KWELI Kuna dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV ndani ya saa 72

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
PEP-HIV-Treatment-Medication-11.jpg

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
 
Tunachokijua
Njia ya kukukinga usipatwe na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira au hali hatarishi ipo. Kitaalamu huitwa Post-exposure prophylaxis, au kwa kifupisho PEP.

Kwa mujibu wa Miongozo ya Matibabu na Orodha ya Kitaifa ya Dawa Muhimu Tanzania Bara iliyotolewa na Wizara ya Afya mwaka 2021, PEP ni utumiaji wa haraka wa dawa ili kuzuia maambukizi kufuatia mazingira ambayo mtu anadhani yanaweza kumsababishia kupata maambukizi ya VVU (Mfano: kugusana kwa damu au maji maji mengine ya mwili).

PEP inasaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Hata hivyo, inaelezwa kuwa inapaswa kuanza PEP ndani ya saa 72, au siku 3, baada ya kuambukizwa au kuhisi kuambukizwa VVU, la sivyo haitafanya kazi.

Mtu aliyepitia mazingira hatarishi yanayoweza kumfanya aambukizwe VVU anapaswa kufika kwenye hospitali yoyote ya serikali ili apatiwe msaada, pamoja na kupimwa kwanza kama tayari ni muathirika wa VVU au la.

Dozi ya mwanzo inapaswa kutumiwa ndani ya saa 2 baada kuhisi kuambukizwa na kabla ya kumpima mtu mwenye mashaka.

Kwa Tanzania, TDF 300mg+3TC 300mg+DTG 50mg au maarufu zaidi kama TLD ndiyo dozi ya dawa inayotumika kwa watu wazima. Kwa watoto, AZT+3TC+LPV/r ndiyo hutumika.

Muongozo huo wa Wizara pia unaonesha kuwa dozi hiyo hutumiwa na watu wazima kwa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa siku 28, huku kwa watoto ikitumiwa mara mbili kwa siku katika muda wa siku hizohizo 28.
Na vipi vidonge vya N33 pia ni PEP nmeona mdau mmoja kavitaja pia?
kwanini Unatumia Coating Debossed Print kama Jina La Dawa?

Dawa Nyingi sana Zimeandikwa N33 ikiwemo Amphetamine plus Dextroamphetamine..
Ambazo sio Miongoni mwa Dawa za ARV..

Dawa nyingi Zinazotengenezwa Tanzania Zina chapa ya GOT..

Unataka kusema kuwa Hizo zote ni dawa aina moja kwakuwa zina jina la GOT??

Debossing Coated Zina maana nyingi sana Mkuu
amphetamine-and-dextroamphetamine (1).jpeg

Kama utakuwa na Jina la dawa Unaweza kuuliza Ni dawa gani ninawza kukujibu vizuri..
 
kwanini Unatumia Coating Debossed Print kama Jina La Dawa?

Dawa Nyingi sana Zimeandikwa N33 ikiwemo Amphetamine plus Dextroamphetamine..
Ambazo sio Miongoni mwa Dawa za ARV..

Dawa nyingi Zinazotengenezwa Tanzania Zina chapa ya GOT..

Unataka kusema kuwa Hizo zote ni dawa aina moja kwakuwa zina jina la GOT??

Debossing Coated Zina maana nyingi sana Mkuu
View attachment 2973789

Kama utakuwa na Jina la dawa Unaweza kuuliza Ni dawa gani ninawza kukujibu vizuri..
Hizi hapa mkuu... Pia ni PEP?
 
Attachments

  • images (7).jpeg
    images (7).jpeg
    24.4 KB · Views: 8
  • images (9).jpeg
    images (9).jpeg
    17 KB · Views: 8
Vp Whk ulikua na michubuko??
Ni dawa hizo LA 75 ndio ulitumia?
Vp ulipima baada ya muda gan?
Nilipima mwezi 1,3,6,8 nilikuwa na mchubuko pia na nilitumia izo izo dawa ARV na zilikuwa 38 mana aliyenipa alifanya kunichotea, nilikunywa kila siku saa mbili usiku zote zikaisha
 
Hizi hapa mkuu... Pia ni PEP?
Hiyo uliyotaja Hapa na uliyotaja kabla ya hapa...
Zote ni Dawa Aina Moja zinaitwa kwa Kifupi TLD..
Yaani Tenofovir+ Lamivudine+ Dolutegravir..

Ni sawa na ile ya kwanza uliyotaja ni dawa aina moja...
Kwa hiyo jibu ni Ndiyo TLD zote huweza kutumika kama PEP japo Haijakuwa Approved kutumika kama PrEP..(Pre Exposure)
 
View attachment 2333560

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
Naomba Nikurekebishe kidogo kwa ulichoandika kama hutojali..

Mtu akishaambukizwa hawezi kutumia PEP tena bali anatumia ARV kama Treatment na Ataandikishwa CTC moja kwa moja kupata Huduma ya Tiba na Matunzo..

Ulichondika inaweza kuwa Umeoverlook ila Kinaweza kuleta Shida endapo Mtu akaondoka na Tafsiri kuwa Ukiambukizwa unaweza ukazuia Maambukizi

Soma hapa chini..
Screenshot_20240425_222711_Chrome.jpg

"PEP inasaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Hata hivyo, inaelezwa kuwa inapaswa kuanza PEP ndani ya saa 72, au siku 3, baada ya kuambukizwa au kuhisi kuambukizwa VVU, la sivyo haitafanya kazi."

Kuwa Exposed Na Hiv Infection Sio kuwa Infected na HIV neno sahihi lilikuwa Ni kuhisi Kuambukizwa.. Hilo baada ya Kuambukizwa halikuwa sahihi kuwepo hapo

Shukrani na Asante
 
Hiyo uliyotaja Hapa na uliyotaja kabla ya hapa...
Zote ni Dawa Aina Moja zinaitwa kwa Kifupi TLD..
Yaani Tenofovir+ Lamivudine+ Dolutegravir..

Ni sawa na ile ya kwanza uliyotaja ni dawa aina moja...
Kwa hiyo jibu ni Ndiyo TLD zote huweza kutumika kama PEP japo Haijakuwa Approved kutumika kama PrEP..(Pre Exposure)
Zinaitwa Volutrip N33 from aurobindo
Hiyo uliyotaja Hapa na uliyotaja kabla ya hapa...
Zote ni Dawa Aina Moja zinaitwa kwa Kifupi TLD..
Yaani Tenofovir+ Lamivudine+ Dolutegravir..

Ni sawa na ile ya kwanza uliyotaja ni dawa aina moja...
Kwa hiyo jibu ni Ndiyo TLD zote huweza kutumika kama PEP japo Haijakuwa Approved kutumika kama PrEP..(Pre Exposure)
Mkuu ni Volutrip N33
From aurobindo
 
Ndio mkuu umeeleweka vyema kweli wewe ni nondo🔥🙌....
Sasa bas Nina swali hapo ikitokea mtu akaenda hospital akapewa LA75 vidonge vya siku15.. Je atakaporudi Tena na kupewa hivo N33 vidonge 15 ili akamilishe doz itakua ni sawa pia?

Maana vyote n generic version ya TLD.
Umenielewa Nilichokuambia hiyo Dawa jina Lake ni TLD? na kirefu chake nimekwisha kukupatia..
Mahospitalini tunaita Hivyo au kirefu Tenofovir+ Lamivudine+ Dolutegravir....

Umesoma Nilichoandika Kabla ya kujibu??
 
Ndio mkuu umeeleweka vyema kweli wewe ni nondo🔥🙌....
Sasa bas Nina swali hapo ikitokea mtu akaenda hospital akapewa LA75 vidonge vya siku15.. Je atakaporudi Tena na kupewa hivo N33 vidonge 15 ili akamilishe doz itakua ni sawa pia?

Maana vyote n generic version ya TLD.
Yeah akamilishe maana ni dawa moja hiyo
 
Baada ya kumaliza dozi ya pep inapaswa kupima baada ya muda gani doctor??
Baada ya Kumaliza Apime.., Akiwa Negative atapima Tena baada ya Miezi Mitatu then akikutwa Tena Negative atapima Tena baada ya Miezi sita..

Akipima akakutwa Positive Anatakiwa Kuwa Enrolled CTC
 
Baada ya Kumaliza Apime.., Akiwa Negative atapima Tena baada ya Miezi Mitatu then akikutwa Tena Negative atapima Tena baada ya Miezi sita..

Akipima akakutwa Positive Anatakiwa Kuwa Enrolled CTC
Asante sana mzee na ikitokea pep ilifail huo mwez mmoja wa pep vipimo vya vitasoma positive?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom