KWELI Baadhi ya Dawa za kutibu Malaria zinaweza kusababisha mzio mwilini, ikiwemo Kuchubuka Uume na Midomo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.

IMG_9090.jpeg

Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
 
Tunachokijua
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Plasmodium ambayo husambazwa na mbu jike aina ya anopheles.

Dalili za awali za ugonjwa huu huanza kuonekana takriban siku 10-15 tangu mhusika ang’atwe na mbu mwenye vimelea na huhusisha kuongezeka kwa joto la mwili, uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya kichwa, kuharisha na kutapika pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

Matibabu yake
Msingi wa matibabu ya ugonjwa huu umekuwa unabadilika ili kuongeza ufanisi kwenye kudhibiti vimelea vyake, pamoja na kupunguza maudhi ya dawa yanayoweza kujitokeza kwa mgonjwa.

Mwongozo wa matibabu unaopaswa kutumiwa na watoa huduma wote wa afya Tanzania Bara uliotolewa na Serikali kupitia Wizara ya afya mwaka 2021 yaani “STANDARD TREATMENT GUIDELINES AND NATIONAL ESSENTIAL MEDICINES LIST FOR TANZANIA MAINLAND” unaelekeza matumizi ya Artemether-Lumefantrine (ALU) kama dawa chaguo la kwanza kwenye kutibu ugonjwa wa Malaria ambapo Dihydroartemisinin-Piperaquine inaweza kutumika kama mbadala.

Ikiwa matumizi ya sindano yatahitajika, Artesunate au Artemether zinaweza kutumika.

Madai ya Baadhi ya Dawa Kusababisha Mzio
Madai yanayojadiliwa hapa yanahusisha dawa inayoitwa Ekelfin, jina la kibiashara linalotumiwa na kampuni ya ELYS CHEMICAL INDUSTRIES LTD. Dawa hii huwa na mjumuiko wa Sulfadoxine na pyrimethamine, baadhi hupenda kuita SP.

JamiiForums imebaini kuwa, Kwa asili yake, Sulfadoxine ni kemikali yenye asili ya sulfa ambayo kwa baadhi ya watu husababisha allergy (mzio) kubwa au ndogo.

Inaweza kusababisha vidonda midomoni na kwenye maeneo yenye ngozi laini mwilini hasa midomo na sehemu za siri, kupauka, mabaka na kutokwa na malengelenge kwenye ngozi, kupungua kwa mkojo, kusikia milio kwenye masikio pamoja na umanjano hivyo madai ya mdau yapo sahihi.

Mfano wa majina mengine ya kibiashara ya dawa hii ni Malafin, sulphadar na Fansidar. Zote ni dawa zinazoweza kuleta madhara yanayofanana kwa mhusika.

Ili kuzuia madhara haya, wataalamu huuliza kwanza kama mgonjwa aliwahi kupata mzio wa aina yoyote ya dawa pamoja na historia yake ya awali.

Aidha, Artemether-Lumefantrine (ALU) ni dawa inayofaa zaidi kwa mtu mwenye mzio wa aina hii.
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.


Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Asanteeee
 
Tatizo kama hili liliwahi kunipata,,Baadhi ya Dawa Zina kemikali inaitwa #Sulphur...watu wengi wana mzio nayo ukigundua una mzio na hii kemikali waambie madaktari kuwa una mzio utapewa dawa stahiki
 
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.


Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.

Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Naprescribe hiyo dawa na kwakweli sio kila mtu anaweza pata matatizo hayo inategemea na mapokeo ya seli nyeupe za mwili.

Mfano mzuli ni wamama wajawazito kila wanapokuja kliniki wanapata dawa hiyo SULPHADOXINE +PYRIMETHAMINE kama kinga ya malaria na ukweli ni kua sijawahi pokea malalamiko.

Ila ukweli ni kua kuna baadhi ya watu wapo allergic na madawa yenye Sulphur hivyo sema kwa daktari wako kila unapokua umeenda kimatibabu.
 
Binafsi dawa zenye sulpher huwa nikitumia huwa zinaniletea vidonda....

Maranyingi hapo nyuma nimekuwa nikitumia SP's drugs sana sana Malafini napo patwa na malaria.....na kila nikitumia natokewa na kidonda kwenye lips za mdomo

Hivyo kwa upande wa malaria napendelea kutumia Artimether Lumefantrine (MSETO/ALU)
 
Hili lilinikuta mwaka 2022 mwezi wa tano nikimeza hizo Ekelfin, baada ya siku kama mbili hivi nikasikia kubabuka sehemu za juu na chini mdomoni na uume nikawa nasikia kama umeungua hivi na mwili kuwashwa. Niliteseka mnooooo! Hiyo dawa na mimi tena ni basi
 
Ni kweli anaweza kua na allergy na Moja ya ingredient ya hio dawa ambayo probably ni sulphur. Elekelfin ni brand name ya dawa aina ya sp sulphadoxine+ pyrimethamine ni kundi la dawa zinazokinga maralia
 
jamani tuache kununua dawa kiholela twendeni vituo sahihi vya afya tukapate vipimo sahihi, ushauri na tiba bora.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom