KWELI Kuna dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV ndani ya saa 72

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
PEP-HIV-Treatment-Medication-11.jpg

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
 
Tunachokijua
Njia ya kukukinga usipatwe na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira au hali hatarishi ipo. Kitaalamu huitwa Post-exposure prophylaxis, au kwa kifupisho PEP.

Kwa mujibu wa Miongozo ya Matibabu na Orodha ya Kitaifa ya Dawa Muhimu Tanzania Bara iliyotolewa na Wizara ya Afya mwaka 2021, PEP ni utumiaji wa haraka wa dawa ili kuzuia maambukizi kufuatia mazingira ambayo mtu anadhani yanaweza kumsababishia kupata maambukizi ya VVU (Mfano: kugusana kwa damu au maji maji mengine ya mwili).

PEP inasaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Hata hivyo, inaelezwa kuwa inapaswa kuanza PEP ndani ya saa 72, au siku 3, baada ya kuambukizwa au kuhisi kuambukizwa VVU, la sivyo haitafanya kazi.

Mtu aliyepitia mazingira hatarishi yanayoweza kumfanya aambukizwe VVU anapaswa kufika kwenye hospitali yoyote ya serikali ili apatiwe msaada, pamoja na kupimwa kwanza kama tayari ni muathirika wa VVU au la.

Dozi ya mwanzo inapaswa kutumiwa ndani ya saa 2 baada kuhisi kuambukizwa na kabla ya kumpima mtu mwenye mashaka.

Kwa Tanzania, TDF 300mg+3TC 300mg+DTG 50mg au maarufu zaidi kama TLD ndiyo dozi ya dawa inayotumika kwa watu wazima. Kwa watoto, AZT+3TC+LPV/r ndiyo hutumika.

Muongozo huo wa Wizara pia unaonesha kuwa dozi hiyo hutumiwa na watu wazima kwa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa siku 28, huku kwa watoto ikitumiwa mara mbili kwa siku katika muda wa siku hizohizo 28.
Mkuu vipi?
Safi asee.... Kuna issue ilimtokea jamaa ang ikabidi nimconnect kwa mtu wa CTC alilala na mdada ambae ni HIV(+) alianza dawa hizi 39hours after exposure na mpaka sasa yupo kwenye dose.,,, Hizo dawa hapo juu LA75 hutumika kama PEP na ufanisi wake upoje kwa waliowahi zitumia?
 
Mmmh sio wewe mkuu?
 
Nashukuru sana bro... Maana ilikua ni sex baada ya kuona mchubuko kwenye uume wake jamaa ikabidi amtafute dem ampime ndipo kukuta yupo positive....so ikabidi afanye mpango huo ndio kupata hizo ndan ya saa 39 LA75 na leo day 13 yupo kwenye dozi...
Sawa Huwa ni ngumu kupata Ngwengwe Kwa ngono ya Mara Moja tu japo ingawa Huwa pia inatokea.

Ila huyohuyo Demu itakua ni rahisi kama angefanga naye ngono Mara Kwa mara Kwa nyakati tofauti.

Mwanangu, tushitukke , tuakataeni, tusiwahi Kufa.

Ngoma ukiipata sahizi unamiaka yako 30 ... Sawa utatumia dawa ila unakuja kufa miaka kwenye 50 hivi..

Wakati miaka 50 ni umri Sasa wa kurudi kua Kijana huku ukitusua mahela yako na kumjua Mungu .
 
Nashukuru sana bro... Maana ilikua ni sex baada ya kuona mchubuko kwenye uume wake jamaa ikabidi amtafute dem ampime ndipo kukuta yupo positive....so ikabidi afanye mpango huo ndio kupata hizo ndan ya saa 39 LA75 na leo day 13 yupo kwenye dozi..
Nashukuru sana bro... Maana ilikua ni sex baada ya kuona mchubuko kwenye uume wake jamaa ikabidi amtafute dem ampime ndipo kukuta yupo positive....so ikabidi afanye mpango huo ndio kupata hizo ndan ya saa 39 LA75 na leo day 13 yupo kwenye dozi...
Dr mambo

DR Mambo Jambo quote hapa mkuu
 
View attachment 2333560

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
Kuna Hawa Wana dawa zinazozuia maambukizi na kuzuia HIV Virus kuongozeka Medicines | Gilead
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom