mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 81,638
- 107,696
Ongezea...Kama unatumia Bodaboda hasa maeneo ya mjini tuzingatie sana
1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii
2. Usipande pikipiki ambayo dereva hajavaa Kofia/helmet
Ile kofia inakioo kinachozuia wadudu wanaoingia machoni na hata vumbi anapopishana na magari makubwa; Fikiria boda anakimbia KMS 70, halafu wadudu wamuingie machoni; ushukuru sana Mungu kama hutaishia kwenye mtaro au hata kugongwa...
Ushauri: Vile vioo vya pembeni vyote viwili havizidi shs 10,000 hivyo kama una bodaboda wako, unaweza kumnunulia/kumkopesha. Kofia ngumu ya kawaida ni kwenye shs 20,000=
1)bodaboda kavaa ndaraa
2)bodaboda kasuka virasta,kanyoa kiduku huku muda wote kafungulia singeli na amapiano
Ova