Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.
Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.
Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.
Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
- Tunachokijua
- Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Plasmodium ambayo husambazwa na mbu jike aina ya anopheles.
Dalili za awali za ugonjwa huu huanza kuonekana takriban siku 10-15 tangu mhusika ang’atwe na mbu mwenye vimelea na huhusisha kuongezeka kwa joto la mwili, uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya kichwa, kuharisha na kutapika pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.
Matibabu yake
Msingi wa matibabu ya ugonjwa huu umekuwa unabadilika ili kuongeza ufanisi kwenye kudhibiti vimelea vyake, pamoja na kupunguza maudhi ya dawa yanayoweza kujitokeza kwa mgonjwa.
Mwongozo wa matibabu unaopaswa kutumiwa na watoa huduma wote wa afya Tanzania Bara uliotolewa na Serikali kupitia Wizara ya afya mwaka 2021 yaani “STANDARD TREATMENT GUIDELINES AND NATIONAL ESSENTIAL MEDICINES LIST FOR TANZANIA MAINLAND” unaelekeza matumizi ya Artemether-Lumefantrine (ALU) kama dawa chaguo la kwanza kwenye kutibu ugonjwa wa Malaria ambapo Dihydroartemisinin-Piperaquine inaweza kutumika kama mbadala.
Ikiwa matumizi ya sindano yatahitajika, Artesunate au Artemether zinaweza kutumika.
Madai ya Baadhi ya Dawa Kusababisha Mzio
Madai yanayojadiliwa hapa yanahusisha dawa inayoitwa Ekelfin, jina la kibiashara linalotumiwa na kampuni ya ELYS CHEMICAL INDUSTRIES LTD. Dawa hii huwa na mjumuiko wa Sulfadoxine na pyrimethamine, baadhi hupenda kuita SP.
JamiiForums imebaini kuwa, Kwa asili yake, Sulfadoxine ni kemikali yenye asili ya sulfa ambayo kwa baadhi ya watu husababisha allergy (mzio) kubwa au ndogo.
Inaweza kusababisha vidonda midomoni na kwenye maeneo yenye ngozi laini mwilini hasa midomo na sehemu za siri, kupauka, mabaka na kutokwa na malengelenge kwenye ngozi, kupungua kwa mkojo, kusikia milio kwenye masikio pamoja na umanjano hivyo madai ya mdau yapo sahihi.
Mfano wa majina mengine ya kibiashara ya dawa hii ni Malafin, sulphadar na Fansidar. Zote ni dawa zinazoweza kuleta madhara yanayofanana kwa mhusika.
Ili kuzuia madhara haya, wataalamu huuliza kwanza kama mgonjwa aliwahi kupata mzio wa aina yoyote ya dawa pamoja na historia yake ya awali.
Aidha, Artemether-Lumefantrine (ALU) ni dawa inayofaa zaidi kwa mtu mwenye mzio wa aina hii.