Search results

  1. S

    Kutegemea Katiba Mpya bora chini ya CCM iliyoko madarakani ni sawa na kusema Yanga wasimamie kutungwa sheria mpya za Ligi Kuu baada ya kuwa mabingwa!

    Tusijidanganye. CCM hawana nia ya kuona Tanzania inapata Katiba mpya inayotoa fursa bora katika utawala wa sheria nchini na ushindani sawa wa vyama vya siasa. Hilo halitakuja kutokea hata siku moja. Kutegemea hilo litatokea ni sawa tu na mashabiki na timu zao za Simba, Azam, Kagera, Mtibwa nk...
  2. S

    Donald Trump apatikana na hatia ya makosa yote 34 katika kesi ya kughushi nyaraka na kutaka kuficha kuhusu hela alizomlipa pornstar ili akae kimya

    Katika kesi iliyokuwa ikimkabili Raisi wa zamani wa Marekani Donald Trump iliyohusu kutumia fedha isivyo halali kumlipa mwanamke aliyelala naye, wazee wa mahakama (jury) 12 wamefikia uamuzi kwamba Donald Trump ana hatia na hivyo lililobaki na jaji kutoa hukumu dhidi ya Raisi huyu wa zamani wa...
  3. S

    Wizi na ufisadi wa fedha za serikali uliokithiri katika awamu hii, suluhisho haliko ndani ya CCM wala upinzani kuwa mbadala wa CCM

    Tumefikia mahali ambapo hali ya wizi na ufisadi wa fedha za serikali inatisha. Si Tamisemi tu, bali hata vyombo vya usalama na taasisi za serikali ugonjwa ni huo huo. Udanganyifu katika mifumo ya malipo imekuwa ndio habari ya mjini, kuanzia tozo za kupaki magari, fine za trafiki, miamara ya...
  4. S

    RC Chalamila maintanance ya barabara za Dar es Salaam imemshinda kabisa, labda sababu ni kuweka nguvu kwenye mambo yasiyo muhimu kama ukahaba!

    Kama ingekuwa maintenance ya barabara za Dar es Salaam ni kigezo cha kupima uwezo wa RC Chalamila kuongoza Dar es Salaam, basi anapaswa aondolewe mara moja. Hili ni eneo ambalo anafeli kwa kiwango cha juu sana. Na kinachoudhi ni kwamba inakuwa kama vile yeye haoni kabisa kwamba barabara za Dar...
  5. S

    Mtoto wa miaka 8 aliepotea Kibaha na kukutwa ametupwa shimoni na amekufa: Ni sahihi Polisi kusema usubiri masaa 24 kabla ya kuripoti kupotea mtoto?

    Kuna tukio la hivi karibuni la Kibaha, ambapo wazazi wa mtoto wa kike wa miaka 8, Angel, mwanafunzi wa darasa la 2, walienda Polisi kuripoti kupotelewa mtoto, wakaambiwa Polisi hawawezi kupokea taarifa yao ya kupotelewa mtoto na inabidi wasubiri kwanza masaa 24 ndio wakaripoti kupotelewa mtoto...
  6. S

    Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

    Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua. Ni kiongozi mjinga tu asieweza kuona kwamba jinsi haya...
  7. S

    Kauli ya Lissu ya Rais Mzanzibar ni matokeo ya kufumba masikio Tanganyika kuwa na Serikali yake na viongozi wake watakaoamua mambo yao, asilaumiwe!

    Kwanza niombe moderators muiache hii thread ijitegemee, inaenda mbali zaidi ya kauli ya Lissu. Kama una akili timamu na za kutosha, utakuwa umegundua kwamba suala la kusema kero za muungano zinatatuliwa limekuwa ni suala la kuzidi kuipa Zanzibar mamlaka yake kama nchi kamili na kuiondoa kwenye...
  8. S

    Hivi inawezekana kwa Waislamu kuwa na hesabu hususa ya siku za kufunga badala ya kutegemea kuonekana au kutoonekana kwa mwezi?

    Ni kitu ambacho siku zote sijakielewa, na labda ndugu zangu Waislamu watanisaidia hapa. Kufunga najua ni suala la kujipa muda wa kutafakari matendo na maisha yako na kuboresha uhusiano wako na Mwenyezi Mungu. Sasa sielewi kwa nini jambo hili lihusianishwe na kuonekana au kutoonekana kwa mwezi...
  9. S

    Nataka kufuga bundi, lakini jamii hainielewi

    Nataka kufuga bundi kuzuia uharibifu wa panya wa mazao shambani kwangu, ila sasa hii jamii ninayoishi nayo wakiona nakusanya bundi hawanielewi, wanadhani mie mchawi. Halafu mie nawaona bundi wako wa-cute! Nifanyeje? Wasije wakanichoma moto ndani ya nyumba yangu.
  10. S

    Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

    Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli...
  11. S

    Tunaelewa kwanini Mwigulu ana hasira na Magufuli hadi leo, na hadi sasa anatoa kauli hasi dhidi yake, na kumwaga maua kwa wingi!

    Tuongee peupe leo, uwazi na ukweli. Mtu yeyote makini atagundua kwamba karibu kila kauli anazotoa Mwigulu zinalenga kutaka kuonyesha Raisi Samia ni bora sana kuliko alivyokuwa Raisi Magufuli. Tunakiri kwamba kuna baadhi ya mambo Raisi Samia ni bora kuliko alivyokuwa Raisi Magufuli, lakini tuseme...
  12. S

    Serikali itufafanulie "hatua za mwisho" maana yake nini badala ya kutufanya kama watoto wadogo wa kudanganywa kwa majibu ya rejareja

    Mwaka jana, June 2023, wakati waziri wa mambo ya nje akiwa Dr Tax, serikali ilitoa hili tamko pale Bungeni Leo April 2024, serikali imetoa tena tamko hilo hilo pale pale Bungeni mbunge wa viti maalumu Suma Fyandomo alipouliza swali kuhusu uraia pacha. Sasa nakumbuka tumekuwa na matamko kama...
  13. S

    Baadhi ya Polisi nchini ni waongo na wauaji

    Hii sio taarifa ya tukio bali ni tathmini ya utendaji wa jeshi letu la Polisi katika kukiuka haki za wananchi wa Tanzania, binadamu walioapa kuwalinda. Hivi karibuni huko Kibaha kumetokea tukio la mtu kuuwawa kwa risasi, na mwili wake "kuokotwa" na wananchi. Ndugu wa mtu alieuwawa wanasema mtu...
  14. S

    Ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa endapo Rais atavunja Katiba kwa kukusudia au kutokukusudia?

    Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume...
  15. S

    Kwa kauli ya DC Mbeya, maandamano ya CHADEMA yanafanyika sababu Rais Samia ameruhusu na sio kwa sababu ya Katiba

    Mara nyingine nikiwaza mambo yanavyofanyika hapa Tanzaniia, naona kama tumekuwa jumuiya fulani katika uwanja wa fujo. Tunaishi kwa matamko ya Raisi, mawaziri, wakuu wa Polisi, wakuu wa mikoa na mara nyingine katibu mwenezi wa CCM! Hivi hakuna watu wenye akili nchini, na hasa viongozi, wakaona...
  16. S

    Tanesco Temeke: Umeme upo wa kutosha, shida miundombinu iliyopo haiwezi kutawanya umeme kwa wakati mmoja

    Kama ulikuwa unafikiria kwamba baada ya umeme wa bwawa na Nyerere kuanza kupatikana basi matatizo ya mgawo wa umeme yatakuwa yamekwisha, basi sasa ni wakati wa kubadili mawazo yako. Tanesco wanasema kwamba, mgawo wa umeme Tanzania kimsingi hautokani na ukosefu wa umeme wa kutosha, bali ni kwa...
  17. S

    Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

    Juzi hapa niliweka thread JF iliyosema wengi wa matajiri wa Tanzania ni wanasiasa na sio wafanya biashara, nikiwa na maana kwamba utajiri wao haujatokana na kufanya biashara bali umetokana na nafasi zao za kisiasa au uongozi serikalini kujitajirisha - urefu wa kamba zao. Kwa wengi wetu huo ni...
  18. S

    Nionavyo mimi: Changamoto za migongano anazokabilili Rais Samia ndani ya CCM ni kubwa kuliko anazokabili toka vyama vya upinzani

    Watu wengi wakisikia maneno ya kina Tundu Lissu , Mbowe na kadhalika, yakionyesha kutoridhishwa na raisi Samia katika majukumu yake kama raisi wa Tanzania, wanapata hisia kwamba watu wa upinzani ndio wanaomnyima raisi Samia usingizi wa usiku. Ukiwaza hivyo uko nje kabisa ya mstari. Changamoto...
  19. S

    Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

    Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa. Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo...
  20. S

    Serikali, CCM na Polisi wanapaswa kujiuliza kwa nini wananchi wakiona askari polisi anashambuliwa hawatoi msaada?

    Juzi hapa kulikuwa na tukia la askari Polisi mkuu wa kituo cha polisi Mwanakwerekwe, Zanzibar, akishambuliwa hadharani, na wananchi wakishangilia japo waliona askari alikuwa amezidiwa (angalia picha hapa chini). Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib, amewalalamikia wananchi kwamba...
Back
Top Bottom