DOKEZO Amewasilisha Polisi malalamiko ya ndugu yake kuuawa lakini Askari wa Kituo cha Polisi Kibaha wanamzungusha tu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Tarehe 24/01/2024 Ndugu Hamis Athumani Mkazi wa eneo la Mashamba Pori, Kibaha Mkoani Pwani aliuliwa kwa kupigwa na machepe.

Siku ya tukio Marehemu alikuwa nyumbani kwake eneo la Mashamba Pori akapigiwa simu katika simu yake no. 0654281507, akaelekezwa aende eneo la Pangani ambalo ni kama Kilometa 4 kutoka nyumbani, alifanya hivyo kwa kuwa waliomuita ni watu anaofahamiana nao na anafanya nao kazi hasa za vibarua.

Alipofika eneo hilo la Pangani akawakuta Watu nane wakati huo tayari kulikuwa na Viroba nane vya kokoto pembeni, yasemeka walianza kuzozana huku watu hao wakimtaka atoe Shilingi Laki Tano ambayo hakuwa nayo na akawasihi wasimshambulie huku akidai mfukoni ana Sh 50,000 tu.

Akawasisitiza kuwa kama wanataka hizo Laki Tano wampigie simu Mama yake kwa simu yake ambayo walikuwa wameshamnyang'anya lakini hata hivyo walikataa na kumshambulia hadi kufa.

Watu walivyoanza kujitokeza baada ya kusikia purukushani, wale jamaa wakadai Hamis ni mwizi wa Kokoto na wamemkuta anaiba, Wananchi kusikia hivyo wakiwemo Bodaboda wakatoa Petrol kwenye Pikipiki zao na kuanza kumbabua kwa Moto.

Mwili Marehemu ulikaa hapo kuanzia alivyouliwa Saa 4 Asubuhi hadi Saa Tisa Alasiri ndipo Askari Polisi wa Wilaya ya Kibaha walipofika eneo hilo kuchukua Mwili na kuupeleka Mochwari.

Jambo la kushangaza kesi iliyofunguliwa hapo Kibaha ni kosa la kujeruhi KBH/IR/333/2024 ya tarehe 24/01/2024, Mpelelezi SGT Ombeni wa Ofisi ya OC CID Kibaha na Mkaguzi wa tukio hilo alikuwa Insp Peter wa Kituo cha Polisi Kibaha.

Kaka wa Marehemu Salehe Athumani mwenye simu namba 0712249269 alifika baada ya kupata taarifa na alikabidhiwa mwili wa ndugu yake tarehe 25/01/2024 na Mpelelezi SGT Ombeni kwa ajili ya kwenda kumhifadhi mpendwa wao.

Baada ya hapo alianza kufuatilia ikiwa ni pamoja na kufika nyumbani kwa Marehemu ambapo alipata taarifa nyingi kuhusiana na kifo cha mdogo wake na kukugundua kuwa hakua mwizi bali kulikuwa na visa vya wivu.

Akaenda hadi Kituo cha Polisi Kibaha kumuona Mpelelezi SGT Ombeni na baada ya kumuekeza yote kuhusiana na kifo cha Mdogo wake pamoja na kutaja hadi majina ya washukiwa waliomuua mdogo wake kuwa ni Watu ambao walikuwa wakishikiana kwenye kazi mbalimbali kwa kuwa marehemu alikuwa Fundi na wauaji mara nyingi walikua wasaidizi wake.

Licha ya maelezo yote hayo bado Mpelelezi SGT Ombeni alimuelekeza aende akawalete Watu walioshudia wakati wanamuua Mdogo wake lakini hata kabla ya hapo kuna mtu alielekezwa aende akaandike maelezo alichoshuhudia lakini inadaiwa baada ya hapa alitakiwa kutorudi tena pale kituoni na wala kutoeleza alichoongea kule Polisi.

SGT Ombeni akamuelekeza kaka wa marehemu kwenda kwa OC CID, akafanya hivyo kwa kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi, akamueleza kila kitu anachokijua na kumtajia majina ya washukiwa wa mauaji, nae akamwambia aondoke akatafute shuhuda wa tukio ambaye yupo tayari kutoa maelezo.

Kufikia hatua hiyo ndugu wa marehemu hakuwa na la kufanya tena zaidi ya kutafuta usafiri wa kurudi Kijijini kwake Makanya Wilaya ya Same.

Hilo ndio Jeshi la Polisi Tanzania.
 
Hiyo ni sheria gani ya kumtuma mtu akalete shahidi?
Je ndio walivyofundisha wakipata taarifa ya kifo au mashtaka wanafanya hivyo?

Kweli jeshi la polisi linaendeshwa hivyo jamani mbona bajeti yao kubwa sana
Kwanini bado wapo kazini hao? Na je hakuna mkuu wa kituo
Tunaomba wanasheria waje hapa
 
Poleni sana!!
Achana na polisi utapoteza muda wako bure!!

Iteni wanamaombi ndani ya nyumba ya marehemu,

Ombi kuu ni kumshukuru Mungu Kwa zawadi uhai wa marehemu na maisha yake duniani Hadi kifo chake! Pia mmshukuru Mungu Kwa uhai wa waliomuua Marehem na muombe mapenzi yake Mungu yafanyike!
 
Daah ila polisi wetu hawa. Hapa nawaza kumpeleka jamaa polisi alinitapeli hela ila sijui kama nitasaidika na ushahidi nilionao ni wa msg tu.
 
Sitaongelea ishu kuu ya huu uzi.

Ila mimi imenikuta pia askari kuniambia ama nikatafute mashahidi au nikamkamate mhalifu nimlete.
Askari wa siku hizi wamekuwa wazembe , hawataki kufanya majukumu Yao kabisa, sasa kazi ya kumkamata muhalifu ni ya raia au Askari?
 
Back
Top Bottom