Mimi ni mtaalamu wa fedha na kwa mawazo yangu tatizo la kodi na TRA linaanza na uratatibu mbaya wa ukusanyaji wa kodi. Kuna kodi za aina mbili kubwa
1. Kodi za mauzo. Kwenye kodi hizi ambazo kwa ulewa wangu ni 18% mlipa kodi sio mfanyabiashara mfano mwenye duka. Mlipa kodi ni mnunuzi na mwenye biashara anatakiwa kuweka kodi pembeni na kuwapa TRA kisheria au kwa lugha ya kitaalamu hii kodi ni withholding tax. Sasa kuna watu wanafikiri mlipa kodi hii ni mwenye duka na imefika wakati mpaka wauzaji wanafikiri wenyewe ni walipa kodi hii kumbe sio hivyo mlipa kodi ni mnunuzi. Hivyo mfanyabiashara anauza kitu Tsh 1000 anatakiwa aweke kodi ya 18% na mnunuzi kulipa Tsh 1,180 na hiyo Tsh 180 hajalipa yeye ni mnunuzi na sio pesa yake.
2. Kodi ya mapato ni kodi za wafanyabiashara. Hizi ni kodi ambazo zinatoka kwenye faida ya biashara. Yaani baada ya mfanyabiashara kutoa matumizi yote na kubali na faidi kuna kodi anatakiwa kulipa ya mapato. Sina uhakika na % lakini inatokana na ukuwa na aina ya biashara. Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi.
Tatizo Tanzania ni hizo kodi za namba 1. Mtu wa TRA badala ya kukagua vitabu vya risiti anaenda kwa mfanyabiashara na makadirio. Sasa makadirio ya nini wakati sheria inataka kila mtu atoe risiti. Na kama kuna risiti basi kiasi cha kodi kinajulikana kuna haja gani tena kuwatuma wafanyakazi na makadirio. Sasa mfano risiti zinaonyesha kodi ambazo wateja wamelipa za kwenda serikalini ni Tsh 10M hawa mafisadi wa TRA wanakuja na makadirio ambayo hatujui yametoka wapi ya kodi ya Tsh 20M halafu wanamwambia mwenye biashara kwamba tupe Tsh 2M halafu lipa kodi Tsh 5M Hivyo serikali inapungukiwa Tsh 3M. Lakini kibaya zaidi mwizi huyo huyo bado analipwa pesa na mshahara wake kwenye hiyo Tsh 7M. Sasa kama nchi tutaendeleo vipi kwa utaratibu huu?
1. Serikali badilisheni utaratibu toeni ujinga wa makadirio
2. Wekeni sheria kali kwa wala rushwa
3. Wekeni sheria kali kwa wafanyabiashara watoa rushwa mfano toeni hongera kama mfanyabiashara akiweza kumleta mla rushwa
4. Wekeni utamaduni na onyo kwa utamaduni wa rushwa