Mlioanzisha mahusiano humu ndani kwa mbwembwe na baadaye mkaachana, mko wapi?

Mh asee waja mna mambo ,ya sirini kweli haya au...ngoja niweke kiti hapa Fake P come here msichana
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Nimechelewa kupata Notification Oky nikiweka jambo langu huu uzi hautakua na maisha i swear. Hogopa
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
 
.......sisi watu wa humu sio watu spesho na timilifu, ni binadamu wa kawaida kama wengine huko mitaani, tunapitia changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii na kimahusiano au hata kiafya kama watu wengine.......
.......sioni kama busara sana kuwananga na kuwanyanyasa watu ktk mitandao as if kuna mambo walitukosea au hata kama tuliwataka wakatukataa, mbaya zaidi tunawataja na I'd zao, tujifunze kujadili vitu vyenye tija kuliko kujadili personal issues za watu, hawa memba tunaowataja hapa wana michango mikubwa sana kuifanya jf kuwa sehemu nzuri ya kupata maarifa na kupumzisha akili, tuwaheshimu basi hata kwa hayo waliotupatia, tusiwafanye wakimbie mahali hapa, please guys!!!........
........licha ya kuwa mtandao wa jf unaaminika kujaa watu waelewa na wasomi wa viwango tofauti, lakini unaweza kuwa mtandao wa kwanza unaotumika kunyanyasa watu wa makundi mbalimbali i.e single moms, waliochelewa kuolewa, wahitaji, walimu na watu waliofanikiwa kifedha(kuwasema ni wauza ngada au mashoga hasa hawa celebrates).......
.........nb:hakuna anaependa kuvunja mahusiano au kuachwa, sio sifa kuachana lakini pia sio crime au dhambi, wanaumia kama watu wengine, tuwe faraja kwao, tusiwe sehemu ya maumivu kwao, hongera wote mliodumu ktk mahusiano na ustawi mzuri wa ndoa zenu.......
Umeongea mambo ya msingi sana mkuu maana muda si muda uzi huu unaweza kugeuka uwanja wa cyber bullying kwa watu kuja kulipiza visasi kwa ama kukataliwa au kuachwa/kuachana. Soon utashangaa ishakuwa vita ni vita mura!

Najua tunatofautiana emotional intelligence/maturity lakini tujitahidi sana maumivu ya kuachwa/kukataliwa/kuachana kwetu yasiwe sababu ya kudogosha na kunyanyasa wengine kihisia hapa. Na kipimo kimojawapo cha ukuaji wa mtu (hasa mwanaume) kisaikolojia ni pale unapokuwa na uwezo, sababu na hata nafasi ya kumuumiza mtu (emotionally, physically na vinginevyo) lakini ukajizuia. Nimejifunza hili na naendelea kujifunza tena kwa gharama kubwa sana!

...and guess what? Labda kama wewe ni sadist au social misfit lakini katika kuumiza wengine mara nyingi mtu anayeumia zaidi na kubakia na makovu ni wewe unayeumiza na siyo muumizwaji hasa kama muumizwaji ni mtu anayejitambua. Kamwe huwezi kujaribu kumpaka mtu matope halafu wewe ukabakia msafi! Ndiyo maana ya msemo kwamba "I hurt myself more by trying to hurt you!" πŸ™πŸΏ

Ndiyo. Kukataliwa, kuachwa na kuachana kunauma sana lakini maumivu hayo kamwe hayawezi kupozwa kwa kuchafua na ku-bully wengine. Kufanya hivyo ni kujitonesha hisia upya na kujiongezea maumivu tu. Mungu na Atusaidie πŸ™πŸΏ
 
Back
Top Bottom