KWELI Kuna dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV ndani ya saa 72

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
PEP-HIV-Treatment-Medication-11.jpg


Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
 
Tunachokijua
Njia ya kukukinga usipatwe na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira au hali hatarishi ipo. Kitaalamu huitwa Post-exposure prophylaxis, au kwa kifupisho PEP.

Kwa mujibu wa Miongozo ya Matibabu na Orodha ya Kitaifa ya Dawa Muhimu Tanzania Bara iliyotolewa na Wizara ya Afya mwaka 2021, PEP ni utumiaji wa haraka wa dawa ili kuzuia maambukizi kufuatia mazingira ambayo mtu anadhani yanaweza kumsababishia kupata maambukizi ya VVU (Mfano: kugusana kwa damu au maji maji mengine ya mwili).

PEP inasaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Hata hivyo, inaelezwa kuwa inapaswa kuanza PEP ndani ya saa 72, au siku 3, baada ya kuambukizwa au kuhisi kuambukizwa VVU, la sivyo haitafanya kazi.

Mtu aliyepitia mazingira hatarishi yanayoweza kumfanya aambukizwe VVU anapaswa kufika kwenye hospitali yoyote ya serikali ili apatiwe msaada, pamoja na kupimwa kwanza kama tayari ni muathirika wa VVU au la.

Dozi ya mwanzo inapaswa kutumiwa ndani ya saa 2 baada kuhisi kuambukizwa na kabla ya kumpima mtu mwenye mashaka.

Kwa Tanzania, TDF 300mg+3TC 300mg+DTG 50mg au maarufu zaidi kama TLD ndiyo dozi ya dawa inayotumika kwa watu wazima. Kwa watoto, AZT+3TC+LPV/r ndiyo hutumika.

Muongozo huo wa Wizara pia unaonesha kuwa dozi hiyo hutumiwa na watu wazima kwa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa siku 28, huku kwa watoto ikitumiwa mara mbili kwa siku katika muda wa siku hizohizo 28.
Usiudanganye umma Mzee wangu, waambie ukweli tu watakuelewa hvohvo.
Ambacho hakiko sawa ni aina ya exposure, sababu ndio naona hiyo 50/50 uliyotaja hukusema ni exposure gani, kama ni vaginal penetration na pep ianze within 72 hours, odd ni 99%

Anal sex odd itashuka sababu anal fluid ina viral load kubwa mara 10 zaidi ya vaginal fluid

Kuchomwa na sindano iliyotumika na mwenye HIV odd ni sawa na vaginal penetration

Pep practice through vaginal penetration exposure inatokea kwa watu kila siku na wanatoka salama baada ya dose

Na si kweli kuwa kuwa hakuna dawa rasmi ya kuzuia maambukizi, CDC wanaelekeza PEP kama official emergency drug, PREP pia ni official drug kwa watu walio kwenye exposures kila mara kama sex workers
 
Pep zipo ila asikudanye mtu kuwa utazipata bure zahanati /kituo cha afya.

Sahau , ufanyaji kazi wake ni kabla ya masaa 72 ulivyokuwa exposed kwa mtu anayedhaniwa kuwa muathirika .

Ndugu PEP zina mambo yake pia japo ni katika siku za mwanzoni.

1/ukizitumia lazima uwe na kinyesi laini kama sio kuharisha kabisa.

2/Zinakuhitaji ule chakula ushibe maana kwa siku za mwanzo utajihisi uchovu .

Kuhusu sijui kuota ndoto za ajabu mara maluweluwe ni wenge la mtu mwenyewe ila hamna ujinga kama huo .

3/Nina siri moja ya PEP katika hizo siku 28 jinsi ya kuzitumia within a week tu .
Hili litaendana na baadhi ya maelezo ya mtoa komenti mmoja hapa kazungumzia habari ya anal sex na vaginal sex lakini pia contamintal effect zinazoweza kutokea.

Japo sitamani kueleza hayo sababu nitakuwa naenda kinyume na maelekezo ya dawa zenye na miongozo ya Afya.

Ukipita huko ukajihisi umepita kubaya wahi tukupe hizi dawa , achana na gharama mnazopigwa kwa vishoka wa ugawaji wa PEP na PREP.
 
Zipo ila dozi yake ukiwa unakunywa utakuwa ukiota ndoto za kuvutwa na mizimu ya mababu zako yaani utakuwa na ukimwi uliochangamka kwa kipindi cha dozi ...aweee so poa tujilindeni
Niliwahi kutumia kwa muda wa siku 3 tu, nikaacha, macho yalikua yanakua mekundu sana.
 
Dogo usikurupuke Kama changudoa wa Mbagala. Soma ukiwa umetulia. Sija ongea kuhusu gharama za PEP Ila nimesema adha ya kunywa dawa siku 28.
Sijakurupuka wewe ndo usome vizuri ulichoandika,na kwa taarifa yako PEP haziuzwi kwenye maduka ya dawa
 
Hizo dawa zipo lakni enyewe umeza kwa sku 5 kwanza ndupo utapata kinga dhidi ya ukimwi na ni muendelezo kunywa mpaka pale utakuwa mbali na hatari ya kuambikizwa ukimwi.. Kwa mfano mtu kazi yake ni kujiuza kwa njia ya ngono. Huyo kwenye hatari kwa hiyo huyo mtu anatakiwa ameze hizo dawa kwa siku 5 kwanza ndipo aendelee kufanya kazi yake ya umalaya na kuendelea kumeza hizo dawa mpaka hapo atakapo acha hyo kazi yake. Nawasilisha
 
Pigeni pipe vijana wala msiwaze. Ukishakutana na dubwana ndio itajulikana kama zipo au hazipo
 
Ila zinatolewa sio kwa wazinzi ni kwa watu walio bakwa, Madaktari waliopata shida wakitekeleza majukumu yao, na is not 100% sure, so jitunze
Watutengenezee na sisi wazinzi watugawie Kama condoms. Ili uku kimboka tule shangwe
 
Big NO, 50/50 Hapana, PEP prevention odd ni 99% kama ikitumika within 72HRS post exposure
Ni sahihi. Teja walinishambulia nilipita kwenye anga zao nikabahatika kuwatembezea kibano walikuwa SITA. Nilicharaza wote ila kwenye purukushani waliniuMa mikono, shingo, mguu nk

Bahati nzuri wasamaria wakafika tukawakalisha wale mateja mpaka police wakafika.

Kufika police post ikabidi vifanyike vipimo, ebhana mmoja TU kati Yao ndo hakuwa muathirika wa VVU. Hivyo Kwa kuwa waliniuma ikabidi nianzishiwe hiyo PEP.


Nilitumia ndani ya mwezi mzima, na pombe nilikuwa nazikata kama mahi bila shida yoyote.

Mwezi ulipita nikapima ngoma negative.

Nikagongaga Tena limalaya Fulani hivi nimeliopoa huko bar, kondom ikapasuka ila mautamu ya mbususu nikapiga hvyo hvyo, heeeh nikaona kikopo Cha dawa zake kumuuliza akanambia tayari anavyo.

Ikabidi mapema tu nimpigie doctor wangu aniandalie mzigo.

Sasa imebidi nichukue kabisa stock nimeihifadhi Kwa dharura
 
Umeieleza vyema PEP, Asante mkuu,
Kiujumla nadhani dawa rasmi ya kuzuia maambukizi haipo, Bali Kuna hio Post Exposed prophylaxis, nayo ni 50/50 utendahi KAZI wake. Ambazo hiz ni dawa rasmi watumiazo waathirika WA VVU basi mtu hupatiwa Kwa haraka na kuzitumia Kwa takribabi mwezi mmoja , wengii hii huwasaidia .
Asante kwa elimu mkuu ila kuna jambo nahitaji kulijua vzur limenipa ukakasi pia ni kukosoe kidogo hapo kwenye indication ya 50/50, indication ya pep ni 99% endapo itatumiwa kwa ufasaha.

Nachohitajikukifahamu ni hapo uliposema kwamba pep ndo hzi ARV wanazotumia waathirika kufubaza makali ya virusi!, ni aina ipi ya ARV ambayo hutumika kama PEP sabu hta hizi ARV pia zimegawanyika sio aina moja zipo aina kama 3 sasa hizi ambazo ndizo PEP ni aina ipi ya ARV?

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Ni sahihi. Teja walinishambulia nilipita kwenye anga zao nikabahatika kuwatembezea kibano walikuwa SITA. Nilicharaza wote ila kwenye purukushani waliniuMa mikono, shingo, mguu nk

Bahati nzuri wasamaria wakafika tukawakalisha wale mateja mpaka police wakafika.

Kufika police post ikabidi vifanyike vipimo, ebhana mmoja TU kati Yao ndo hakuwa muathirika wa VVU. Hivyo Kwa kuwa waliniuma ikabidi nianzishiwe hiyo PEP.


Nilitumia ndani ya mwezi mzima, na pombe nilikuwa nazikata kama mahi bila shida yoyote.

Mwezi ulipita nikapima ngoma negative.

Nikagongaga Tena limalaya Fulani hivi nimeliopoa huko bar, kondom ikapasuka ila mautamu ya mbususu nikapiga hvyo hvyo, heeeh nikaona kikopo Cha dawa zake kumuuliza akanambia tayari anavyo.

Ikabidi mapema tu nimpigie doctor wangu aniandalie mzigo.

Sasa imebidi nichukue kabisa stock nimeihifadhi Kwa dharura
We jamaa ni balaa. Kwamba umeweka stock kikinuka tu unameza
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom