusherehekea muungano wetu huu wa Jamhuri ya watu wa Tanzania

Licha ya hayo, bado muungano wetu umeendelea kuzaa kero nyingi kulikoni hata awali, na kero hizo huwenda zinatokana na mfumo mzima wa jinsi muungano wetu ulivyo

Tatizo la muungano wetu wa kutokuwa serikali moja, naamini kiini cha matatizo yetu yanatokea hapa

Je, tumewekeza juhudi gani kuwezesha kufikia kwenye serikali moja?

Ni kwa nini pia, karibu kila kero inayoibuka inatokea hasahasa kule Zanzibar?

Kama kiongozi wetu na ndugu Waziri, Ni kweli kwamba Zanzibar ndiyo yenye changamoto nyingi zinazotokana na muungano au ni Wabara ni watu wasiopenda kuzungumzia kero za Muungano
 
Wasaalam mpendwa katika JMT 🇹🇿.

Huenda mimi na wewe hatukuwepo wakati Muungano wa 🇹🇿 ulipozaliwa, ila leo tumepata Neema ya kuwepo unapotimiza miaka 60. Tumeingia kwenye historia hii kubwa.

Nami nimefika mapema Sana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujumuika kuadhimisha, kusikiliza na kuelimika zaidi juu ya historia hii ndefu.

Heri ya Miaka 60 ya Muungano wa 🇹🇿🌹

View attachment 2974160
View attachment 2974161
View attachment 2974162
Asante sana mama kwa kuonesha uzalendo mkubwa na kwa utumishi mzuri! Nipo tayari kushirikiana na wewe katika kujenga nchi yetu.
 
Back
Top Bottom