ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 44,199
- 50,920
Rais Samia amesema pamoja na kutoa Maelekezo Kwa TRA wasichukue Kodi za Dhuluma ila anasikitika kwamba wafanyabiashara ndio wamekuwa Wanaidhulumu Serikali Kwa kukwepa Kodi.
Samia amesema watu hawatoi risiti na wengine wanatoa risiti pungufu ya mzigo halisi.
---
Rais Samia Suluhu Hassan amesema licha ya yeye kukataa kodi za dhuluma kutoka kwa wafanyabiashara lakini wafanyabiashara ndio wamegeuka na kuanza kudhulumu kodi ya Serikali.
Akizungumza wakati wa Baraza la Eid El Fitr kitaifa mkoani Dar es Salaam Rais Samia amesema, ameamua kutumia Jukwaa hilo la Baraza la Eid kuwakumbusha wale wote ambao wanatumia mbinu chafu kukwepa kodi za Serikali na kudhohofisha utoaji wa huduma za kijamii.
"Nilipomuapisha Kamisha mkuu wa TRA nilimpa maelekezo kuwa sitakubali kodi za dhuluma na huo ndio msimamo wangu. Lakini cha kushangaza kwa sasa wamegeuka wafanyabishara wasio waaminifu wameanza kudhurumu kodi ya Serikali kwa kutumia njia za ujanja ujanja", Amesema Rais Samia na kuongeza kuwa
"Katika dini yetu pia kuna wafanyabiashara ambao wanatumia njia zisizo halali kukwepa kodi ya Serikali na ndio maana nimeamua kusema hapa ili wajue hata maandiko ya dini yanaelekeza kuhusu kulipa kodi".
My Take
TRA rungu Hilo hapo,mshindwe wenyewe Mfanyabiashara sio wa kucheka nae ,hapendi kulipa Kodi.Mama Rudisha task force maana Kwa Sasa Uchumi umekuwa sana lakini mchango wa Kodi Kwa wafanyabiashara ni mdogo haulingani na uhalisia.