SoC04 Tanzania Tuitakayo: Kilimo biashara kitainua uchumi wa nchi na kuondoa umasikini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Xpertz

Member
May 3, 2024
8
6
UTANGULIZI
Sekta ya kilimo nchini Tanzania bado imekua na changamoto kubwa ya kutokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje mchango wake kwa pato la taifa bado ni mdogo pia. Pamoja na jitihada za Serikali kuongeza nguvu kwenye kilimo cha uhakika cha umwagiliaji ila dira ya taifa inapaswa kujikita kwenye kilimo BIASHARA cha KIMKAKATI ili kiwe na tija kwa uchumi wa nchi hasa ikizingatiwa kilimo kinaajiri zaidi ya asilimia 70 ya watanzania. Mambo yafuatayo nashauri yafanyike kufanikisha kilimo BIASHARA chenye tija nchini:

1. Uzalishaji wa mashamba makubwa kwa mazao ya KIMKAKATI
Nashauri serikali ijikite kuwezesha wakulima mitaji, pembejeo na ruzuku kwa ajili ya kufanikisha kilimo cha mashamba makubwa cha mazao ya kimkakati yenye uhitaji mkubwa katika soko la ndani na nje ya nchi ikiwemo nafaka kama ngano, miwa (sukari) na alizeti. Kwenye hili serikali ifungue milango kwa mabenki kutoa mikopo nafuu kwa wakulima pamoja na kuvutia wawekezaji wengi kwenye uzalishaji huo wa kimkakati pia iwapunguzie utitiri wa kodi na vikwazo vya kiuwekezaji.

2. Iundwe tume ya masoko ya mazao ya kilimo
Taasisi hii iwe na jukumu la kuunganisha wazalishaji(wakulima)au vyama vya wakulima na wateja ndani na nje pamoja na kusimamia miongozo ya bei zenye tija kwa wakulima. Soko la chakula ni kubwa afrika mashariki na kati na hata duniani ila bado kuna pengo kubwa baina ya wakulima wetu na masoko mfano wazalishaji wakubwa wa nyanya Dumila Morogoro kuna wakati wanakosa pa kuuza nyanya zao na wakati mwingine kupata hasara

3. Serikali ijikite kuanzisha viwanda vya uchakataji mazao ya kimkakati kila eneo
Hii itasaidia wakulima kuongeza thamani ya mazao yao kabla ya kuyaingiza sokoni. Itasaidia kuuza bidhaa badala ya malighafi. Wawekezaji wavutiwe kujenga viwanda maeneo yote yenye uzalishaji mkubwa wa kimkakati

4. Elimu ya teknolojia za kisasa za kilimo itumike kumkomboa mkulima.
Serikali ihakikishe wakulima wote vijijini wanaachana na kilimo cha mazoea, wafikishiwe elimu ya teknolojia mpya za kilimo zenye tija zaidi ikiwemo matumizi ya mbegu bora, mbolea na viuatilifu. Mashamba darasa ya mkakati kila kata inayozalisha zao fulani yaanzishwe ili kuwapa wakulima elimu bora ya teknolojia mpya kwa vitendo

5. Vijana wavutiwe kwenye kilimo.
Serikali itoe mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vingi zaidi vya wakulima vijana kwenye uga wa mazao ya kimkakati sambamba na kuwapa ruzuku ya pembejeo muhimu kuwawezesha kuwa nguzo ya kilimo BIASHARA nchini Tanzania kwa kizazi cha sasa na baadae
 
Iundwe tume ya masoko ya mazao ya kilimo
Taasisi hii iwe na jukumu la kuunganisha wazalishaji(wakulima)au vyama vya wakulima na wateja ndani na nje pamoja na kusimamia miongozo ya bei zenye tija kwa wakulima. Soko la chakula ni kubwa afrika mashariki na kati na hata duniani ila bado kuna pengo kubwa baina ya wakulima wetu na masoko mfano wazalishaji wakubwa wa nyanya Dumila Morogoro kuna wakati wanakosa pa kuuza nyany
Hapa ndipo penyewe.

Tuje na sera na nyenzo na watu wa kutusaidia hili suala asee. Masoko, masoko, masoko ✔

Serikali ijikite kuanzisha viwanda vya uchakataji mazao ya kimkakati kila eneo
Hii itasaidia wakulima kuongeza thamani ya mazao yao kabla ya kuyaingiza sokoni. Itasaidia kuuza bidhaa badala ya malighafi. Wawekezaji wavutiwe kujenga viwanda maeneo yote yenye uzalishaji mkubwa wa kimkakati
Kuna documenti ziliwahi kutolewa na taasisi ya uwekezaji, walitoa kila mkoa fursa za uwekezaji shime sasa kuwezesha uwekezaji wa ndani na wa nje kwenye viwanda hivyo. Ahsante kwa andiko lililoshiba.
5. Vijana wavutiwe kwenye kilimo.
Serikali itoe mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vingi zaidi vya wakulima vijana kwenye uga wa mazao ya kimkakati sambamba na kuwapa ruzuku ya pembejeo muhimu kuwawezesha kuwa nguzo ya kilimo BIASHARA nchini Tanzania kwa kizazi cha sasa na baadae
Kijana amevutiwa na betting kwa kuiona fursa, hata kilimo kikijionesha (kupitia mifumo ya masoko na usambazaji) kuwa ni dili. Wawekezaji vijana watajaaa hadi tushangae. Waone kuna fursa ya mtonyo tu.
 
Back
Top Bottom