Mlioanzisha mahusiano humu ndani kwa mbwembwe na baadaye mkaachana, mko wapi?

.......sisi watu wa humu sio watu spesho na timilifu, ni binadamu wa kawaida kama wengine huko mitaani, tunapitia changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii na kimahusiano au hata kiafya kama watu wengine.......
.......sioni kama busara sana kuwananga na kuwanyanyasa watu ktk mitandao as if kuna mambo walitukosea au hata kama tuliwataka wakatukataa, mbaya zaidi tunawataja na I'd zao, tujifunze kujadili vitu vyenye tija kuliko kujadili personal issues za watu, hawa memba tunaowataja hapa wana michango mikubwa sana kuifanya jf kuwa sehemu nzuri ya kupata maarifa na kupumzisha akili, tuwaheshimu basi hata kwa hayo waliotupatia, tusiwafanye wakimbie mahali hapa, please guys!!!........
........licha ya kuwa mtandao wa jf unaaminika kujaa watu waelewa na wasomi wa viwango tofauti, lakini unaweza kuwa mtandao wa kwanza unaotumika kunyanyasa watu wa makundi mbalimbali i.e single moms, waliochelewa kuolewa, wahitaji, walimu na watu waliofanikiwa kifedha(kuwasema ni wauza ngada au mashoga hasa hawa celebrates).......
.........nb:hakuna anaependa kuvunja mahusiano au kuachwa, sio sifa kuachana lakini pia sio crime au dhambi, wanaumia kama watu wengine, tuwe faraja kwao, tusiwe sehemu ya maumivu kwao, hongera wote mliodumu ktk mahusiano na ustawi mzuri wa ndoa zenu.......
 
Back
Top Bottom