Fundi manyumba

Senior Member
Nov 25, 2018
177
287
"""Dah Zuchi, Mungu amlaze mahala pema peponi 🙏 nakumbuka wakati na Show ya #ThePlaylist ikabidi nitafute mtu mkali wa kufanya nae Professional Photoshoot nikakutana na Zuchi kipindi iyo anajitafuta na Studio yake Mwenge ndani ndani!

Akawasha midude hatari sana na kutokea apo ikawa kila kazi tunapiga nae na watu wakibao wakamuamini zaidi, njaa yake ya kutamani kupiga picha kali ikampeleka mpaka kwa Millard na kufanya kazi kupitia Ayotv, Pole sana @millardayo pole kwa familia, ndugu na jamaa 🙏 M/Mungu amlaze mahala pema peponi 🙏. """Lulyommy

1714138285113.jpg
1714138292873.jpg
IMG-20240426-WA0023_1.jpg


======

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU KIFO CHA ZUCHY - MPIGA PICHA WA AYOTV
———
Kuna taarifa yenye kichwa cha habari SHUHUDA inayosambazwa katika mitandao ikieleza

“Zuchy kapata ajali na boda hit and run mbele ya mataa ya masana kama 100 mita hivi toka saa nane usiku dereva wa boda akapelekwa hospital. Umoja wa bodaboda wamekaa na mwili barabarani pale wakiita Polisi kisingizio gari haina mafuta kweli. Pia tarifa hiyo inaeleza bodaboda walikaa na mwili hadi wakafunga barabara ili kushinikiza Polisi waitwe.”

Kwanza, Jeshi la Polisi linasema hili ni tukio la huzuni na la kusikitisha kwasababu tumempoteza Mtanzania mwenzetu katika ajali hiyo.

Pia lingependa kueleza kuwa, tukio hilo liliripotiwa saa kumi na dakika kumi na mbili alfajiri kuwa, kuna ajali imetokea eneo la Mbezi Makonde. Baada ya kupokelewa tarifa hiyo Maafisa na Askari waliokuwa kwenye majukumu katika mkesha wa Tamasha la Shangwe la Utawala lililokuwa linafanyika eneo la Tanganyika Packers waliondoka wakiwa na gari ya Polisi kuelekea eneo la tukio na kuchukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Mwananyamala kwa taratibu zingine za kisheria.

Askari waliofika eneo la tukio katika uchunguzi imebainika marehemu alipata ajali na pikipiki aliyokuwa amepanda yenye namba MC 436 CMU iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye
alipata majeraha na anaendelea na matibabu.

Hivyo, mara baada ya tarifa ya tukio hilo kutolewa na kupokelewa, Maafisa na Askari Polisi walifika kwenye tukio kwa wakati na kutekeleza yale yanayopaswa kutekelezwa kwenye eneo la ajali.

Tunawashukuru bodaboda wa eneo hilo wanaojali utu wa binadamu kwa kuzuia magari yasimkanyage marehemu.

Endapo kuna mwenye tarifa tofauti na si za uzushi/uwongo kama hizo zinazosambazwa azifikishe kwa viongozi ili zifanyiwe kazi na hatua zichukuliwe.
e073558cd6d474749b89653580b2b49d.jpg


Pia soma
 
p
"""Dah Zuchi, Mungu amlaze mahala pema peponi 🙏 nakumbuka wakati na Show ya #ThePlaylist ikabidi nitafute mtu mkali wa kufanya nae Professional Photoshoot nikakutana na Zuchi kipindi iyo anajitafuta na Studio yake Mwenge ndani ndani! Akawasha midude hatari sana na kutokea apo ikawa kila kazi tunapiga nae na watu wakibao wakamuamini zaidi, njaa yake ya kutamani kupiga picha kali ikampeleka mpk kwa Millard na kufanya kazi kupitia Ayotv, Pole sana @millardayo pole kwa familia, ndugu na jamaa 🙏 M/Mungu amlaze mahala pema peponi 🙏. """"
poleni sana
 
Ajali imetokea jana usiku mida ya saa 8 nadhani, boda boda wa mbezi wamefika eneo la tukio wanawapigia simu polisi kuwapa maelezo ya tukio ili wafike kwa wakati lakini ajabu jibu walilotoa askari linafikirisha sana..

Jibu walilotoa polisi walisema Gari yao haina MAFUTA ☹️,boda boda ilibidi waustili mwili vizuri ili hali ukiendelea kubakia eneo lile ukinyeshewa na mvua😢, mpaka ilipofika leo mida ya saa 4 asubuhi ndipo askari waliweza kufika eneo la tukio na kuutoa mwili wa marehemu kuupeleka hospitali.

TUKIO LA JANA NI UDHIHIRISHO TOSHA KUWA TUNA ASKARI WAPUMBAVU ZAIDI YA NENO LENYEWE WASIOKUWA NA WELEDI WOWOTE NA KAZI YAO 😒😠
 
Pole sana mkuu...
Nchi zilizoendelea zilishapiga marufuku haya matakataka mjini.

Kwanza zinachafua mji, zinaongoza kwa kuleta ajali na kuua vijana.
Sina la kusema mkuu, maana kuna wanaotegemea kuishi kwa hizo boda hivyo siwezi kuziita takataka labda sheria zikaziwe, usalama uzingatiwe watozwe faini kali huenda ikapunguza tatizo hali ni mbaya boda zinaua sana barabarani
 
Back
Top Bottom