Nimekoswakoswa mwezi huu hadi nimeapa sipandi tena boda... labda kuwe na sababu isiyozuilika.
 
Hivi mnafahamu wateja wa visungura ni kina nani?

Tujitahidi kutumia bajaj inapobidi ni salama.

Hawa bodaboda, unakuta amevaa ndala amenyanyuwa mguu mmoja, halafu amefungulia singeli volume mpaka mwisho na kwenye bomba la moshi sijui huwa wanaweka nini inaripuka kama bomu halafu bado mtu na akili zako unakubali kubebwa na kichaa kama huyo?
 
...Hivi Marekani, Uingereza, Ujerumani, Chena, Uholanzi, Dubai na Kwingine Kwa hivyo Kuna Boda Boda ? Mbona India Zimejaa ?...Tatizo ni Maendelea ??....
Kuna pikipiki hakuna bodaboda, tena China ndio inaongoza kwa hizi scooter ni usafiri muhimu lakini huwezi kusikia ajari.

South Africa pia pikipiki zipo lakini hakuna biashara ya bodaboda, pikipiki zinatumika kwa delivery kama vile DHL.
 
R.I.P. Kijana

Nani aliamua kwamba amekufa na polisi ndio wamchukue? Kwa khali yoyote si ilibidi apeleke hospitali kwanza au?

Hii issue natumaini Serikali utaangalia na kuelezea iweje, bila Daktari nani mwingine anapaswa kufanya kazi yao?
Mara nyingi polisi ndio huwa wanachukua miili kupeleka hospitali.
 
Polisi aisee! Eti mwenye taarifa tofauti apeleke kwa viongozi 😀😀😀 sidhani kama kuna atakaethubutu..
 
Ajali imetokea jana usiku mida ya saa 8 nadhani, boda boda wa mbezi wamefika eneo la tukio wanawapigia simu polisi kuwapa maelezo ya tukio ili wafike kwa wakati lakini ajabu jibu walilotoa askari linafikirisha sana..

Jibu walilotoa polisi walisema Gari yao haina MAFUTA ☹️,boda boda ilibidi waustili mwili vizuri ili hali ukiendelea kubakia eneo lile ukinyeshewa na mvua😢, mpaka ilipofika leo mida ya saa 4 asubuhi ndipo askari waliweza kufika eneo la tukio na kuutoa mwili wa marehemu kuupeleka hospitali.

TUKIO LA JANA NI UDHIHIRISHO TOSHA KUWA TUNA ASKARI WASIOKUWA NA WELEDI WOWOTE NA KAZI YAO 😒😠


"""Dah Zuchi, Mungu amlaze mahala pema peponi 🙏 nakumbuka wakati na Show ya #ThePlaylist ikabidi nitafute mtu mkali wa kufanya nae Professional Photoshoot nikakutana na Zuchi kipindi iyo anajitafuta na Studio yake Mwenge ndani ndani!

Akawasha midude hatari sana na kutokea apo ikawa kila kazi tunapiga nae na watu wakibao wakamuamini zaidi, njaa yake ya kutamani kupiga picha kali ikampeleka mpaka kwa Millard na kufanya kazi kupitia Ayotv, Pole sana @millardayo pole kwa familia, ndugu na jamaa 🙏 M/Mungu amlaze mahala pema peponi 🙏. """Lulyommy

View attachment 2974681

======

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU KIFO CHA ZUCHY - MPIGA PICHA WA AYOTV
———
Kuna taarifa yenye kichwa cha habari SHUHUDA inayosambazwa katika mitandao ikieleza

“Zuchy kapata ajali na boda hit and run mbele ya mataa ya masana kama 100 mita hivi toka saa nane usiku dereva wa boda akapelekwa hospital. Umoja wa bodaboda wamekaa na mwili barabarani pale wakiita Polisi kisingizio gari haina mafuta kweli. Pia tarifa hiyo inaeleza bodaboda walikaa na mwili hadi wakafunga barabara ili kushinikiza Polisi waitwe.”

Kwanza, Jeshi la Polisi linasema hili ni tukio la huzuni na la kusikitisha kwasababu tumempoteza Mtanzania mwenzetu katika ajali hiyo.

Pia lingependa kueleza kuwa, tukio hilo liliripotiwa saa kumi na dakika kumi na mbili alfajiri kuwa, kuna ajali imetokea eneo la Mbezi Makonde. Baada ya kupokelewa tarifa hiyo Maafisa na Askari waliokuwa kwenye majukumu katika mkesha wa Tamasha la Shangwe la Utawala lililokuwa linafanyika eneo la Tanganyika Packers waliondoka wakiwa na gari ya Polisi kuelekea eneo la tukio na kuchukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Mwananyamala kwa taratibu zingine za kisheria.

Askari waliofika eneo la tukio katika uchunguzi imebainika marehemu alipata ajali na pikipiki aliyokuwa amepanda yenye namba MC 436 CMU iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye
alipata majeraha na anaendelea na matibabu.

Hivyo, mara baada ya tarifa ya tukio hilo kutolewa na kupokelewa, Maafisa na Askari Polisi walifika kwenye tukio kwa wakati na kutekeleza yale yanayopaswa kutekelezwa kwenye eneo la ajali.

Tunawashukuru bodaboda wa eneo hilo wanaojali utu wa binadamu kwa kuzuia magari yasimkanyage marehemu.

Endapo kuna mwenye tarifa tofauti na si za uzushi/uwongo kama hizo zinazosambazwa azifikishe kwa viongozi ili zifanyiwe kazi na hatua zichukuliwe.
View attachment 2975042
Polisi wetu ukitaka wawahi sehemu waambie kuna mtu anamtukana mwanasiasa wa ccm. Wanaweza kuja hata na magari 10 kumkatamata mropokaji mmoja.

Kwenye issue za msingi tuwasamehe
 
Usha wai pata msiba wa aina izo??!

Unajua MTU akipata ajari kwanini huenda polisi kuchukua PF3??! Before hajapelekwa hospital??!

Eg. Mtu akichomwa kisu, kujinyonga, akinywa sumu, kujifungia nyumbani na kukutwa amevuja damu nyingi lazima walinzi wa amani wahusike in short

Uliza kingine
Huyo boda aliepelekwa hosp walifata huo utaratibu? Swali lang, km ajali wamepat pamoja inakuaje mmoja apelekwe hosp na mwingine asipelekwe?
 
Huyo boda aliepelekwa hosp walifata huo utaratibu? Swali lang, km ajali wamepat pamoja inakuaje mmoja apelekwe hosp na mwingine asipelekwe?
Unajua Nani mwenye mamlaka ya kuondoa maiti kwenye Eneo la tukio??


Ikijua hilo nadhani discussion itakua easy
 
Imeniuma Sana......

Mwanadamu ni kiumbe cha thamani sana.... kuanzia kikiwa hai na hata kikiwa hakina Uhai.....ndio maana kuna mazishi na makaburi.........

Yaani binadamu wanaacha maiti ya binadamu mwenzao inadharirika kwenye mvua kwa kauli ya polisi.......

Seriously mwanadamu anazungukwa na binadamu wenzake wanamtazama kama mzoga kwa masaaa zaidi ya sita.......

Watu wanashindwa kwenda kituo cha polisi na kujitolea hata elf 20 ya mafuta kuja kumchukua marehemu....???

Binadamu tumefikia kubaya Sana kwenye matendo ya kibinadamu na utu...............

Dah!!!!
Hili swala mm nasema hao watu pia waliokuwa hapo wajinga, ww binadam mwenzio unaona anahangaika hapo chini eti polisi mpaka aje kwani kusimamisha bajaji mkampeleka ama gari ikampeleka polisi ilishinidikana 😇😇.Mm ningekuwepo hapo ni bora nibaki sina hata mia lakini huyo jamaa afike sehemu salama mm silaumu polisi nalaumu hao waliofika hapo mapema.
 
Hili swala mm nasema hao watu pia waliokuwa hapo wajinga, ww binadam mwenzio unaona anahangaika hapo chini eti polisi mpaka aje kwani kusimamisha bajaji mkampeleka ama gari ikampeleka polisi ilishinidikana 😇😇.Mm ningekuwepo hapo ni bora nibaki sina hata mia lakini huyo jamaa afike sehemu salama mm silaumu polisi nalaumu hao waliofika hapo mapema.
Amefariki kifo cha kusikitisha sana japo vifo vyote vinasikitisha, ila masaa 6 mtu mnamuangalia tu hii ni mbaya zaidi, kweli siku ikifika imefika.
 
Poleni Kwa msiba huu wa Zuchi.

Kamanda akiwa katika majukumu ya kazi kapata ajali, kafariki kaacha watoto wawili, vipi kuhusu mirathi na stahiki nyingine za marehemu?

NB: Waajiri walazimishwe kuwakatia bima ya maisha wafanyakazi wao. Ona Sasa familia unaenda kuonja maisha magumu bila kutarajia.
Alishaacha kazi kwa millard siku nyingi na alikua kwenye biashara ya vipodozi.
 
Poleni Kwa msiba huu wa Zuchi.

Kamanda akiwa katika majukumu ya kazi kapata ajali, kafariki kaacha watoto wawili, vipi kuhusu mirathi na stahiki nyingine za marehemu?

NB: Waajiri walazimishwe kuwakatia bima ya maisha wafanyakazi wao. Ona Sasa familia unaenda kuonja maisha magumu bila kutarajia.
Alikuwa katika majukumu ya kazi ila ni kazi yake binafsi. Mauti yamemkuta akiwa sio muajiriwa bali mjasiliamali
 
Back
Top Bottom