Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
822
1,345
Tarehe 13 April, Meya Mastaafu wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob alitoa taarifa ya kupotelewa na ndugu yake Bw. Robert Mushi maarufu kama Babu G, ambaye alipotea mapema mwezi April 2024. Inadaiwa alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa Polisi maeneo ya Kariakoo na baada ya hapo hakuonekana tena.

Ndugu walimtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio. Taarifa ilitolewa Polisi lakini walikanusha kumshikilia. Polisi walisema Robert hakuwa kwenye orodha ya wahalifu wanaotafutwa na Polisi. Na hata angekua mhalifu wangemkamata kwa utaratibu rasmi na kumpeleka mahakamani, sio kumvizia mtaani.

Baada ya hapo Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar likatoa taarifa ya kupotea kwa Robert na kwamba anatafutwa na ndugu zake. Hata hivyo ndugu walipofuatilia waliambiwa Jeshi la Polisi halijapata taarifa wala fununu zozote za alipo kijana wao, hivyo waendeele kuwa wavumilivu, wakati juhudi za kumtafuta zikiendelea.

Ndugu wamehangaika kumtafuta hospitali zote kubwa za jijini Dar, wakihisi huenda alipata ajali na akaumia kiasi cha kushindwa kujieleza hivyo akalazwa kama "unknown patient". Lakini jitihada hizo hazikuleta matokeo.

Leo wakaambiwa "nendeni hospitali ya Polisi Kilwa Road, ndugu yenu amefichwa mochwari pale". Wakaenda. Lahaula! Wakamkuta Robert akiwa kwenye jokofu la baridi. Hakuwa Robert tena bali ni mwili wake ukiwa na majeraha ya kipigo. Ni mauaji ya kikatili. Maskini Robert, hajawahi kuwa na ugomvi na mtu, kwanini atendewe haya?

Ndugu walipouliza wakaambiwa maiti ilipelekwa tarehe 10 April 2024. So ina siku 12 hapo Mochwari. Hii inamaanisha wakati Polisi wakidai kumtafuta Robert, alikua tayari Mochwari 😭.

Watumishi wa Mochwari wanasema maiti ililetwa na Askari. Walipoulizwa majina ya Askari na wanatoka kituo gani, wamewataka ndugu wa marehemu kuuliza uongozi wa hospitali. Viongozi wa hospitali walipoulizwa wakataka ndugu kuwasiliana na Msemaji wa jeshi la Polisi, kwani wao sio wasemaji.

Ni tukio la kinyama linalopaswa kulaaniwa na watu wote. R.I.P Babu G. Gone too soon. Damu yako iwe juu ya wote waliohusika.
IMG_1647.jpeg

Pia soma:

-
Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

- Utata sakata la ndugu wa Boniface Jacob: Kupotea mpaka kukutwa mochwari ya polisi, Amana wapigilia msumari!
 
Kuna sababu ya kuangalia upya sheria zetu, hawa polisi ni kama vile wamepewa mamlaka ya kuua raia kwa kisingizio cha kuitwa majambazi.

Sasa panatakiwa itungwe sheria itakayowataka wakuu wa hospitali zote nchini, iwe za wilaya au mikoa, wawe na mamlaka ya kuwahoji polisi pale wanapopelekewa marehemu kwenye hospitali zao kwa ajili ya kuwahifadhi, polisi wakishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, wakuu wa hospitali wawe na mamlaka ya kukataa kupokea marehemu hao.
 
kuna mwaka fulani wafanyabiashara walitandikwa risasi wakaibiwa fedha zao na madini na kadhalika wa kadha......harafu wakasema warikuwa ni majambazi.....sasa tukio lilitokea mbele ya ofisi ya mcha Mungu.....wakampanga yule mgha Mungu akatoe ushahidi wa uwongo......waapiii damu nziiitooo.....mcha Mungu akawaambia mie namuogopa Mungu........
 
Yule Mcha Mungu walimuua maana angeongea ukweli na mbaya zaidi nae alipewa kesi akauawa huko huko Jela...
 
Back
Top Bottom