Uratibu mbaya wa makadirio ya kodi ndiyo sababu kubwa ya ukwepaji kodi

Mkuu kuna Point fulani Unayo ila sasa Jinsi ulivoiweka Hata TRA hawataelewa.

Kwanza nianze na Utaratibu wa Makadirio,

Utaratibu wa makadirio una utaratibu wake na Kanuni zake.Kuna threshold za Kiwango cha Mapato na kiasi cha kodi unayopaswa kulipa.Sasa kwenye kuamua kiwango cha mapato TRA wanatumia vyanzo mbalimbali vya Taarifa zikiwamo Taarifa zinaotolewa na walipa kodi wenyewe,aina ya biashara,eneo la biashara na wakati mwingine hali ya kiuchumi.Sasa katika kufanya hivyo unaona kabisa kwamba Upo Utaratibu mzuri na Rahisi wa kuweza kusimamia Hiyo kodi ya Makadirio.

Sasa Tatizo ni nn?
Kwanza Tatizo ni Watanzania kutokuelewa kuhusu elimu ya kodi na sheria za kodi pamoja na haki zao kama walipa kodi na wajibu wao kama walipa kodi.

Suluhisho:
Suala kama hilo haliwezi kurekebishwa kwa sheria kali wali amri kali.Ni suala ambalo litachukua muda likihitaji wananchi kuendelea kujifunza na TRA nao kuendelea kujifunza na kuboresha Huduma zao.

Swala la Pili ni kuhusu hiyo kodi ya 18% ambayo inaitwa VAT,Kwanza tuelewe kwamba kodi ya VAT au kama inavyoitwa Sales TAX lengo lake kubwa ni kupanua wigo wa ulipaji wa kodi na kurahisisha ukusanyaji wa kodi.Kodi ya VAT inatozwa kwa assumtion kwamba yule mlaji wa Mwisho Ndio atakuwa mlipaji.Sasa Tafsiri ya Mlaji wa mwisho ni nani ndipo ambapo watu inabidi waelewe.Kwa mfano,Ukienda Sokoni ukanunua Mboga au uakaenda dukani kwa mangi ukanunua Bidhaa ambayo inatozwa VAT(Zinagatia kwamba sio kila bidhaa inatozwa VAT) basi ufahamu kwamba Wewe ambaye unaenda kutumia bidhaa hiyo Ndio Mlipaji.Hata kama utapewa Risit ambayo haina VAT bado wewe ni mlaji wa Mwisho.Yule Muuzaji wa Duka kwa sababu Yeye hajasajiliwa na VAT naye ni Mlaji wa Mwisho katika Mtazamo wa Kikodi mpaka atakapokuwa amesajiliwa kukusanya VAT.Kwa mtu ambaye amesajiliwa VAT yeye ataidai Mamlaka ya Mapato Ile Tofauti ya Kodi kati ya Makusanyo yake kutokana na Mauzo na Manunuzi ambapo iwapo Manunuzi yatazidi ila iwapo mauzo ndio yatazidi basi Ile Tofauti ya VAt atapaswa kulipa TRA.

Kwa wale ambao wanatuza kumbukumbu za Hesabu wao huwa wanao wajibu wa kuandaa HESABU za MWAKA kwa kupita Wahasibu na Wakaguzi pamoja na Wataalamu wa KODI ambao wamesajiliwa na TRA na NBAA ili waweze kupigiwa HESABU ya KODI Kikamilifu.

Baada ya kuchangia Mada hii kwa ujumla wake sasa nitoe Maoni ya Ujumla kuhusu Mfumo wetu wa KIKODI na namna ambavyo unaweza kurekebishwa:

  1. Swala la kwanza ni Viwango vyetu vya kodi,Kiwango cha Kodi ya Mapato kwa Tanzania ni 30% hiki ni kiwango kikubwa sana kwa aina ya uchumi tulio nao.Nasema nikiwango kikubwa kwa sababu kiwango hiki hakihamasishi ukuaji wa Biashara na kinaathiri sana gharam za uendeshaji hasa ukizingatia kwamba kuna gharama nyingi ambazo ni za kikodi ambazo kwa sasa zinaitwa TOZO ambazo zimeingizwa katika mfumo wetu wa Biashara.Ukitazama kwa ukaribu utaona kwamba Serikali ambayo haitoi vihamasishi vyovyote kwa wafanyabiashara inawatoza wafanyabiashara kodi ya 30% kisha kuna kuwa na gharama nyingine nyingi ambazo mfanyabiashara analipa kwa serikali hiyo hiyo.Ukija ukitazama unakuta Majukumu ya Compliance tu yanamgharimu mfanyabiashara zaidi ya 5% au zaidi ya mapato yake.Kitu serikali inaweza fanya ni Kupunguza Kiwango Cha Kodi ya Mapato kutoka 30% mpaka 15 au 20% na kisha kufanya VAT iwe Single DIGIT.Baada ya Hapo Biashara zote zilazimike kuwa na EFD regardless of SIZE na LOCATION na ihamasishe Digital Payment kwa kuondokana na TOZO za moja kwa moja katika Miamala ya Malipo kwa njia mtandao na zibaki standard charges.
  2. Swala la Pili ni Mifumo;Serikali iondokana kabisa na Suala la Mfanyakazi wa TRA kumfanyia Mjasiriamali Makadirio ya KODI.Kama kuna viwango elekezi viwekwe kwenye Mfumo na Kila Mtu awe na uwezo wa kutazama masuala yake ya kikodi na kuyasimamia Peke yake.TRA wafanye Monitoring ya Mifumo na iwapo kuna dalili z ukwepaji basi hapo ndipo waingilie kati.Unaporuhusu watu kukutana na kuanza kuneogotiate ndipo mazingira ya Rushwa yanapokuwepo.
All in all niwapongeze TRA kwa MFumo wao mpya ingawa bado una changamoto na unahitaji maboresho.Wajitahidi sana kuufanya huu mfumo uwe Intelligent System Yaani uwe na uwezo wa kujifunza kulingana na Data za walipa kodi wengine,location za walipa kodi wengine na taarifa nyingine za mlipa kodi.Teknoljia zipo na ninaamini kabisa kwamba wanaweza wakiwa na nia ya dhati.Yako Mengi sana ambayo ninayaona ila kwa leo tuanze na hayo na wengine nao wajdili

Mimi sikubaliaani kabisa na makadirio. Makadirio yalikuwa ni mihimu zamani kwasababu tulikuwa hatuna teknologia kwa sasa ni lazima utoe risiti na kutumia machine za kutoa risiti sasa kwa misingi hii makadirio ni ya nini? Hapo ndiyo kwenye tatizo. Kwanini nchi nyingine hawana makadirio?? Yaani huwezi kuweka machine za risiti halafu wewe uliyoweka usiziamini tena! na kuna risiti za makaratasi.

Kikubwa ni kufuata sheria na teknologia haya mambo ya makadirio rushwa haitaweza kuisha na serikali haitaweza kupata pesa halisi.
 
Kodi za mauzo hazitakiwi kukadiriwa kabisa. Kinachotakiwa na kutumia risiti na zitaonyesha kwa uwazi kabisa kodi ni kiasi gani. Utabiri ndiyo umetuletea matatizo yote
Mkuu,Kukadiria Maana yke ni nini?Kukadiria maana ni kufanya Makisia ambayo yanakaribia Uhalisia.Kwa nin serikali inataka Kukadiria ni kwa sababu hata yenyewe inapopanga Mapato na matumizi huwa ni Makadirio.So Makadirio kama Makadirio Sio tatizo,Tatizo ni namna na usimamizi wa makadirio na utaratibu wote unaohusisha Ukadiriaji wa Mapato kwa Malengo ya Kikodi.
 
Mimi sikubaliaani kabisa na makadirio. Makadirio yalikuwa ni mihimu zamani kwasababu tulikuwa hatuna teknologia kwa sasa ni lazima utoe risiti na kutumia machine za kutoa risiti sasa kwa misingi hii makadirio ni ya nini? Hapo ndiyo kwenye tatizo. Kwanini nchi nyingine hawana makadirio?? Yaani huwezi kuweka machine za risiti halafu wewe uliyoweka usiziamini tena! na kuna risiti za makaratasi.

Kikubwa ni kufuata sheria na teknologia haya mambo ya makadirio rushwa haitaweza kuisha na serikali haitaweza kupata pesa halisi.
Mkuu Makadirio hayana SHida na ni Utaratibu wa Kawaida kabisa ambazo sioni shida yake Kabisa?Swali langu ni Je wewe ni Mlipa KODI?Umewahi kufanya au kufanyiwa Makadirio?Tatizo lilikuwa ni nini hasa ili TRA Tanzania wakuelewe vizuri.
 
Mimi ni mtaalamu wa fedha na kwa mawazo yangu tatizo la kodi na TRA linaanza na uratatibu mbaya wa ukusanyaji wa kodi. Kuna kodi za aina mbili kubwa

1. Kodi za mauzo. Kwenye kodi hizi ambazo kwa ulewa wangu ni 18% mlipa kodi sio mfanyabiashara mfano mwenye duka. Mlipa kodi ni mnunuzi na mwenye biashara anatakiwa kuweka kodi pembeni na kuwapa TRA kisheria au kwa lugha ya kitaalamu hii kodi ni withholding tax. Sasa kuna watu wanafikiri mlipa kodi hii ni mwenye duka na imefika wakati mpaka wauzaji wanafikiri wenyewe ni walipa kodi hii kumbe sio hivyo mlipa kodi ni mnunuzi. Hivyo mfanyabiashara anauza kitu Tsh 1000 anatakiwa aweke kodi ya 18% na mnunuzi kulipa Tsh 1,180 na hiyo Tsh 180 hajalipa yeye ni mnunuzi na sio pesa yake.

2. Kodi ya mapato ni kodi za wafanyabiashara. Hizi ni kodi ambazo zinatoka kwenye faida ya biashara. Yaani baada ya mfanyabiashara kutoa matumizi yote na kubali na faidi kuna kodi anatakiwa kulipa ya mapato. Sina uhakika na % lakini inatokana na ukuwa na aina ya biashara. Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi.

Tatizo Tanzania ni hizo kodi za namba 1. Mtu wa TRA badala ya kukagua vitabu vya risiti anaenda kwa mfanyabiashara na makadirio. Sasa makadirio ya nini wakati sheria inataka kila mtu atoe risiti. Na kama kuna risiti basi kiasi cha kodi kinajulikana kuna haja gani tena kuwatuma wafanyakazi na makadirio. Sasa mfano risiti zinaonyesha kodi ambazo wateja wamelipa za kwenda serikalini ni Tsh 10M hawa mafisadi wa TRA wanakuja na makadirio ambayo hatujui yametoka wapi ya kodi ya Tsh 20M halafu wanamwambia mwenye biashara kwamba tupe Tsh 2M halafu lipa kodi Tsh 5M Hivyo serikali inapungukiwa Tsh 3M. Lakini kibaya zaidi mwizi huyo huyo bado analipwa pesa na mshahara wake kwenye hiyo Tsh 7M. Sasa kama nchi tutaendeleo vipi kwa utaratibu huu?

1. Serikali badilisheni utaratibu toeni ujinga wa makadirio
2. Wekeni sheria kali kwa wala rushwa
3. Wekeni sheria kali kwa wafanyabiashara watoa rushwa mfano toeni hongera kama mfanyabiashara akiweza kumleta mla rushwa
4. Wekeni utamaduni na onyo kwa utamaduni wa rushwa
1. Siyo wafanyabiashara wote wana mashine za risiti. Sheria inamtaka mtu ambaye mauzo ya ni 11m kwa mwaka kutoa risiti. Kama mauzo yako hayafiki 11m hulazimiki kutoa risiti. Kodi yako itakadiriwa kulingana na aina ya biashara unayofanya.

Hapa ndo tatizo linaanza. TRA wameweka viwango kwa aina ya biashara kwa Mfano Duka la mangi, Glocery ya vinywaji, Stationery etc. Katika kundi hili wote mnalipa.sawa bila kujali volume ya mauzo.

Ili kuondokana na tatizo la makadirio basi unaondoka kwenye hilo kundi la presumptive taxpayer unaanza kutunza hesabu.

2. Kunawafanyabiashara wanatoa risiti lakini hawatumzi hesabu. Hawa pia wataangia kwenye kundi la kukadiriwa kodi. TRA watatumia data za mauzo yako kutoka kwenye mashine kukukadiria kodi. Kama unataka kuepukana na tatizo hili tunza hesabu na ulipe kile tu unachotakiwa kulipa.

Pia mfumo ulivyo ni kwamba utakadiriwa kulipa say laki 3 kwa robo mwaka. Lakini mwaka unapoishia unapeleka hesabu. Kama umelipa zaidi wanakurudiahia. Kama umelipa kidogo unamaliza kiasi kilichobaki.

Sasa matatizo makubwa yako kwa wafanyabiashara.
1. Hawatoi risiti hata kama wana mashine
2. Hawatunzi hesabu.

Hivyo.afisa wa TRA atakachofanya ni kukuhoji maswali, kuomba daftari kukadiria mzunguko.wa biashara na kukudiria kodi.
 
Mimi ni mtaalamu wa fedha na kwa mawazo yangu tatizo la kodi na TRA linaanza na uratatibu mbaya wa ukusanyaji wa kodi. Kuna kodi za aina mbili kubwa

1. Kodi za mauzo. Kwenye kodi hizi ambazo kwa ulewa wangu ni 18% mlipa kodi sio mfanyabiashara mfano mwenye duka. Mlipa kodi ni mnunuzi na mwenye biashara anatakiwa kuweka kodi pembeni na kuwapa TRA kisheria au kwa lugha ya kitaalamu hii kodi ni withholding tax. Sasa kuna watu wanafikiri mlipa kodi hii ni mwenye duka na imefika wakati mpaka wauzaji wanafikiri wenyewe ni walipa kodi hii kumbe sio hivyo mlipa kodi ni mnunuzi. Hivyo mfanyabiashara anauza kitu Tsh 1000 anatakiwa aweke kodi ya 18% na mnunuzi kulipa Tsh 1,180 na hiyo Tsh 180 hajalipa yeye ni mnunuzi na sio pesa yake.

2. Kodi ya mapato ni kodi za wafanyabiashara. Hizi ni kodi ambazo zinatoka kwenye faida ya biashara. Yaani baada ya mfanyabiashara kutoa matumizi yote na kubali na faidi kuna kodi anatakiwa kulipa ya mapato. Sina uhakika na % lakini inatokana na ukuwa na aina ya biashara. Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi.

Tatizo Tanzania ni hizo kodi za namba 1. Mtu wa TRA badala ya kukagua vitabu vya risiti anaenda kwa mfanyabiashara na makadirio. Sasa makadirio ya nini wakati sheria inataka kila mtu atoe risiti. Na kama kuna risiti basi kiasi cha kodi kinajulikana kuna haja gani tena kuwatuma wafanyakazi na makadirio. Sasa mfano risiti zinaonyesha kodi ambazo wateja wamelipa za kwenda serikalini ni Tsh 10M hawa mafisadi wa TRA wanakuja na makadirio ambayo hatujui yametoka wapi ya kodi ya Tsh 20M halafu wanamwambia mwenye biashara kwamba tupe Tsh 2M halafu lipa kodi Tsh 5M Hivyo serikali inapungukiwa Tsh 3M. Lakini kibaya zaidi mwizi huyo huyo bado analipwa pesa na mshahara wake kwenye hiyo Tsh 7M. Sasa kama nchi tutaendeleo vipi kwa utaratibu huu?

1. Serikali badilisheni utaratibu toeni ujinga wa makadirio
2. Wekeni sheria kali kwa wala rushwa
3. Wekeni sheria kali kwa wafanyabiashara watoa rushwa mfano toeni hongera kama mfanyabiashara akiweza kumleta mla rushwa
4. Wekeni utamaduni na onyo kwa utamaduni wa rushwa
Hii mkuu unaizungumzia wewe kama mtaalam ila ukija kwenye Biashara kama Kkoo kunakuwa na uhalisia mwingine.

MFanya biashara mkubwa anauzia wafanyabiashara wadogo bila risiti, mfanya biashara mdogo anapata faida ndogo ila mauzo makubwa hii ina inflate kodi anayotakiwa kulipa sababu hana risiti ya manunuzi, at same time kuna machinga na mawinga wanachukua mzigo kule kule anapochukulia mfanyabiashara mdogo mwenye Efd, wanauza kwa margin ndogo hivyo inabidi mwenye duka arespond, hapa ndo unakuta bidhaa ya 98,000 inauzwa 100,000 faida 2,000 tu, kule Tra inasoma ulipe kodi 18% ya 100,000 lakini mfanya biashara kapata 2000 tu inabidi mfanya biashara atafute alternative.

Ushauri wangu ni kila mtu alipe kodi haijalishi ni Machinga, winga, Page ya insta Etc watengeneze database watoe mambo ya 18% kwa wafanyabiashara wadogo bali kuwe na kodi fixed kwa kila bidhaa, mfano Box la wall tiles linajulikana linanunuliwa 13,000 inauzwa 15,000 basi inakadiriwa kodi maybe 300 kila box, ukiuza box 10 kuwe na 3,000 ya Tra na iandikwe kwenye risiti ama mahala husika wote mfanya biashara na mteja wajue.

Then kuwe na wallet unamalizana na Tra instant, umeuza box 10 una generate control no hapo hapo unalipia ama mwisho wa siku unalipa like that, mfanya biashara kulipa 5000 ama 10,000 Tra kila siku na kuja kutoa 500,000-1M kwa awamu ni tofauti.
 
Ninarudi palepale suluhisho ni kila mmoja kutoa risiti. Ukiwa na mfumo ambao kuna watoa risiti na wasiotoa risiti apo una tatizo. Cha kwanza kabisa kila waazaji watakiwe kutoa risiti bila hivyo mfumo mzima wa kodi matatizo hayataisha. Machinga akiuza kitu kwenye bei inatakiwa kuwepo kodi na hiyo kodi sio pesa ya machinga bali ni pesa ya serikali.
 
Haya wafanyabiashara pia hukutana penalties sababu ya mifumo yetu ya ulipaji Kwa mfano mtu keshafika TRA awamu ya january hadi march kwenye makadirio alilipa umemkadiria Kwa kiwango atalipa kila miezi miwili au mitatu atalipa kias fulani basi ile control namba Kwa mwaka husika atumie hiyo hiyo kama itawezekana ili kuepuka safari za mara Kwa mara, au mfano kila ukifika muda wa kulipa atumiwe meseji ya control namba yeye popote alipo hata Kwa simu yake alipe ili kuepuka foleni kila wakati na sijui hua wanadhani mtu akifungua biashara lindi basi anaishi lindi tu hadi anakufa, kama wanaweza kutuma meseji za kuwatakia heri ya eid na pasaka na mwaka mpya Kwa nini control namba wasitume Kwa meseji?
Mbona wanasema control number unaweza kutengeneza wewe mwenyewe tu ofisini kwako? Ile kwenda ofisi za TRA ni kupenda tu.
 
Ninarudi palepale suluhisho ni kila mmoja kutoa risiti. Ukiwa na mfumo ambao kuna watoa risiti na wasiotoa risiti apo una tatizo. Cha kwanza kabisa kila waazaji watakiwe kutoa risiti bila hivyo mfumo mzima wa kodi matatizo hayataisha. Machinga akiuza kitu kwenye bei inatakiwa kuwepo kodi na hiyo kodi sio pesa ya machinga bali ni pesa ya serikali.
Haiwezekani kila mmoja atoe risiti wakati kuna loophole ya Machinga na winga, njoo field utaona hio issue haitekelezeki.
 
Back
Top Bottom