SoC04 Serikali ifanye haya kuboresha Sekta ya Kilimo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Apr 20, 2024
26
11
Katika Tanzania tuitakayo Serikali iboreshe katika sekta ya kilimo kwani ndio uti wa mgongo katika kuimalisha uchumi wa nchi yetu. Mambo yakufanyiwa kazi ni pamoja na:-

1. Kutoa elimu juu ya hatua zote za kilimo husika(tangu kuandaa shamba hadi kuvuna) kwa wadau wote wa kilimo.
2. Kuboresha nyanja za kilimo ikiwa ni pamoja na matumizi ya mashine za kisasa zinazoendana na wakati.
3. Kuboresha uzalishaji wa mbegu bora za mazao pamoja na dawa nzuri za kuyalinda mazao dhidi ya wadudu waharibifu.
4. Kupanua wigo wa kilimo cha umwagiliaji(irrigation scheme) katika maeneo yote yenye kuruhusu uwekezaji ktk kilimo .
5. Kuhakikisha mkulima ananufaika na bei za mazao katika msimu wowote .
6. Kutenga maeneo makubwa kwaajiri ya kilimo pendekezwa kitakachoendeshwa kwa hatua za kisasa zaidi na kitaalamu kwani itakuwa chanzo cha ajira pia.
a60952def699c0bddc0b19bbb5709c28.jpg
kilimo cha kisasa na kitaalamu.
 
. Kuhakikisha mkulima ananufaika na bei za mazao katika msimu wowote
Nakazia hapa.

Hapa mwisho pakitengemaa, basi mnyororo wote utavuta kilimo kwenda mbele.

Kuna watu watajitokeza kuuza ujuzi na elimu kukiwa na SOKO.

WApo watakaojitokeza kusindika bidhaa kukiwa na Soko IMARA.

Wasomi na wawekezaji wenye mitaji watajikita huko na ndio utakuwa mwanzo wa mapindizi makubwa katika ajira, uchumi na kila kitu.
 
Back
Top Bottom