Mtoto wa miaka 8 aliepotea Kibaha na kukutwa ametupwa shimoni na amekufa: Ni sahihi Polisi kusema usubiri masaa 24 kabla ya kuripoti kupotea mtoto?

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,208
19,001
Kuna tukio la hivi karibuni la Kibaha, ambapo wazazi wa mtoto wa kike wa miaka 8, Angel, mwanafunzi wa darasa la 2, walienda Polisi kuripoti kupotelewa mtoto, wakaambiwa Polisi hawawezi kupokea taarifa yao ya kupotelewa mtoto na inabidi wasubiri kwanza masaa 24 ndio wakaripoti kupotelewa mtoto.

Kesho yake huyu mtoto alipatikana akiwa ametupwa kwenye shimo la choo na akiwa amekufa. Ninashawishika kwamba kama Polisi wangeanza kufanyia kazi taarifa za kupotea mtoto pale zilipotolewa mara ya kwanza, huenda mtoto angepatikana akiwa hai.

Katika nchi nyingi, kama sio zote, suala la kusubiri masaa 24 kabla ya kutoa taarifa ya kupotea mtu, linahusu watu wazima, sio mtoto. Sasa najiuliza, hapa Tanzania tuna utaratibu tofauti wa kuripoti kupotelewa mtoto na polisi kuipokea hiyo taarifa rasmi, kwamba hawawezi kuifanyia kazi kabla masaa 24 hayajapita?

Kama ni kweli kwamba uratatibu wa Polisi hapa nchini kuhusu mtoto anaeripotiwa kupotea unahitaji yapite masaa 24, basi natoa wito kwa Raisi Samia na Waziri wa Mambo ya Ndani, kwamba itolewe amri ya DHARULA MARA MOJA, utaratibu huu ubadilishwe sasa hivi. Mtoto chini ya miaka 16 (au hata 18) akiripotiwa kupotea kituo cha polisi, Polisi wanatakiwa wapokee hiyo taarifa rasmi na kuanza kuifanyia kazi mara moja. Masaa 24 iwe ni kwa mtu mzima tu.

Na kama Polisi Kibaha waliwapotosha hawa wazazi wa huyu mtoto kuhusu kusubiri masaa 24, basi hatua kali za kisheria zichukiliwe dhidi ya Polisi wote waliohusika na wanaowajibika na hao waliohusika.

Nyumbani kwako kuna mtoto mdogo wa chini ya miaka 10? Sasa fumba macho, fikiria kwamba amepotea, hujui alipo, hujui kama amekula au la, hujui kama analia kwa uoga hapo alipo au la, hujui kama ana maumivu, analia kukuita umsaidie, hujui kama kuna mtu anamtesa, anamuumiza, anamfanyia vitendo vibaya kama ubakaji au ulawiti, anamchapa fimbo au ngumi kumlazimisha. Damu zinamtiririka sehemu sehemu, na amevimba viungo kadhaa vya mwili. Halafu unaenda polisi kuomba msaada waanze kuchunguza yuko wapi, alionekana na nani mara ya mwisho, wanakuambia subiri masaa 24 yapite!

Habari kamili iko Mwananchi
 
Polisi ni chombo Cha Dola,Dola ni neno la kiarabu (dawla) lenye maana ya serikali,polisi haipo kwa ajili ya usalama wa raia na Mali zao Kama wanavyodai,kwa raia huku,utaibiwa ndipo waje kusaka wezi,utauawa ndipo waanze kusaka wauaji,hawakulindi,zaidi hufanya patrol kupitia makusanyo kwenye biashara Fulani na kukamata watu watakaotoka kwa pesa baadae baada ya kuwaweka mahabusu,polisi ni duka la haki na malango yao yasiyofungwa
 
Hii nayo mpya, na labda ndivyo Polisi wetu wana mtazamo huu.

Lakini jambo la msingi hapa ninalosema ni kwamba kama kuna sheria au utaratibu wa kusema mtoto mdogo akipotea lazima usubiri masaa 24 kuripoti kuwa amepotea, haufai na unapaswa kuondolewa haraka.

Nimeongeza hivi hapo juu;

Nyumbani kwako kuna mtoto mdogo wa chini ya miaka 10? Sasa fumba macho, fikiria kwamba amepotea, hujui alipo, hujui kama amekula au la, hujui kama analia kwa uoga hapo alipo au la, hujui kama ana maumivu, analia kukuita umsaidie, hujui kama kuna mtu anamtesa, anamuumiza, anamfanyia vitendo vibaya kama ubakaji au ulawiti, anamchapa fimbo au ngumi kumlazimisha. Damu zinamtiririka sehemu sehemu, na amevimba viungo kadhaa vya mwili. Halafu unaenda polisi kuomba msaada waanze kuchunguza yuko wapi, wachunguze alionekana na nani mara ya mwisho, wanakuambia subiri masaa 24 yapite!
 
Kiuhalisia polisi walipaswa kupokea report ya ya mtoto kupotea, though wasingejua pia wapi kwa kuanzia zaidi ya kuambatana na wazazi kutafuta maeneo anayopenda kwenda, kwa kesi kama hiyo ya mtoto kukutwa kwenye shimo la Choo ambacho hakijaanza kutumika unadhani polisi wetu wangetumia technology gani kujua alipo mtoto, zama hizi ni za kufunga watoto GPS tracker, mnunulie mtoto GPS watch n.k sababu hata case za watoto kuibiwa ni nyingi na huenda zika zidi kuelekea 2025 .
 
Mkuu umetoa mawazo mazuri sana, kuna kipindi niliwai gusia kuhusu hicho kitu mtu kupotea na taarifa polisi lazima ziwe zimepita saa 24.

Huo ni utaratibu mbovu sababu zikipita hizo saa24 ndipo wigo unazidi kuongezeka wa kutompata yule aliepotea hasa kwa watoto na wale watu wenye matatizo ya akili.

Hebu fikiria mtoto ameibiwa au kutekwa na mtekaji anasafiri na huyo mtoto je ndani ya saa 24 atakua ametembea umbali gani, hapo kimasihara kwa TZ mtu ndani ya saa24 anaweza kutoka kusini let's say Mtwara hadi Singida anafika sasa hapo wigo wa kutompata unakua ni mkubwa zaidi.

Kwahiyo polisi wangepitia tena hiyo sheria kandamizi na ya hovyo ambayo inaleta maumivu kwa watu hasa wazazi maana watu wanaishi kwa woga sana siku hizi hakuna kuaminiana.
 
Kingine unatakiwa uelewe, suala la mtu kupotea na kutafutwa kama wewe muhusika mmeshindwa kumpata huyo mpotevu basi polisi hataweza pia. Wampate Kwa njia gani Sasa? Wataota? Hapana.
Suala la masaa 24 ni kutoa muda watu waendelee kumtafuta muhusika wakati huo tayar taarifa ya mdomo inakuwa imesharipotiwa kituon ikisubiri 24hrs iwekwe kwenye maandishi, na pia Ile taarifa inakulinda na wewe mwenyewe Kwa Leo na kesho endapo mambo yataenda ndivyo sivyo. Hutawajibika kujibu
 
Kiuhalisia polisi walipaswa kupokea report ya ya mtoto kupotea, though wasingejua pia wapi kwa kuanzia zaidi ya kuambatana na wazazi kutafuta maeneo anayopenda kwenda, kwa kesi kama hiyo ya mtoto kukutwa kwenye shimo la Choo ambacho hakijaanza kutumika unadhani polisi wetu wangetumia technology gani kujua alipo mtoto, zama hizi ni za kufunga watoto GPS tracker, mnunulie mtoto GPS watch n.k sababu hata case za watoto kuibiwa ni nyingi na huenda zika zidi kuelekea 2025 .
Mkuu, polisi wana weredi kwenye kesi za kupotea. Huwa wanaanza kwa kuhoji watu, kwa mfano wakishajua aliondoka nyumbani saa ngapi, wanaanza kuangalia alipita wapi, nani alikuwepo njia aliyopita, nani alimwona nani akiongea naye. Watauliza watu wenye maduka jirani nk. Polisi kazi yao ni kufanya upepelezi sio kumtafuta mtoto.

Inaweza kutokea kabisa watu walimwona amesimamishwa na mwanaume fulani, wakaenda nyumbani kwa huyo mwanaume wakakuta yuko nae ndani. Unaposubiri masaa 24 unampa mhalifu muda wa kutosha wa kumdhuru na kwenda kumtupa shimoni usiku wa manane wakati watu hawapo. Anaemdhuru mara nyingii atamuua na kumtupa usiku
 
Mkuu umetoa mawazo mazuri sana, kuna kipindi niliwai gusia kuhusu hicho kitu mtu kupotea na taarifa polisi lazima ziwe zimepita saa 24.

Huo ni utaratibu mbovu sababu zikipita hizo saa24 ndipo wigo unazidi kuongezeka wa kutompata yule aliepotea hasa kwa watoto na wale watu wenye matatizo ya akili.

Hebu fikiria mtoto ameibiwa au kutekwa na mtekaji anasafiri na huyo mtoto je ndani ya saa 24 atakua ametembea umbali gani, hapo kimasihara kwa TZ mtu ndani ya saa24 anaweza kutoka kusini let's say Mtwara hadi Singida anafika sasa hapo wigo wa kutompata unakua ni mkubwa zaidi.

Kwahiyo polisi wangepitia tena hiyo sheria kandamizi na ya hovyo ambayo inaleta maumivu kwa watu hasa wazazi maana watu wanaishi kwa woga sana siku hizi hakuna kuaminiana.
Utaratibu wa saa 24 kwa mtu mzima aliyepotea ni kawaida, lakini sio kwa mtoto!

Hata ukienda UK, USA, South Africa nk, masaa 24 ni kwa mtu mzima. Ukiripoti mtoto amepotea polisi wanaanza uchunguzi immediately. Ndicho ninachosema hapa, kwamba iwe hivyo kwa watoto.
 
Ni sahihi
 
Kingine unatakiwa uelewe, suala la mtu kupotea na kutafutwa kama wewe muhusika mmeshindwa kumpata huyo mpotevu basi polisi hataweza pia. Wampate Kwa njia gani Sasa? Wataota? Hapana.
Polisi huendi kuripoti ili wakutafutie mtu aliyepotea, bali wa assume kuna jinai na kuanza kupeleleza. Hiyo ndio lojiki ya kusubiri masaa 24, kwamba kwa mtu mzima anaweza akawa kaamua kwenda mahali bila kutoa taarifa.
 
Kuna mambo yanaumiza sana🥹....hakuna kitu kibaya kama expectations, unapohisi panaweza kuwa msaada na hapawi mwisho unapata machungu na maumivu kama haya
 
Hii nayo mpya, na labda ndivyo Polisi wetu wana mtazamo huu.

Lakini jambo la msingi hapa ninalosema ni kwamba kama kuna sheria au utaratibu wa kusema mtoto mdogo akipotea lazima usubiri masaa 24 kuripoti kuwa amepotea, haufai na unapaswa kuondolewa haraka.

Nimeongeza hivi hapo juu;

Nyumbani kwako kuna mtoto mdogo wa chini ya miaka 10? Sasa fumba macho, fikiria kwamba amepotea, hujui alipo, hujui kama amekula au la, hujui kama analia kwa uoga hapo alipo au la, hujui kama ana maumivu, analia kukuita umsaidie, hujui kama kuna mtu anamtesa, anamuumiza, anamfanyia vitendo vibaya kama ubakaji au ulawiti, anamchapa fimbo au ngumi kumlazimisha. Damu zinamtiririka sehemu sehemu, na amevimba viungo kadhaa vya mwili. Halafu unaenda polisi kuomba msaada waanze kuchunguza yuko wapi, wachunguze alionekana na nani mara ya mwisho, wanakuambia subiri masaa 24 yapite!
Ndiyo maana nikasema hawapo kwa ya usalama wa raia na Mali zao
 
Kuna mambo yanaumiza sana🥹....hakuna kitu kibaya kama expectations, unapohisi panaweza kuwa msaada na hapawi mwisho unapata machungu na maumivu kama haya
Na hakuna kitu kinaumiza kama upotelewe mtoto mdogo, usijue yuko wapi usiku ukipita
 
Back
Top Bottom