KWELI Baadhi ya Dawa za kutibu Malaria zinaweza kusababisha mzio mwilini, ikiwemo Kuchubuka Uume na Midomo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

IMG_9090.jpeg

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
 
Tunachokijua
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Plasmodium ambayo husambazwa na mbu jike aina ya anopheles.

Dalili za awali za ugonjwa huu huanza kuonekana takriban siku 10-15 tangu mhusika ang’atwe na mbu mwenye vimelea na huhusisha kuongezeka kwa joto la mwili, uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya kichwa, kuharisha na kutapika pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

Matibabu yake
Msingi wa matibabu ya ugonjwa huu umekuwa unabadilika ili kuongeza ufanisi kwenye kudhibiti vimelea vyake, pamoja na kupunguza maudhi ya dawa yanayoweza kujitokeza kwa mgonjwa.

Mwongozo wa matibabu unaopaswa kutumiwa na watoa huduma wote wa afya Tanzania Bara uliotolewa na Serikali kupitia Wizara ya afya mwaka 2021 yaani “STANDARD TREATMENT GUIDELINES AND NATIONAL ESSENTIAL MEDICINES LIST FOR TANZANIA MAINLAND” unaelekeza matumizi ya Artemether-Lumefantrine (ALU) kama dawa chaguo la kwanza kwenye kutibu ugonjwa wa Malaria ambapo Dihydroartemisinin-Piperaquine inaweza kutumika kama mbadala.

Ikiwa matumizi ya sindano yatahitajika, Artesunate au Artemether zinaweza kutumika.

Madai ya Baadhi ya Dawa Kusababisha Mzio
Madai yanayojadiliwa hapa yanahusisha dawa inayoitwa Ekelfin, jina la kibiashara linalotumiwa na kampuni ya ELYS CHEMICAL INDUSTRIES LTD. Dawa hii huwa na mjumuiko wa Sulfadoxine na pyrimethamine, baadhi hupenda kuita SP.

JamiiForums imebaini kuwa, Kwa asili yake, Sulfadoxine ni kemikali yenye asili ya sulfa ambayo kwa baadhi ya watu husababisha allergy (mzio) kubwa au ndogo.

Inaweza kusababisha vidonda midomoni na kwenye maeneo yenye ngozi laini mwilini hasa midomo na sehemu za siri, kupauka, mabaka na kutokwa na malengelenge kwenye ngozi, kupungua kwa mkojo, kusikia milio kwenye masikio pamoja na umanjano hivyo madai ya mdau yapo sahihi.

Mfano wa majina mengine ya kibiashara ya dawa hii ni Malafin, sulphadar na Fansidar. Zote ni dawa zinazoweza kuleta madhara yanayofanana kwa mhusika.

Ili kuzuia madhara haya, wataalamu huuliza kwanza kama mgonjwa aliwahi kupata mzio wa aina yoyote ya dawa pamoja na historia yake ya awali.

Aidha, Artemether-Lumefantrine (ALU) ni dawa inayofaa zaidi kwa mtu mwenye mzio wa aina hii.
Mdau wa JamiiForums.com analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Nakubaliana na hili na huwa linanitokea kila nikitumia dawa hii.
 
Nakubaliana na hili na huwa linanitokea kila nikitumia dawa hii.
Mimi pia ni mhanga wa hizi dawa unachubuka sehemu za siri na muwasho mkononi unatoka kama vishilingi
Mie nikitumia malafin tu hali tete na mwanzo ilikuwa ndo dawa yangu hiyo.
 
Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari taj

Mdau wa JamiiForums.com analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Mimi naona cha muhimu ni mtu kuangalia aina ya hizo dawa ambazo zinakufaa. Dawa siku zote huwa zina side effect ambayo huwezi epuka.
 
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
kila sawa ina side effect kuna mtu alikunywa dawa tatu alivimba macho
 
Kuna uhusiano wowote kati ya dawa za malaria na pumu ya ngozi?
Mwanangu ninapomtibu malaria hutokea vipele {harara mwili mzima} kuna mtu kaniambia mtoto atakuwa na pumu ya ngozi, je ukweli ni nini? na je tiba au msaada wake ni nini? Naomba msaada nimsaidie huyu kiumbe

Sent from my 2107113SG using JamiiForums mobile app
 
Ujana kumbe mfupi sana ‍🦯
Si muda mrefu nilikuaga na miaka 25 sasaiv miaka 35 duuh .
Ndo basi Tena mie weeh🧎
 
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Kuna fomu maalumu ambazo zinatolewa nadhani ni TMDA kama sijasahau ambazo hutumika kuripoti maudhi ya Dawa
 
Asishangae inatakiwa ajue tu kua ana allergy na mchanganyiko huo wa dawa na atumie aina ingine ya dawa ili kupatwa na tatzo hilo.Na asiishangae gov maana sio kazi ya gov kutangaza mzio wa kila mtu kwenye dawa fulani.
 
Hawa pharmacist wa mtaani wanahitaji kuwapa watu dawa kwa kuwauliza na sio Kama wafanyavyo hivi.
 
Kuna ulazima pia wa kujenga Mazowea ya kujua ya kupima kujua kama una mzigo wowote ktk miili yeti sababu muda mwengine kinachokudhuru wewe mwengine hakina shida kwake.

Binafsi niliteseka sana niliumwa kuanzia kuambiwa nina pumu ya ngozi na dalili za saratani ya ngozi kumbe ni mzio wa viungo viwili vya dawa Aspirin na Sulfur toka nimetambua hilo siteseki nikiumwa nikifika zahanati tu najieleza ili nipewe dawa mbadala.

Kuna haja ya kubadilisha mfumo wa maisha kwa kukagua afya zetu na jamii zetu angalau kwa mwaka mara moja au mbili.
 
Dawa nyingi za malaria zinakua na side effect ya skin itching (kuwashwa kwa ngozi), ambayo ni kawaida lakini madhara zaidi hutokea kwa mtu ambaye ana mzio( allergy) ya dawa zinazobeba " sulfonamides".
Habari yako bro, unaufahamu ugonjwa wa korodan kuchoma kama vl kuna m2 anakuchanja na kiwemb na inatokea napotembea nijuz kama wafaham
 
Habari yako bro, unaufahamu ugonjwa wa korodan kuchoma kama vl kuna m2 anakuchanja na kiwemb na inatokea napotembea nijuz kama wafaham
...hizi zinaleta allergic reaction
Nakubaliana na hili na huwa linanitokea kila nikitumia dawa hii.
Mimi pia ni mhanga wa hizi dawa unachubuka sehemu za siri na muwasho mkononi unatoka kama vishilingi
Mie nikitumia malafin tu hali tete na mwanzo ilikuwa ndo dawa yangu hiyo.
Iuokyoupyluiijyi
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom